Kwanza nianze kwa kuikiri imani yangu kuwa mimi ninaamini katika Biblia na nitatoa mifano yangu kutoka katika kitabu hiki kitakatifu.
KWENYE BIBLIA IMEANDIKWA
"Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua."..... MITHALI 29:2
"Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi; Bali waovu waondokapo, watu hujificha."..... MITHALI 28:12
......Ni huzuni kubwa imetanda katika Taifa baada ya haki na maamuzi ya wapiga kura walio wengi kuporwa, demokrasia na uhuru wa kuchagua kuuwawa na kufanywa kuwa danganya toto kwa ajili ya kuficha maovu ya watawala na watu wachache wanaonufaika na kutajirika na utajiri wa taifa huku wananchi walio wengi wakiendelea kuwa masikini na kuteseka.
........Ni huzuni nchi nzima baada ya watanzania kuporwa matunda ya mabadiliko waliyoyahangaika kwa miaka mingi. Ushindi aliopewa mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. John Pombe Magufuli umeoneka kuwaumiza watanzania wengi sana. Nchi imejawa na huzuni, kila mtu anasononeka kila kona ya nchi.
Mabadiliko waliyokuwa wanayahitaji wananchi walio wengi yameporwa kwa nguvu na vitisho na CCM, Jeshi la Polisi na Serikali.
Magufuli ametangazwa kuwa Rais lakini ni rais wa manung'uniko na maumivu ya watanzania.
Nchi imekuwa ukiwa kama mtoto yatima aliyekosa msaada. Nchi imejawa na huzuni kila kona, hakuna shangwe wala furaha machoni, usoni wala kwenye mioyo ya watanzania.
Wananchi wameogopeshwa na kutishwa kuwa wakidai haki yao watauwawa, watapigwa virungu, watamwagiwa maji ya kuwasha na hata kufungwa jela LAKINI ni nani atakayewaokoa watanzania hawa waliotawanyika huku na huko kwa hofu na uoga kama kondoo waliokosa mchungaji jangwani huku wakiwindwa na simba?
Magufuli sio chaguo la Watanzania wengi waliojitokeza kupiga kura na kutaka mabadiliko. Magufuli ametajwa kuwa Rais wa wananchi wasiokuwa tayari kuongozwa naye ila kwa hofu ya kupigwa na kuteswa wamenyamaza na kukubali kuumia ndani ya mioyo yao.
Mungu anasikia sauti za maumivu ambazo huwa hatuziongei. Sheria ya Mungu ipo wazi ya kuwa "MTANYAMAZA NAMI NITAWAPIGANIA" kwahiyo watawala wetu wanapoona tumenyamaza wasifikiri ndio mwisho ila watapambana na ghadhabu ya Mungu muda si mrefu.
CCM unayoiona leo HUTAIONA TENA.
Magufuli unayemuona leo HUTAMUONA TENA.
Mungu aliporuhusu wanadamu wajichagulie viongozi wao wenyewe sio kwamba aliamua kuwasusa wanadamu na kuamua kuwaacha kabisa, LA HASHA! Ndivyo itakavyokua, Mungu hajawatupa watanzania, anayasikia majonzi, huzuni na vilio vya watanzania wengi.
TANZANIA MPYA INAKUJA.
Mh. Edward Ngoyai Lowassa ndiye Rais wa nchi mpya ya Tanzania ambayo wananchi wengi wanaamini katika mabadiliko wamekuwa wakiisubiri kwa shauku kubwa.
Watanzania, msiogope huu ni muda wa mambo yasiyowezekana kuwezekana. Hakuna uchaguzi uliokuwa umejawa na ndoto nyingi kama huu wa mwaka huu.
Wazee waliota, vijana waliota na watoto pia waliota na wakasema walichokiota na kuandika chini ya kuwa Lowassa ndiye atakuwa Rais wa nchi hii. Hakika ndoto ni BAYANA na MUNGU HADHIHAKIWI.
"Kilichotoka kwa Mungu hakuna mwanadamu wa kukizuia ila kitacheleweshwa kidogo tu kufikia malengo yake"
TANZANIA MPYA INAKUJA.