Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Sijawahi/Sidhani kama kutakuwa na Rais atakayepata shida katika kuongoza Nchi kama Magufuli. Anyway bado mapema sana kusema na huu msiba wa Taifa.
 
Mungu kwa rehema zake, na atupe utulivu wa ndani na furaha tena......Bwana asipoujenga mji, ajengaye afanya kazi bure.
.
 
habari wadau..

naona watu wote wanaonizunguka hawana furaha kabisa ni kama watu waliokata tamaa..

nikiangalia status za watu social network, ofisini, kwenye dala dala.. na hata mtaani kwangu watu wapo kimyaaa wana huzuni tele..

hii ni changamoto kubwa sana kwa magufuli kufanya kazi kwa bidii kurudisha furaha kwa mamilion ya watanzania...

kiukweli leo ni kama kuna msiba wa taifa

Hayo ni macho yako tu hayaoni vizuri. Nenda ccbrt
 
Kwa sisi wenye imani Fulani huwa tunasema wananchi wakilaani nchi yao hata aje nani nchi haitakuwa na maendeleo kwa magufuli hata afanye vipi nchi haiwezi songa maana tumeshailaani mpaka tuje kuitengua hio laana
Na hip laana itaondoka tu pale tutakapo kuwa na imani na mtu atakayetuongoza nb "haki huinua taifa Bali dhambi ni aibu ya watu wote "
Mungu hawezi kulaani kwa kushindwa kulichaguwa jizi fisadi lililotubia nchi yetu.
 
Sasa wew unategemea kwamba hao chadema wenzio walio kuzunguka wafurahi kuchaguliwa kwa magufuli?
 
Sema sina furaha. Mimi sijalala na wenzangu leo tumekesha kusherehekea ushindi wa tingatinga.

Hata kipindi cha Sodoma na Gomola watu wali kesha na kusherehekea kama Ninyi. Lakini sikiliza maneno yanayo semwa na watu hapa kwani Mungu hutenda haki kwa njia nyoofu. Kama CCM imeshinda kwa Ushindi wa haki Taifa hili lita simama Imara. Lakini kama watanzania wali shinda kwenye jua na mvua na kutembea kwa miguu na wengine kutumia hata kile kidogo walicho nacho na kukesha kwa imani wakijua wana kwenda kumchagua Rais wampendaye na haki hiyo ikaenda kuchukuliwa kwa dhuruma Basi mwenyezi mungu atakwenda kuwajibu.
 
Poleni sana ukawa jahazi lenu limezama jipangeni upya msirudie kuwapaka wanja mafisadi sisi wananchi tumewapaka pilipili pokeeni salamu zangu za rambirambi

Waache wachochee kuni mbichi ili ugali uivee
 
Mmegeuka wapiga ramri, lakn duwa zenu ni uongo coz mlitangaza ushindi wa lowasa bado amepigwa
 
Hata kipindi cha Sodoma na Gomola watu wali kesha na kusherehekea kama Ninyi. Lakini sikiliza maneno yanayo semwa na watu hapa kwani Mungu hutenda haki kwa njia nyoofu. Kama CCM imeshinda kwa Ushindi wa haki Taifa hili lita simama Imara. Lakini kama watanzania wali shinda kwenye jua na mvua na kutembea kwa miguu na wengine kutumia hata kile kidogo walicho nacho na kukesha kwa imani wakijua wana kwenda kumchagua Rais wampendaye na haki hiyo ikaenda kuchukuliwa kwa dhuruma Basi mwenyezi mungu atakwenda kuwajibu.
Kwani ni lazima watanzania wote tuipende Chadema? Nyie vipi
 
Mnajifanya mnasikitika hapa? Hivi mnajuwa Sana lowasa kuliko sisi tulioamua kumkataa? Wananchi wamekataa kuongozwa na fisadi lowassa basi.maamuzi ya watu yaheshimiwe.siyo lazima watu wote tumpende lowassa. Nawauliza angekuwa anagombea kupitia ccm mngemchaguwa?
 
Ebu tuache kumtengenezea mazingira ya kushindwa rais wetu mteule.Tumuombee arudishe matumaini kwa watanzania wote bila kujali vyama vya siasa
 
Kazi kubwa inayotakiwa ni kutimiza ahadi alizotoa
 
habari wadau..

naona watu wote wanaonizunguka hawana furaha kabisa ni kama watu waliokata tamaa..

nikiangalia status za watu social network, ofisini, kwenye dala dala.. na hata mtaani kwangu watu wapo kimyaaa wana huzuni tele..

hii ni changamoto kubwa sana kwa magufuli kufanya kazi kwa bidii kurudisha furaha kwa mamilion ya watanzania...

kiukweli leo ni kama kuna msiba wa taifa

Uko wapi KLM Au ARUSHA??
 
baada ya taarifa ya Libovu kutangaza kwamba mchoma nyavu ndio kaibuka kidede..
nilishuhudia baadhi ya kina mama wakishindwa kujizuia na kububujikwa na machozi..
wazo lililonijia kichwani niliwaza kwamba haya yatakua machozi ya furaha.
sijui nilipatia ?
 
labda uko kwenye vijiwe vya bodaboda walikoahidiwa mafuta ya bure kila mwezi, maofisi ya serikali watu wana furaha sana
 
totaona nikisikia mtu analalamika kuhusu kuonewA au maisha magumu au dawa hakuna au mshahara umechelewa.. jibu ni....hapa kazi tu na tuliza kalio dawa ikuingie vizuri...mie pia sina furaha hata kidogo
 
baada ya taarifa ya Libovu kutangaza kwamba COLOR=RED]mchoma nyavu ndio kaibuka kidede..[/COLOR]
nilishuhudia baadhi ya kina mama wakishindwa kujizuia na kububujikwa na machozi..
wazo lililonijia kichwani niliwaza kwamba haya yatakua machozi ya furaha.
sijui nilipatia ?
Ni kweli mkuu maana fisadi eddo angeturuhusu kuvua kwa KOKORO NA BARUTI Alituahidi
 
Back
Top Bottom