Nchi 10 zinazoongoza kwa ubaguzi duniani

Nchi 10 zinazoongoza kwa ubaguzi duniani

Ubaguzi upo kila mahali mkuu, nitakupa miafano michache:
1. Hospitalini wagonjwa mahututi wanabaguliwa kwa kuwekwa katika chumba chao maalumu kinachoitwa I.C.U. Pia wagonjwa wa kifua kikuu wanabaguliwa kwa kulazwa katika wodi yao pekeyao. Hapo sijamaliza na akina mama waliojifungua.

2.Jeshini kuna ubaguzi wa vyeo hivyo maofisa wana mess (Sehemu ya kulia chakula) yao pekeyao na hivyo kuwatenga wasio maofisa.

3.Nyumbani kwenu / kwako mgeni akikutembelea na kuisha hapo hata kwa mwaka mmoja hawezi kupata haki zote sawa na wewe au wanafamilia wengine aliowakuta hapo hivyo kuna vitu fulani ataruhusiwa kufanya lakini vingine atakatazwa kwa kuwa ni mgeni tu.

4.Kwenye vyoo vya umma kuna vya wanawake pekee na vya wanaume pekee, huu pia ni ubaguzi.

5.NK
Mkuu nimeipenda sana signature yako ..unasema ujanja ni sawa..lakini ujanjaujanja haukubaliki!!Hahahahaaaaa....
 
-Niweke Sawa hapo kwanza.
Chogo hupenda kuita mtu yoyote wa Bara,ukisikia Chogo ujue ni wa Bara,wakina na maana kwamba Asili ya Watu wa bara vichwa vyao ni Vichogo.
-Kuhusu Guest inategemea ulienda Vipi,wakiona umekaa kihatari hatari hata Dar hawawezi kukupa
Pale Adams Inn kwanza sio watu wa kuhoji Saana,maana Pale ni Bandarini,ila usalama wa kila mgeni ni juu yao.Na ndio maana inabidi wakuulize kama mgeni wa kawaida wakati wa kucheck in na kama wana daubt basi watakuuliza masuali ya Ziada
Utakumbuka kwamba pale Adams Inn kuna Guest inaitwa Malindi inaelekezana na Adams Inn,kuna jamaa alikuja haeleweki,akakodi chumba,na chumba chake alilocate chumba kilichopo juu ya Duka la Sim,basi ailipofika usiku,akaja na wageni wake,wakaingia room kumbe walienda kutoboa zege na kudongokea kwenye duka la sim na kuiba simu kibaooo.Sasa hadhari ni muhim mkuu
Ila Guests Houses na sehem zote za kulaza wageni hazina ubaguzi,na ifahamike kwamba ubaguzi mwingine ni wewe baada ya kujishuku.Watakubagua vipi wakati wana Room`s Rates za Foreigners na Resident.
ATM ya Umoja,kwanza kama unauliza bila kusalimia hatamie sikujibu.
Ila vijana wa Pale forodhani ni Wastaarabu wengi wao,wewe ungeuliza hata Driver Tax angekuelekeza,sasa kama umeenda na mbwembwe zako kama Bill Gate na kuuliza tu watakuzingua tu lazima,na unabahati wanatabia ya kuku locate mbaliii kama ukifanya madharau.
Kuhusu kumuuliza huyo Mama,ni kwamba hata vijana wa kawaida wangpata tabu kukujibu ilipo ATM ya UMOJA,wewe mama anauza maandazi unategemea mambo hayo ya Bank.Huyo mama hata neno ATM halijui maana yake,anajua,usilaumu kila kitu mkuu,lazima uendane na uhalisia,ni ATM Chache sana za Umoja na almost kama zote zipo chini ya PBZ(People`s Bank of Zanzibar)
Kuhusu kuambiwa Camera haizwi,hii ni umetia chumvi nyingi saana,inawezekana ikawa hauzwi kweli,maana sio kila kitu ukiona dukani kinauzwa,na Wafanyabiashara wanaangalie sana hela,sio salam yako,sasa Suala la Kusalimia ni kuonyesha uungwana tu,ila sio kwamba linafanya mtu asikuuzie Bidhaa
Overall
Inaonekana hata wewe mwenyewe ni Mtata,kwanini yote yatokee kwako?

Nini kinakufanya ufikiri kuwa ninaweza kumuuliza mtu njia bila kumsalimia? Usije ukadhani mimi nimezaliwa Congo au Peru, mimi nimezaliwa Dar es Salaam, na nimekulia na kusoma hapa kwa hiyo sitarajiwi kukosa hekima kiasi nimuulize mtu miswali kibao bila salamu, hata mimi ukiniuliza bila salamu sitajibu.

Kuhusu vyumba vya hoteli, kwangu mimi ule ni upuuzi. Nimekuja hotelini kwako, unaniambia vyumba vimejaa, at the same time unaadmit wazungu, any way labda sababu za kibiashara lakini kuna namna ya kum-turn mtu sio kumpa makavu as if tulihitilafiana hapo zamani ilhali hatujuani ndio leo tunaonana.

Kuibiwa duka la simu siku moja hakumfanyi mtu muungwana kumshuku kila anayekatisha mbele. Tena kuna sehemu umetanabahisha juu ya mtu kuwa na muonekano wa 'hatari hatari', ukiashiria pengine ni appearance yangu imewafanya wanitilie shaka. My friend, unajua GAIDI anafananaje?

Nilipoambiwa nijifunze kusalimia, haikumaanisha kuwataka hali niliowakuta dukani hilo nililifanya, suala pale SIKUWA NIMEVAA MAKUBAZI na SIKUSALIMIA SALAM ALEIKHUM. Na kuhusu kuambiwa kitu hakiuzwi, sio kwamba sikukinunua...nilinunua the same camera lkn kwa kupelekwa na mtu mwingine.
 
Mi sio mjinga kama wewe.Kabla ya kuja na kuanza kutoa mapovu kwangu inabidi ujipange kwanza.Nitakurudisha huko kubaya ulipotoka,tena kwa kupitia nyuma..Source nilizozitumia ni nyingi,chukua hiyo hapo= Most racist countries-Top ten list. Una jingine?

Ungekuwa mjinga kama mimi, ungekuwa na akili. Hujajibu swali la msingi, hapo unaleta bangi. Source inaweza kuwa GOOGLE? Ukiulizwa SOURCE ukataja gazeti, ni imani kuwa gazeti litakuwa limeresearch hilo jambo in question, wewe unaulizwa source unasema GOOGLE, umepiga ila kitu ya kujibia maswali bungeni nini?

Hapo ni sawa ya kusema Source = Meza ya Muuza magazeti
 
Sidhani kama hapa kuna Sababu ya kulumbana saana.
List imetajwa na Mwana Mtoka Pabaya ameeleza muono wake juu ya Zanzibar na amejibiwa na mie.
Sasa sioni kama ni baya sana,maana ukutoa post sio lazima kilichomo kwenye post tuu ndio kiongelewa,kuna vitu kama ziada tu vinaweza kuingia,unaweza kukuta post ya real madrid ukakuta hata Simba au Yanga imeingizwa,sasa ni vitu vya kawaida,sioni haja ya kutukanana,muhim iwe kueleweshana na kudhibit jazba zetu ili kutoa mwanga kwa wengine.
Maana hata hao wanaosema hivyo ni binaadam,wamefanya uchunguzi kwa kupitia madawati ya Vituo vikuu vya Polisi,ila je tujiulize ni kesi ngapi ambazo haziendi polisi za kibaguzi?na je wao wameupima vipi ubaguzi?kwa kusoma magazeti,au kupita mitaani,laaa,wao wametumia vyombo vya usalama ambapo sio 100% rank hiyo ikawa sawa.

Kwa akili ya kawaida huwezi ku I rank USA kuwa ya kwanza Badala ya German
 
Kuna wamerekani weusi,walizaliwa huko.Mbona hatuoni waarabu weusi kule kwao uarabuni wakati nao walijihusha vizuri na biashara ya watumwa?
 
Kuna wamerekani weusi,walizaliwa huko.Mbona hatuoni waarabu weusi kule kwao uarabuni wakati nao walijihusha vizuri na biashara ya watumwa?
Mkuu wale wa huko unaowasemea walikuwa wanaHASIWA,samahani lkn mkuu kwa kusema ukweli huu ambao unaweza kuwaudhi baadhi ya watu humu[emoji87] [emoji87]
Sidhani kama hapa kuna Sababu ya kulumbana saana.
List imetajwa na Mwana Mtoka Pabaya ameeleza muono wake juu ya Zanzibar na amejibiwa na mie.
Sasa sioni kama ni baya sana,maana ukutoa post sio lazima kilichomo kwenye post tuu ndio kiongelewa,kuna vitu kama ziada tu vinaweza kuingia,unaweza kukuta post ya real madrid ukakuta hata Simba au Yanga imeingizwa,sasa ni vitu vya kawaida,sioni haja ya kutukanana,muhim iwe kueleweshana na kudhibit jazba zetu ili kutoa mwanga kwa wengine.
Maana hata hao wanaosema hivyo ni binaadam,wamefanya uchunguzi kwa kupitia madawati ya Vituo vikuu vya Polisi,ila je tujiulize ni kesi ngapi ambazo haziendi polisi za kibaguzi?na je wao wameupima vipi ubaguzi?kwa kusoma magazeti,au kupita mitaani,laaa,wao wametumia vyombo vya usalama ambapo sio 100% rank hiyo ikawa sawa.

Kwa akili ya kawaida huwezi ku I rank USA kuwa ya kwanza Badala ya German
 
Mkuu wale wa huko unaowasemea walikuwa wanaHASIWA,samahani lkn mkuu kwa kusema ukweli huu ambao unaweza kuwaudhi baadhi ya watu humu[emoji87] [emoji87]
Sawa mkuu,ila wangekuwa wanahasiwa basi idadi isingekuwa kubwa namnahiyo,Kuna majimbo mtu mweupe unamtafuta,sasa ingekuwa wanahasiwa ingekuwaje?Kina Pididdy mbona wapo,Tyson,Rihanna,na wasanii maarufu almost wote weusie kina Jay Zee hao nk.
Hizi ni dhana tu,nakumbuka zamani watu walisema kwamba Dr.Kaunda alihasiwa kwanza kabla ya kumtibu malkia Elizabeth,aiseee
 
Hiyo case niliyokutajia iliwakumba wenzetu waliokwenda utumwani nchi za kiarabu ila wale waliokwenda nchi za marekani haikuwakuta ndio maana unawaona akina jay z,50 cent and the like.Hiyo ishu ya Kaunda mimi pia nimewahi kuisikia shuleni.
 
Binafsi naona badala ya kulalamika nasi tuwe wabaguzi zaid dhidi ya anayetubagua. Mimi binafsi ukinibagua tu bila kujali rangi yako nakubagua na kukudharau mara mia zaidi.
 
Ungekuwa mjinga kama mimi, ungekuwa na akili. Hujajibu swali la msingi, hapo unaleta bangi. Source inaweza kuwa GOOGLE? Ukiulizwa SOURCE ukataja gazeti, ni imani kuwa gazeti litakuwa limeresearch hilo jambo in question, wewe unaulizwa source unasema GOOGLE, umepiga ila kitu ya kujibia maswali bungeni nini?

Hapo ni sawa ya kusema Source = Meza ya Muuza magazeti
Mtu anapokuuliza source ina maana kuna kitu hajaridhika nacho au hakiamini katika andishi lako.Njia nzuri ya kujiridhisha ni yeye achukue hicho kitu agugu aone nilichoandika ni fake au ni kweli aje aniumbue hapa..
 
Mimi nimewahi fika Kenya, Marekani na Qatar, lakini sijawahi kubaguliwa huko. Mara pekee niliyowahi kubaguliwa maishani, nilienda Zanzibar.....sitaraji kwenda tena.

Waliniita chogo, sijui maana yake kwa kiswahili lkn nafikiri wanamaanisha kafiri. Kila guest house nilikoenda waliniambia vyumba vimejaa, mpk teja mmoja pale ferry akanipeleka Adams Inn, ndio nikalala hapo baada ya yeye kunisaidia kujieleza.

Asubuhi nilitafuta ATM ya UMOJA, nikamuuliza kijana mmoja pale Forodhani, akaniambia yeye sio kazi yake kuelekeza watu. Nilifanikiwa kusogea maeneo ya karibu na lilipokuwa soko la watumwa, kuna benki pale ya FBME, nikamuuliza mama mmoja akasema haijui na hajapata kuisikia. Baadaye FFU mmoja alinielekeza, kwa maajabu...ni jengo hilo hilo alilokaa huyo mama akiuza vitafunio.

Kama haitoshi, pale darajani niliona video camera ya mtumba inauzwa, nilipouliza bei nikaambiwa haiuzwi. Dalali aliniambia siku nyingine nijifunze kusalimia kistaarabu kama nataka kuhudumiwa.

Jamani, Waarabu wa Qatar ni wakarimu sijapata kuona. Americans hawana time na mtu. Usimuulize kitu Black America, atakujibu huku anaenda hata hutaelewa alichosema.
Nimesikitishwa sana na hili la Zanzibar mtu mweusi kumdharau mweusi mwenzake, ni tatizo kubwa...ni matatizo ya akili kwakweli..Yaani kweli slavery mentality imewakaa vizuri
 
Jamhuri ya kiislamu ya irani sasa cjui nimeropoka nn???
Jamhuri ni Nchi !? .......? unajua vigezo vya Nchi kuwa ni ya Kiislaam ?
Hata Korea ya Kaskazini inajiita Nchi ya Kidemokrasia (DPRK) Democratic Peoples Republic of Korea, ni kweli hao watu wana Demokrasi ?
melkiorysaranga Iran si Nchi ya Kiislaam na hata Uislaam wao ni wa Kishia ! (Kishia ni moja ya Madhehebu inayovuruga 'Doctrine' ya Uislaam)
 
Mkuu mimi cjaleta udini ni kweli hao watu wanaitwa wapersian na pia hiyo nchi yaitwa jamhuri ya kiislamu ya irani na ndio maana wapo katika umoja wa nchi za kiislamu OIC ila kunamdau hapo alipanic bure kwa ajili ya jina la ID hii pia mimi ni muislamu
.......Muislaam gani wewe usiye jua mambo madogo madogo kama haya ya Uislaam unazungumziaje kuhusu ubaguzi na Taifa lipi lenye vigezo gani ndilo unaloweza kuhukumu kuwa ni Taifa la Kiislaam !?
 
Jamhuri ni Nchi !? .......? unajua vigezo vya Nchi kuwa ni ya Kiislaam ?
Hata Korea ya Kaskazini inajiita Nchi ya Kidemokrasia (DPRK) Democratic Peoples Republic of Korea, ni kweli hao watu wana Demokrasi ?
melkiorysaranga Iran si Nchi ya Kiislaam na hata Uislaam wao ni wa Kishia ! (Kishia ni moja ya Madhehebu inayovuruga 'Doctrine' ya Uislaam)
Iran sio nchi ya kiislamu na hata uislamu wao ni wa kishia umesema sio nchi ya kiislamu then unasema uislamu wao wa kishia sasa hapo huoni kama huo ni ubaguzi???je uislamu halisi ni uislamu upi??mwisho uache itikadi kali
 
Back
Top Bottom