Nawezaje kumuomba baba wa mtoto anisaidie?

Nawezaje kumuomba baba wa mtoto anisaidie?

Anajua nina mimba yake na hajaonyesha kukataa tatizo ni hanisaidii kitu. Na mimi toka nilivyojua ni mume wa mtu sikutaka habari nae zingine zaidi ya kuongea nae kuhusu mtoto na huwa anasisitiza atanitafuta tuongelee malezi ya mtoto. Toka ameniambia tutaonana tuongee hajawahi nitafuta mpaka leo ila anajua kabisa ujauzito ni wake.
Sasaaa wewee utatembeajee na mume wa mtuu!!!! Ndoo wanaumee wameixhaa au!!!???
 
Mtokee kwake,mbele ya mke wake, kwa nn akuharibie maisha alafu yy ale starehe na mke wake?, mfate akuchakue hela acha kuzubaa
Akikana mtoto sio wake anafanyaje?Acha kiherehere alivyokuwa ana manua unajua waliongea nini?alimuharibia maisha amekuambia alikuwa bikra?
 
Hahahhahaha hamnaa...naona tu unavonifatilia team Zarina Hassan...i js feel sorry for ur friend
Mimi sina team ila nawashangaa watanzania tunavyojitahidi kuhesabu dhambi za wenzetu na kuzikoleza wino
 
Niko kwenye stage ya mwisho wa ujauzito ila mambo naona yamekua mengi na mimi ndo kwanza naanza maisha ila baba wa mtoto yuko vizuri na anajua situation yangu vizuri kabisa. Hapa nilipofikia nahitaji msaada hasa wa kifedha lakini mwenzangu haonyeshi kunisupport japo anajua kabisa nina kiumbe chake na uwezo wa kunisaidia anao. Nawezaje kumwambia anisaidie hapa nilipofikia sababh toka mwanzo mpaka hapa hajawahi nitumia hata elfu moja inisaidie kwenye ujauzito.
Naombeni mawazo yenu maana sijui pa kuanzia.
Daaah kumbe ushapigwa kipapai
 
Unaonekana hujazoea kuomba omba, pia baba mtoto hakudhamiria mimba na hakuifurahia/ hakuwa tayari kuwa na majukumu ya mtoto. Inawezekana pia umeamua kuibeba mimba kama sababu ya kumuweka karibu na yeye au pesa zake.

Kumwambia mzazi mwenzio kuhusu kumuomba pesa ni jambo la kawaida sana sababu ni jukumu lake mwanaume kumtunza mtoto wake. Au huyo mwanaume ni mkali unamuogopa na hasira zake au ameikataa mimba na wewe umemjibu utamlea mwenyewe mwanao.

Ukiona unashindwa kumwambia basi ujue kuna historia nyuma yenu au kuna kitu nyuma ya pazia unatuficha.
Hii story haijakamilika kabisa. Kuna deleted scenes ambazo hatujaambiwa.
 
Kweli sipendi kuomba omba sababu mtu akininyima huwa namchukia kabisa afu sipendi kuwa disappointed. Wote hatukuidhamiria mimba na alitaka niitoe nikamwambia sitaitoa akasema sawa nitakusupport lakini baadae akaja akatuma hela niende nikatoe nikamwambia sitatoa. Akakaa kimya muda mrefu sana labda alihisi nimetoa baada ya miezi kadhaa nikamtafuta mimi nikamwambia sijatoa mimba ili ajue ana mtoto. Akarespond vizuri tu baada ya hapo akakaa kimya tena. Nikaja kumtafuta tena nikamuuliza anataka mtoto amtambue kama baba yake au nijue jina la kumuandika mtoto kwenye cheti akasema yeye ndo baba wa mtoto na atanitafuta tuongelee mustakabali wa ujauzito hapo ilikua miezi kama miwili toka nimtumie ujumbe wa kutotoa.
Akakaa kimya tena. Week mbilj zilizopita nikamchek tena kumwambia nakaribia kujifungua akitaka kumtafuta mwanae yuko huru ila kwa kuwa ameshajijua ndo baba basi mtoto atachukua majina yake kama baba. Akaonyesha kuwa na.furaha kabisa ila sasa hawezi nitafuta mpaka nimtafute na hajawahi hata kunisupport financially. Hiyo ndo story behind
Habari za leo Dada yangu!
Kama amekubali na anafurahi unapompa maendeleo ya ujauzito mueeleze kwamba nimejitahidi kulea ujauzito lakin hali ya kifedha imekuwa mbaya kwangu naomba unisaidie fedha za kujikimu. Sikilizia majibu yake,kama nimuelewa na ana utu atakutumia fedha. Ukiona amekaa kimya ujue hana huruma wala hana mpango na huo ujauzito.Anza kutafuta mbadala wa aidha kwa kumlazimisha atimize wajibu wake au wewe binafsi kutafuta chanzo mbadala kisichokuwa huyo mlengwa cha kujitunza wewe binafsi na ujauzito.Mueleze na kwa jibu lolote usijisikie vibaya.Maisha yataendelea tu.
 
Kwnza moja kwa moja uyo baba mtto hajamfurahia uyo kiumbe uliyembebeaa....pili na ww ni mzembe na ndo unamuendekeza yn inakuaje huombi pesa na akat una shida....uku wenzko (wtto wa kike) wanaomba pesa mpk za pedi ckuiz
 
Niko kwenye stage ya mwisho wa ujauzito ila mambo naona yamekua mengi na mimi ndo kwanza naanza maisha ila baba wa mtoto yuko vizuri na anajua situation yangu vizuri kabisa. Hapa nilipofikia nahitaji msaada hasa wa kifedha lakini mwenzangu haonyeshi kunisupport japo anajua kabisa nina kiumbe chake na uwezo wa kunisaidia anao. Nawezaje kumwambia anisaidie hapa nilipofikia sababh toka mwanzo mpaka hapa hajawahi nitumia hata elfu moja inisaidie kwenye ujauzito.
Naombeni mawazo yenu maana sijui pa kuanzia.
vipi ulishamueleza na nini muitikio wake baada ya kumueleza?
 
isije kukuta yeye part yake ilikuwa kudonate sperm tu na keshamaliza jukumu lake hapo unamsingizia mengine
nilijua ukubwa wa mwili is directly proportional to brain capacity kumbe hamna kitu....
 
Asante kwa kunisahihisha. Ni mume wa mtu nilijua baadae kabisa na mimba ilishaingia sikua na cha kufanya tena. Ina maana mtu akiwa mume wa mtu haruhusiwi kulea ujauzito wake? Angejijua mume wa mtu asingenidanganya.
Ohooo....!!
 
ina maana huyu mwanamme hakupendi ndiyo maana hataki kukuhudumia!!

ukute yy alikua anapita njia tu!
pole sana!
Hata angekuwa anamhudumia bado ukweli ungebaki pale pale tu hampendi. Sisi wanaume tunaweza tukasex na wewe mara milioni na bado upendo wetu ukawa kwa mwengine kabisa. Ndoa ni kitu kikubwa sana na apendwae huolewa
 
Duuuh Pole saaaana, pole saaana zaidi ya thaaana. Madam hapo tunasema hasara taslimu yaani hesabu maumivu. ckuvunji madam lakini huo ndo ukweli. tatizo ni huyo mwanaume wako ni sifuri, yaani hamna kitu. Mwanaume timamu, mwenye nafsi roho na mwili kama wewe ulivyoumbwa hawezi kuwekeza mimba sehemu na kukaa kimya mpaka hatua ya mwisho. Madam mmmmmhhhhh kwa mwelekeo huo namuhesabu kuwa mwanaume mwenye fikra chakavu.
 
Hata kama ni mume wa mtu bado alipaswa kukuhudumia kwa kila hitaji lako. binafsi ananiwazisha saana kwa sababu mimba c kitu cha kupuuza, mimba inahitaji matunzo, upendo na ukaribu.
 
Kweli sipendi kuomba omba sababu mtu akininyima huwa namchukia kabisa afu sipendi kuwa disappointed. Wote hatukuidhamiria mimba na alitaka niitoe nikamwambia sitaitoa akasema sawa nitakusupport lakini baadae akaja akatuma hela niende nikatoe nikamwambia sitatoa. Akakaa kimya muda mrefu sana labda alihisi nimetoa baada ya miezi kadhaa nikamtafuta mimi nikamwambia sijatoa mimba ili ajue ana mtoto. Akarespond vizuri tu baada ya hapo akakaa kimya tena. Nikaja kumtafuta tena nikamuuliza anataka mtoto amtambue kama baba yake au nijue jina la kumuandika mtoto kwenye cheti akasema yeye ndo baba wa mtoto na atanitafuta tuongelee mustakabali wa ujauzito hapo ilikua miezi kama miwili toka nimtumie ujumbe wa kutotoa.
Akakaa kimya tena. Week mbilj zilizopita nikamchek tena kumwambia nakaribia kujifungua akitaka kumtafuta mwanae yuko huru ila kwa kuwa ameshajijua ndo baba basi mtoto atachukua majina yake kama baba. Akaonyesha kuwa na.furaha kabisa ila sasa hawezi nitafuta mpaka nimtafute na hajawahi hata kunisupport financially. Hiyo ndo story behind
Pole baby, Mungu akutie nguvu....kuzaa na mwanaume wa mtu tena ambae hayuko tayar kuzaa na wewe ni mtihani mkubwa,
 
Lolote laweza kutokea hapo. Atakuwa hakuhitaji na upendo na wewe hana jiongeze jiandae kisaikolojia na kiuchumi.
Sio kila jambo litakuwa kama unavyotegemea
 
Back
Top Bottom