Arafat Bahdellah
Member
- Jan 15, 2013
- 77
- 28
sijambo bidada, wewe?
Unajua tupo tofauti. Imagine upo na shosti hapa, ghafla mtu wake wa karibu sana anaumwa na anahitaji matibabu ambayo ni ghali, na unajua kwa haki ya Mungu kabisa hana hizo hela, na wewe unazo. kuendelea kuzitafuta kwa wengine wakati wewe upo naye hapo hata kama hajui kama unazo halafu unamnyima....... hili sitajisamehe, hata mgonjwa akija kupona..... na hata kama shosti hatajua kama ile siku nilikuwa na hizo hela ila sikumsaidia. Kulipana sasa ni majaaliwa......... la maana kwangu nimesaidia kuokoa hatari, Mungu ndo atajua atanilipaje.
Kama ni kukopeshana kwa kununua viwalo au shida ambayo siyo life serving, hapo sasa nitaamua nimpe au nisimpe. na hata kama anajua nina hela namwambia tu bila wasiwasi
Kabla hujaandika hapa ungeniuliza wewe una tabia gani kwnye utoaji ningekujibu kama ulivyoandika!!!
Yaani naweza kumjua mtu 'mtoaji' kiasi fulani kupitia maandishi yake!
By the way......nilkuwa Kigoma nikakutafuta kuanzia Ujiji mpaka Uvinza sijakuona, nilkuwa nauliza 'mmeshamwona yule dada wa kinyamwezi aliyejaaliwa?'...holaa
Binamu umetisha, mtu ukimkopesha laki mbili hata asipokulipa roho haikuumi dah uko juu
Bahati nzuri hao wa laki mbili hawaji kila siku. Tena saana ni ndugu. Akiomba nne, ninamwambia labda 150,000 inategemea na shida yake then naweza mpa 2 then nafuta. Na bahati nzuri, watu wa hivyo akukuliza hawezi rudi tena; hivyo unakuwa umeondoa one mkopaji in your life.
Bora wewe charminglady weakness yako ina unafuu, muulize Dinazarde sasa weakness yake, yani sasa ivi hana shoga wote wamemkimbia kwa umbea, kashachambwa sana mtoto wa watu na vigodoro juu lakini wapi, binamu sio wa kumwamini yani ya siri anatoa na ya bayana anaficha
Pole sana, kila mtu ana mapungufu yake
halafu kuna watu ukiwasaidia wanaona kama we ndio una hela nyingi au tajiri sana. hawajui wenzao wanajiminya vile wanajali matatzo ya wenzao.Hii ndio disadvantage yake....
Saa nyingine unaacha kumsaidia mtu kumbe ana tatizo la kweli hii yote inatokana na baadhi ya watu kuwatumia wenzao moaka hujui nani umuamini nani usimwamini
halafu kuna watu ukiwasaidia wanaona kama we ndio una hela nyingi au tajiri sana. hawajui wenzao wanajiminya vile wanajali matatzo ya wenzao.
Tunafanana....tungoje ushauri.
Me nimejitahidi kujifunza roho mbaya but nimeshindwa.
hahahah!!! utanchelewesha kugraduate ujue
Mkuu ungetoa solution hapa hapa ilo wengine wafaidike, si.umeona kumbe kuna wengi tu wenye tatizo kama langu....
Asante
Husninyo nisaidie basi mimi mtoto yatimaa ati...
We umeshasaidia yatima wangapi? Halafu usikose kwenda na wanaJF wenzako kuangalia wagonjwa wa saratani pale spitali ya Ocean Road....
Sawa....? Usipoenda nakuchafulia nyota yako....
hhahahahahahha!!!!! hivi ujue umepinda? yaani hilo jina avatar na comment vimenichekesha sana. natamani ningeenda ila sitakuwepo pande zile
Ndivyo binadamu tunavyopaswa kuwa. Na ndivyo maandiko ya dini yanavyotaka, giving what you cherish the most without expecting anything in return.
Sikushauri ubadilike, na l wish ungeniambukiza hiyo roho ningefurahi sana. Maana I am struggling to punguza uselfish.