Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Kama ile nguvu na rafu zote zilizotumiwa na mabepari wa hii nchi kwenye uchaguzi zingetumika katika kuleta maendeleo basi ndani ya miaka kumi tu Tanzania ingekuwa mbali sana kiuchumi,lakini waapi hilo haliwezi kutokea.mkiwa na maendeleo na elimu mtawapa watawala wakati mgumu kwahyo inabidi tu muendelee kuwa makapuku.hivi kuna mtu yoyote mwenye akili tu ya kawaida anayeweza kuamini kama uchaguzi huu ulikuwa huru na wa haki?.
 
Kama ile nguvu na rafu zote zilizotumiwa na mabepari wa hii nchi kwenye uchaguzi zingetumika katika kuleta maendeleo basi ndani ya miaka kumi tu Tanzania ingekuwa mbali sana kiuchumi,lakini waapi hilo haliwezi kutokea.mkiwa na maendeleo na elimu mtawapa watawala wakati mgumu kwahyo inabidi tu muendelee kuwa makapuku.hivi kuna mtu yoyote mwenye akili tu ya kawaida anayeweza kuamini kama uchaguzi huu ulikuwa huru na wa haki?.



Ukiona hadi Tume ya haki za Binadamu LHRC, inavamiwa na Police, kwa nguvu na amri ya kutoka juu, yaani Viongozi wa Dola... na kunyanganywa, BASI HIYO SERIKALI NI YA DOCTATOR...!!!

Wizi mkubwa sana wa Kura umefanyika..!!😨😨
 
Nchi iko kwenye matatizo tunafurahi nini? Kila mtu aendelee na majukumu yake, subirini mechi ya simba na yanga mkafurahie uko.
 
Mungu yuko upande wetu sisi tunaoteseka na mfumo mbovu wa utawala wa CCM.Hakika siku zote haki haipotei ila hucheleweshwa tu.LOWASA ndiye Rais wetu Watanzani tuwe watulivu muda si mlefu hili litakuwa wazi.
 
Habari wadau.

Naona watu wote wanaonizunguka hawana furaha kabisa ni kama watu waliokata tamaa.

Nikiangalia status za watu social network, ofisini, kwenye dala dala.. na hata mtaani kwangu watu wapo kimyaaa wana huzuni tele.

Hii ni changamoto kubwa sana kwa magufuli kufanya kazi kwa bidii kurudisha furaha kwa mamilion ya watanzania.

Kiukweli leo ni kama kuna msiba wa taifa.

Mlijidanganya kabla ya uchaguzi, mwaendelea kujidanganya na sasa baada ya uchaguzi. Tangu lini NCHI imekuwa mtaani kwako? Umezunguka kila kona ya Tanzania na kuona watu hawana furaha? Na hata kama hawana, umewauliza kwanini hawana furaha? Mlifanya madudu kwenye process ya kupata mgombea urais, mmevuna mlichopanda. Mwaweza kuendelea kunung'unika milele au kukubali hali halisi.
 
Hukumu ya yote yaliyofanyika gizani katika uchaguzi wa mwaka huu ni katika siku ya kiyama.
 
Haya mambo mawili yananichanganya kuporwa kura na kushutumu kanda ya ziwa kuwa wamepiga kura za kikabila sijaelewa bado lipi ni sahihi au yote mawili?watu wa dodoma na singida wamesemwa kwa umasikini wao ndo umechangia wapige kura kwa ccm nabaki kuchanganyikiwa kipi ni sahihi kwa nia njema mnijuze.
 
Kwa mara ya kwanza nimejikuta naichukia Tanzania!!! Sina furaha ndani ya nchi yangu.
 
Awali tuliitwa malofa.

Leo tumeitwa wanya viroba.
 
All we do is win, No matter what!

Hata Mungu kasema shetani ana mwisho wake japo mpaka leo anatutesa humu duniani. Tunachoamini ni kwamba yoote mliyofanya yana mwisho wake.
Homgereni, acheni sisi tuendelee kuumia ndani ya nchi yetu pendwa.
 
Jamani m nauliza hivi nini kimewakumba watanzania hasa siku ya leo? Maana naona mitaa iko kimya watu wamejawa na simanzi kuu badala ya kuwa na furaha
 
Siyo kweli. Mi mbona nina furaha kubwa tu.
We jisemee kivyako kwamba huna raha na siyo kwa wote. HAPA KAZI TU
 
Wanaomboleza miaka mitano mingine ya dhiki na ulaghai wa CCM.
 
Demokrasia imebakwa.Utawala wa kimabavu umechukua nafasi.
 
utoto mwingine raha sana

furaha itoke wapi wavivu, wezi, waliofoji vyeti mashaka matupu kaja jamaa kuwaadabisha

mlitaka apite goi goi mshangilie kula raha wakat hamfanyi kazi

Hata huku Ulaya wapo wanao kula raha bila kufanya kazi. Yaani ukiwa unafanya kazi Ulaya nyuma yako umebeba mzigo wa Jobless guys 5 ama walevi flani hivi. Nakushangaa wewe unaye shangaa watu kufurahia au kula raha wakati hawafanyi kazi!! Au hujui kwamaba hata Royal Family wana kula maisha ya kiRoyal kwa kodi za wamatumbi walio jazana pale UK.

Uwe una tafuta habari kabla ya kutoa taarifa usizo zijua. Gamba wewe!!
 
Back
Top Bottom