Habari za jumapili wadau wa jukwaa hili....
Hii tabia imenishinda kuacha, iko hivi....
Iwapo akatokea mtu wangu wa karibu iwe mpenzi/mshikaji/shost ana shida fulani huwa nakuwa mwepesi sana kumsaidia hata kama itanicost kifedha, muda hata nguvu huwa najitahidi sana kumsaidia....
Hata kama niko kazini, niko radhi nitoroke nikamsaidie mtu, kwa mpenzi ndio kabisa yeeeuuuwwiii nashindwa kujizuia.
Nitadanganya hata msiba ilimradi tu nikamsaidie atakacho... Either kazi flan au kumpeleka mahali fulani au kumfatia kitu fulani.
Lakini in returns sasa wananifanyia ndivyo sivyo, huwa napatwa hasira weee nachukia ila baada ya muda nasahau na kuendelea vivyo vivyo....
Unaweza kuwa na shida ukamfata mpenzi, mshikaji / shost kumueleza lakini akadai yuko busy au hana pesa labda, ilhali unafahamu kabisa ana uwezo wa kukusaidia. Mtu huyo huyo hapo baadae anakufata umsaidie wakati yeye huwa hakusaidii ukiwa na shida.
Nifanyeje niiache hii tabia, make inanicost ila nimekuwa kichwa ngumu kuishinda!
Wasalaam
CL