Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Nchi haina furaha kabisa, kwa maoni yangu

Mwenyewe nilitegemea watu watakuwa na Ndelemo lakini imegeuka kinyume
 
Mmewasaliti majembe kina Slaa mkategemea mtapewa nchi kwa dizaini hiyo,na pale ndipo mlipopoteza mvuto majinga kabisa! Ndipo mlipopoteza hizo raia mil 2.8 na usheee

Leo hii Slaa amegeuka kuwa jembe kama ni hivyo mbona hamkumpa kura mwaka 2010 unafiki ni kitu kibaya
 
Nipo Mikocheni saiv ni shangwe la hatari, jioni Kino ilikuwa amsha popo.. Ukawa ndio wapo kwenye majonzi maeneo ya kimara kina manka wanalia toka asubuhi.

Uzuri rais tuliyempata hana aja na kuuza sura yeye ni kazi tu. Mnune mpasuke Magu ndo president.
Umeongea kishabiki sana bila kutafakari, hivi huyo unayesema yeye ni hapa kazi tu anaweza kufanikiwa bila ushiriki wa wananchi anaowaongoza?
 
itabidi nitafute uraia wa nchi ingine naona hapa siwezi

mmbaki na tanzania yenu
 
Kura hazipigwi kwenye social medias.

We vipi, kwani huko mtaani ambapo uhalisia wa huzuni unaonekana nako ni social media!? Bisheni tu kwa ubabe wenu lakini vyombo vya habari jana vimeonyesha sehemu mbalimbali tz watu wakiwa na huzuni. Kwa jana tv zilionysha furaha ni Geita, sijui kwingine.
 
Jamaa wamevaa kofia za ccm wanapita kariakoo wanaelekea lumumba,hawajiamini kabisa,wanahisi kama watavamiwa vile....
 
Ni kweli kabisa nchi imejaa huzuni kuu. Hata wachache wanaoshangilia wanafika mahali wanaona aibu inabidi waache. Kama hakuna haki huwa hakuna amani. Kumbuka utulivu si amani
 
mda si mrefu MAGUFULI Atalijua tatizo la TZ nini? mafisadi waliompandisha hapo watamzuguka akigusa maslahi yao.yeye ni km kondoo kwenye kundi la mbwa mwitu
 
Duuh! Mvua ghafla tu katika jiji la Dar na sio ndogo. Wingu limetanda. Baraka?
 
Mimi ninasema nanitasema..Alaaniwe JANUARY MAKAMBA KWA KIPIMO ALICHOPIMIA WATANZANIA JAMII YANGU...January ulaaniwe na kwa kipimo hichohicho tena chakusukwa sukwa ndicho utakachopokea siku za usoni....January ulaaniwe kwa uratibu ulioufanya kwenye sekta ya mawasiliano mpka mkafanikiwa kukwapua haki za wavuja jasho...km Mungu aishivyo,haki haitapotea,KAMA KURA ZOTE MLIPATA KIHALALI BASI NA IWE BARAKA KWENU KM MTAJI WAKUBARIKIWA KTK MWANZO WENU...LKN KM MLIPATA USHINDI KWA HILA YEYOTE JANUARY MAKAMBA NAWENZAKO NASEMA KURA ZETU NAZIWE LAANA JUU YENU NA ipatilizwe kizazi chenu chote..
Na Mungu aketiye mahali pa juu palipo inuka awape upofu wa macho, kansa ya damu, wazibe njia ya mikojo, wazibwe masikio, wanyong'onyee na walegee kabisa. Wataongoza nchi hii wakiwa hawana amani. Toka lini mtu akawa na amani na kitu alichokiiba? Walaaniwe saba mara sabini!
 
Kiza kimetanda kwenye mioyo ya watanzania wengi...wengi wanadhani hawakutendewa haki kabisa...poleni watanzania,poleni sana!!
 
Ni kweli kabisa nchi imejaa huzuni kuu. Hata wachache wanaoshangilia wanafika mahali wanaona aibu inabidi waache. Kama hakuna haki huwa hakuna amani. Kumbuka utulivu si amani

Nilikuwa bar moja kkoo jana ikiingia mijimama minne ikishangilia Magufuli, watu wakawa bize na bia zao, ikabidi ione aibu ikaacha na kuendelea kunywa bia zao kwa ukimya.
 
Kweli mpaka maofisini tena ofisi nzito furaha zilianza kutoweka tangu Matokeo ya wizi yakijumlishwa. Ni majonzi.

Watu hawana amani kwa sababu the " Bullidozzer" atafyeka michongo yote ya Ofisini, walitegemea yule mpiga dili ataingia Ikuru waendeleze michongo yao, kiama cha wapiga dili kimewadia. ndo maana hakuna furaha.
 
Habari wadau.

Naona watu wote wanaonizunguka hawana furaha kabisa ni kama watu waliokata tamaa.

Nikiangalia status za watu social network, ofisini, kwenye dala dala.. na hata mtaani kwangu watu wapo kimyaaa wana huzuni tele.

Hii ni changamoto kubwa sana kwa magufuli kufanya kazi kwa bidii kurudisha furaha kwa mamilion ya watanzania.

Kiukweli leo ni kama kuna msiba wa taifa.
Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa wananchi wake kutokuwa na furaha kabisa. Sasa ndio wameongezewa huzuni kuu. Kweli inakatisha tamaa na wakati mwingine ni bora kusiwepo uchaguzi mkuu kwani pesa inapotea bure wakati watawala wanajua nani atakuwa mtawala. Nahisi uchaguzi ujao wengi hawatapiga kura na mimi nikiwa mmoja wapo. Kuna haja gani ya kwenda kupiga kura ambayo itachezewa? Mimi mpaka leo nahangaika kusafisha wino kwenye kidole changu ingawa wakati wa kupiga kura nilipiga kwa furaha na matumaini makubwa. Furaha yangu imegeuka kuwa huzuni na msiba mkuu. Kama ingekuwa huru na haki hakuna neno. Lakini kwa kila jambo kuna malipo yake. Wasubiri malipo ya vilio vya watanzania wengi.
 
Mkuu.sisi wapenda Demokrasia na maendeleo tumeumia sana. Maana maamzi wa Wengi ya mezikwa na kundi la wafisadi wachache tu.
 
Hii nchi Ina wenyewe, na wenye nchi ni CCM, haakuna cha haki Wala sheria ni dola inatawala na ubabe...

Lowasa asitegemee any change.... CCM ikiangua ni aibu kwa wengi wapo watakao kimbia nchi na hii haitokaa itokee

Kila mtanzania ale kwa urefu wa kamba yake.....Basi.

Democrasia iliyo huru ni ndoto
Sikupiga kura mwaka huu na sitokaa nipoteze Muda eti nikapige kura.....

Tanzania Oye
 
Wakati wa kutafakari huu na kisikiliza baade furaha na shangwe kwa kupongeza mshindi wetu
 
Back
Top Bottom