Nayaona Maandamano katika ulimwengu wa kiroho

Nayaona Maandamano katika ulimwengu wa kiroho

maandamano

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2025
Posts
709
Reaction score
1,523
Mimi hupenda kuongea kiroho zaidi,nayaona maandamano tarehe 9,nakushauri ndugu yangu nunua mahitaji yako muhimu weka ndani,kuanzia vyakula maji dawa,hakikisha una Cash mkononi ya kukutosha ingalau kwa wiki 2
 
Watu wanakumbuka shaba za juzi unadhani watarudia kuchezea sharubu
Wengine huangalia ulimwengu katika ulimwengu wa kiroho zaidi maana yake ni kwa yale yajayo au la baadaye ambalo kwa macho ya kawaida huwezi kuyaona
Ni kama vile Mama Samia hana mda mrefu madarakani lolote litatokea kwake,
 
Dar watachelewa kuanza ila wakisikia kuna maeneo ya Mbeya, Mwanza na Arusha huko kumeanza kuhappen na penyewe rasharasha zitaanza.

Wakikata mitandao ili taarifa zisisambae ndiyo wataharibu zaidi maana sintofahamu na ombwe la taarifa ndiyo litazidisha mzuka wa maandamano.

Nadhani umeme nao utakatwa safari hii nchi nzima ili msiangalie Al Jazeera na BBC na simu zenu ziishe chaji.

Hivi kwa nini hawaoni meza ya mazungumzo ndiyo njia pekee na rahisi kulimaliza hili. Mbona vitu vinavyodaiwa vina faida kwa wote hata watoto wao?

Yaani unakataa njia ya kukaa mezani kuongea huku unakunywa soda na korosho halafu badala yake unachagua njia ya kuwindana na kupasuana vichwa?
 
Hivi kwa nini hawaoni meza ya mazungumzo ndiyo njia pekee na rahisi kulimaliza hili. Mbona vitu vinavyodaiwa vina faida kwa wote hata watoto wao?
Mkuu lakini wao ndio wamesema wanataka "maridhiano", vijana ndio wamekataa hayo mazungumzo, kwa sababu mazungumzo yameonekana ni ulaghai tu
 
Mkuu lakini wao ndio wamesema wanataka "maridhiano", vijana ndio wamekataa hayo mazungumzo, kwa sababu mazungumzo yameonekana ni ulaghai tu
Kwa tulipofikia, maridhiano yatakayowezekana ni yale yanayosimamiwa na Msuluhishi anayeheshimika na pande zote na inawezekana atahitajika kutoka nje.

Unadhani CCM hawajui hayo mambo ya Usuluhishi basi? Viongozi wa Tanzania wangapi wameongoza na wameshiriki katika usuluhishi sehemu mbalimbali?

Hawataki njia hiyo kwanza kwa sababu wanataka kuonyesha hali siyo mbaya kiasi hicho. Pili wakifanya usuluhishi kwa njia wanazotaka sasa, watabuy tu time, watarubuni baadhi ya majumbe wa upande wa pili na wale wabishi watawapoteza na mwisho wa siku hakuna kitakachofanyika.
 
Mkuu lakini wao ndio wamesema wanataka "maridhiano", vijana ndio wamekataa hayo mazungumzo, kwa sababu mazungumzo yameonekana ni ulaghai tu
Sasa utataka maridhiano kwa mtu ambaye amepata madaraka kwa ulaghai
 
Mimi hupenda kuongea kiroho zaidi,nayaona maandamano tarehe 9,nakushauri ndugu yangu nunua mahitaji yako muhimu weka ndani,kuanzia vyakula maji dawa,hakikisha una Cash mkononi ya kukutosha ingalau kwa wiki 2
Nami nimeshuhudiwa na Roho wa Bwana hapa kuwa yatakuwepo... tuchukue tahadhari, tuombe, tusipuuzie chochote..
 
Back
Top Bottom