NBC Visa + MasterCard zaanza kugawiwa

Mkuu, mimi ni muislamu niliyesoma dini kidogo. Sasa nikukumbushe tu kuwa hizi zinazoitwa islamic bank ni majina tu kuwapata waislamu wafungue ac nk. Wanasema islamic kwasababu hawakupi riba. Lakini unapoenda kuchukua pesa zako au kuweka kwani huwa wanakupa zile zile au zozote zinazowekwa na wezi, wala rushwa, tbl nk (huu ni mfano tu, simaanishi kuwa wateja wote wana sifa hizo).
Pili mtaji wa bank umetoka wapi? Je wakikopana bank kwa bank hawalipani riba? Ambayo ndio inaendesha biashara zote za kibenki?
Tatu, sheria za bank kuhusu hisa wanazouza kwa sababu mbali mbali zinaendana na sheria za kiislamu?
Nne, je ukifungua islamic bank ukakopa kwao sh laki moja, utawalipa laki moja hiyo hiyo bila riba yeyote? (Hapana)
Tano, nani msimamizi wa miamala ya kiislamu katika bank hizo? (Niliuliza nbc hawakunipa jibu, kifupi hawana)
Sita, unapohifadhi pesa zako, hawazitumii katika mambo ambayo dini yetu imeyaweka katika kundi la vitu haramu? Kama vile kukopesha wengine kwa riba nk?
Saba, je islamic ac haihusishwi na WIZI wa banks kwa raia kutokana na charges mbali mbali zisizo na msingi. Imagine unaweka laki moja kwenye kabati yako halaf kila ukiifungua kutazama kama ipo ile laki inapungua sh 300 kwa kuitazama tu ili kuhakiki kama ipo. Hivyo ndivyo banks zinavyotufanya. Kucheki salio kwenye atm wanakucharge, kutoa pesa wanakucharge, mwisho wa mwezi wanakucharge. Khaa! Sasa hizo pesa wanazofanyia biashara ya kukopesha na kula riba haziwatoshi?
Kifupi hii ndio nchi pekee niliyowahi kuwa na ac ina charges za namna hii. Tz unaweza kuweka 100,000 mwisho wa mwaka ukakuta elf 5 ya kitabu, zote zimeenda kwenye charges.
Haya maswali na mengine mengi sana niliuliza pale kichele wakati nafungua ac wakashindwa kunipa majibu. Hata huyo islamic banking advisor wao hakunijibu lolote. Mwisho tuliishia kucheka tu (kuashiria ni usanii wa mabank kuwapata waislamu wasiotaka kufungua ac kwao waone wanaendana na sheria zao). Nikaamua kufungua tu ac ya hawaida.
Nimeridhika na majibu yako hapo mwisho uliposema baada ya kuuliza ulilza ukaamua kufungua tu.Unajua uislamu ni dini nyepesi na inayoendana na ubinadamu,huwa unalipwa kwa nia tu kabla kutenda jambo jema.Hivyo ulipoamua kufungua kwa nia ya kukwepa riba inatosha kujisafisha.Zaidi ni kwamba matawi mengi yana kopi ya sharia compliance certificate ambayo ukiiangalia ina sahihi za masheikh maarufu katika jamii.Sasa ikiwa wao kwa pamoja wametudanganya wewe huna jukumu.Kuhusu kukatwa pesa unapoangalia salio na mwisho wa mwezi kwangu na hasa kwa upande wa uislamu sioni kwamba ni tatizo.Sisi tunataka tumlipe mtu aliyetufanyia kazi sio kumhonga au kumgawia kutokana na jasho la watu wengine wakati mwenyewe kalala tu.

Nikimalizia,naona zipo dalili kwamba tangu NBC kufungua islamic accounts imepata faida sana na hata kabla ya kuanzisha corporate islamic accounts ukilinganisha na CRDB yenye utitiri wa wateja lakini mchango kwa pato la taifa wamepitwa sana na NBC.
 
Wazee wa mafeki/China nao wameanzisha card network yao inaitwa Cha Ching, wanataka ku-compete na Visa, Master Card, Discovery na American Express. Subirini hiyo nayo

Hiyo ya kichina unaingiza kwenye atm unataka euro 50 inakutolea euro 5!
 
Back
Top Bottom