Nawezaje kubadilika?

Nawezaje kubadilika?

ha haaaaa, kama unamkopesha ambaye ana shidwa haswaaaaaa, ni baraka

Wakati unamdai haukasiriki hata kidogo? Ndio maana mimi sikopeshi zaidi ya 200,000 maana hata asiponilipa siumii. Zaidi ya hapo nitakasirika baadaye kusononeka. Na hasira ni mzizi wa dhambi.

Baraka kwangu ni kumpa muhitaji ambaye hana uwezo wa kunilipa zaidi ya kusema "ubarikiwe".

BTW hujambo bibiye?
 
mi ntakuja unibadili tabia, kuna kiroho flani cha huruma nahisi bado hakijaondoka fresh.

Nakumbuka ulivyochukua sabbatical leave away from JF baada ya kulizwa. Hiyo haijakufundisha tu? Sasa watu kama ninyi, unapomkopa mtu; chukulia unampa tu. Akikurudishia hewala, asipokurudishia pia hewala. Sonono sio nzuri inaondoa Baraka ambazo ungezipata kwa kudhulumiwa.
 
Wakati unamdai haukasiriki hata kidogo? Ndio maana mimi sikopeshi zaidi ya 200,000 maana hata asiponilipa siumii. Zaidi ya hapo nitakasirika baadaye kusononeka. Na hasira ni mzizi wa dhambi.

Baraka kwangu ni kumpa muhitaji ambaye hana uwezo wa kunilipa zaidi ya kusema "ubarikiwe".

BTW hujambo bibiye?

Binamu umetisha, mtu ukimkopesha laki mbili hata asipokulipa roho haikuumi dah uko juu
 
Habari za jumapili wadau wa jukwaa hili....

Hii tabia imenishinda kuacha, iko hivi....
Iwapo akatokea mtu wangu wa karibu iwe mpenzi/mshikaji/shost ana shida fulani huwa nakuwa mwepesi sana kumsaidia hata kama itanicost kifedha, muda hata nguvu huwa najitahidi sana kumsaidia....

Hata kama niko kazini, niko radhi nitoroke nikamsaidie mtu, kwa mpenzi ndio kabisa nashindwa kujizuia. Nitadanganya hata msiba ilimradi tu nikamsaidie atakacho.

Either kazi flan au kumpeleka mahali fulani au kumfatia kitu fulani. Lakini in returns sasa wananifanyia ndivyo sivyo, huwa napatwa hasira weee nachukia ila baada ya muda nasahau na kuendelea vivyo vivyo.

Unaweza kuwa na shida ukamfata mpenzi, mshikaji / shost kumueleza lakini akadai yuko busy au hana pesa labda, ilhali unafahamu kabisa ana uwezo wa kukusaidia. Mtu huyo huyo hapo baadae anakufata umsaidie wakati yeye huwa hakusaidii ukiwa na shida.

Nifanyeje niiache hii tabia, make inanicost ila nimekuwa kichwa ngumu kuishinda!

Wasalaam

CL

Hii tabia ni pure kama ya mama yangu mzazi, so watu kama nyie ni wachache sana pia ni gifted people from heaven .
 
Wakati unamdai haukasiriki hata kidogo? Ndio maana mimi sikopeshi zaidi ya 200,000 maana hata asiponilipa siumii. Zaidi ya hapo nitakasirika baadaye kusononeka. Na hasira ni mzizi wa dhambi.

Baraka kwangu ni kumpa muhitaji ambaye hana uwezo wa kunilipa zaidi ya kusema "ubarikiwe".

BTW hujambo bibiye?
sijambo bidada, wewe?
Unajua tupo tofauti. Imagine upo na shosti hapa, ghafla mtu wake wa karibu sana anaumwa na anahitaji matibabu ambayo ni ghali, na unajua kwa haki ya Mungu kabisa hana hizo hela, na wewe unazo. kuendelea kuzitafuta kwa wengine wakati wewe upo naye hapo hata kama hajui kama unazo halafu unamnyima....... hili sitajisamehe, hata mgonjwa akija kupona..... na hata kama shosti hatajua kama ile siku nilikuwa na hizo hela ila sikumsaidia. Kulipana sasa ni majaaliwa......... la maana kwangu nimesaidia kuokoa hatari, Mungu ndo atajua atanilipaje.
Kama ni kukopeshana kwa kununua viwalo au shida ambayo siyo life serving, hapo sasa nitaamua nimpe au nisimpe. na hata kama anajua nina hela namwambia tu bila wasiwasi
 
Nakumbuka ulivyochukua sabbatical leave away from JF baada ya kulizwa. Hiyo haijakufundisha tu? Sasa watu kama ninyi, unapomkopa mtu; chukulia unampa tu. Akikurudishia hewala, asipokurudishia pia hewala. Sonono sio nzuri inaondoa Baraka ambazo ungezipata kwa kudhulumiwa.

hicho ndo ninachokifanya sahv, yaani ni bora kujihesabia umetoa kuliko kukopesha. sahv mtu akinifata na shida ya mkopo jibu ni moja tu kuwa sina.
 
sist Kaunga lile somo nilijifunza kweli. mwaka jana kuna mwingine aliniambia nimkopeshe laki afanye nauli akirudi huku atanipa. nikamwambia sina, baada ya kama wiki tatu akaniambia yupo home ila anaumwa sana. nikamuuliza umeanza kuumwa lini akanambia ana zaidi ya mwezi maana alianza kuumwa huko alipokuwa.
nikajiuliza hivi ningemdai vipi ile laki na mtu naumwa hivi, alinitumia na picha zake whatsapp hadi chozi lilinitoka. atanisamehe kama atajiskia vibaya akinisoma hapa. ni ushuhuda tu wa somo nililojifunza.
 
Last edited by a moderator:
Wakati unamdai haukasiriki hata kidogo? Ndio maana mimi sikopeshi zaidi ya 200,000 maana hata asiponilipa siumii. Zaidi ya hapo nitakasirika baadaye kusononeka. Na hasira ni mzizi wa dhambi.

Baraka kwangu ni kumpa muhitaji ambaye hana uwezo wa kunilipa zaidi ya kusema "ubarikiwe".

BTW hujambo bibiye?

200,000 yote hiyo??? Mie mwisho 15,000. Hapa kuna mtu namdai 20,000 mwezi wa tatu sasa namlia timing tu......

La unatakiwa ukikopesha uhesabu umetoa sadaka tu
 
Hii ndio disadvantage yake....

Saa nyingine unaacha kumsaidia mtu kumbe ana tatizo la kweli hii yote inatokana na baadhi ya watu kuwatumia wenzao moaka hujui nani umuamini nani usimwamini

sist Kaunga lile somo nilijifunza kweli. mwaka jana kuna mwingine aliniambia nimkopeshe laki afanye nauli akirudi huku atanipa. nikamwambia sina, baada ya kama wiki tatu akaniambia yupo home ila anaumwa sana. nikamuuliza umeanza kuumwa lini akanambia ana zaidi ya mwezi maana alianza kuumwa huko alipokuwa.
nikajiuliza hivi ningemdai vipi ile laki na mtu naumwa hivi, alinitumia na picha zake whatsapp hadi chozi lilinitoka. atanisamehe kama atajiskia vibaya akinisoma hapa. ni ushuhuda tu wa somo nililojifunza.
 
Last edited by a moderator:
Thats about your personality,

Utakuwa na sifa kadhaa miongoni mwazo; unachukia ugomvi, anamjali yeyote hata kama haumjui, mtaalamu wa kutunza siri (serious to those you dont know)

Aina ya personality yako ni Phlegmatic

With your time read; armchair_academic.homestead.com/PersonalityComp...

Hivyo ndivyo ulivyo, usijaribu kubadirika

Ushauri wangu; dont expect anything in return from them, just do it for them.
 
Aiseeeeeee ila hao wanavyoendelea watakuvunja moyo nakuambia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom