Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
NAWATAKIA WAISLAM WOTE RAMADHAN NJEMA, HAYA NI YANGU MACHACHE.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu Jeusi.
Ninapenda kuwatakia Waislam wote Ramadhan njema. Mwezi huu ni muhimu katika dini ya kiislam kwani inaaminiwa kuwa ndio mwezi ambao Quran tukufu ilishushwa Kwa mara ya Kwanza, yaani ufunuo wa kwanza"wahayi wa Kwanza" kushushwa.
Quran ilishushwa katika mwezi wa tisa katika Kalenda za kiarabu za Wakati huo, ambao uliitwa Ramadhan, uliitwa Ramadan Kutokana na Tabia na Hali y hewa Kwa mwezi huo kuwa na jua Kali na ukame, hivyo neno Ramadan ni neno la kiarabu lenye maana ya "dryness" au ukame" au kiangazi Kwa Lugha ya kijiografia.
hivyo Baada ya ujio wa uislam ulirithi Kalenda hiyo ambao Kwa sasa Kalenda ya kiislam hutumia Lunar Calendar yaani Kalenda inayofuata Mzunguko wa mwezi.
Hii ni kusema kwenye Kalenda ya kiislam Mwaka Una siku kama 354 hivi Kutokana na Mzunguko wa mwezi kwenye Dunia. Zingatia Mzunguko wa mwezi ni siku 28 mpaka 30 kutegemeana na mwezi husika na Aina ya Kalenda. Hautakula wala kunywa Kwa nyakati zote za Mchana na utafungua Swaumu nyakati za jioni kabisa, Kwa kula Iftars.
Tunaweza kujiuliza ni Kwa nini Quran ishushwe mwezi wa tisa, yaani Mwezi wa Ramadhan na sio mwezi mwingine? Hilo tutajadili siku nyingine, lakini lazima kuwe na sababu. Kwa maana katika dini au sayansi kila kitu kina sababu na maana yake.
Kwa nini Waislam waliamrishwa Wafunge katika mwezi huu wa Ramadhan na sio mwezi mwingine?
i) Sababu kubwa ni kuadhimisha, kuheshimu, kukumbuka mwezi ambao Quran tukufu ambayo ni kitabu wanachoamini kimetoka Kwa Mungu wao kama kitabu cha kuwaongoza.
Hivyo kuiheshimu Ramadan ni kukiheshimu kitabu cha Quran na kumheshimu aliyekishusha.
ii) Kupitia Swaumu(njaa itakayowapata Wakati wamefunga) Wataweza kuelewa Kwa vitendo namna Watu wenye uhitaji kama Maskini wasio na Chakula jinsi wanavyojisikia. Na hii itawafanya wao wawe na Shukrani Kwa vile Mungu wao alivyowaneemesha, pia itawapa Ari na hamasa ya kuwasaidia wenye njaa na uhitaji.
Na hii italeta sababu ya tatu hapo Chini.
iii) Kutoa Zakat, yaani sehemu ya Mali Yao kama Sadaka Kwa wenye uhitaji.
Iv) kutenda Mema kadiri ya majaliwa MTU aliyojaliwa.
Uislam kama zilivyodini nyingine za Haki zinatambua kuwa Watu wote sio Sawa, Watu hawafanani, kuna wenye afya na wasio na afya. Ndio maana amri hii iliweka uwanja WA kutokea Kwa wale wagonjwa na wenye udhaifu unaofahamika na kukubalika kisheria, Watu wa hivyo hawatakiwi kufunga Ramadan.
Kufunga Ramadan ni lazima, pia ni sehemu ya nguzo ya lazima katika Uislam.
Mtu mwenye afya njema halafu hajafunga lakini anajinasibisha na uislam anamaanisha nini;
1. Anamdharau Mungu wake(Mungu wa Waislam)
2. Anadharau kitabu cha Quran na Dini yote ya Waislam.
Mtu huyo ni Mbaya zaidi kuliko Kafiri asiyemuamini Mungu.
Kwa sababu yeye anamuamini na kumjua Mungu(Mungu wa Waislam) lakini hamfuatishi vile asemavyo.
Sisi wengine tusiowaislam Kwa maana ya kufuata dini hiyo, tunauona utaratibu huu wa Mungu aitwaye Allah na Mtumishi wake Muhammad ni mzuri, na Kwa sababu tunapenda vitu vizuri tunawapongeza walitunga Jambo hilo na wanaolifuata. Kwa sababu lengo lake ni kujenga jamii na kuifanya jamii iwe na Matendo Mema.
Wazazi na watu wote wenye nafasi ya uongozi. Ni muhimu kuwalea Watoto wetu katika misingi ya maadili Mema yenye kuifanya jamii yetu kuwa jamii inayoupinga na kuukataa uovu.
Sisi kina Taikon tunazichukulia dini kama vyuo vya kufundisha maadili Mema.
Hivyo Kusoma chuo cha uislam au Ukristo au ubudha au Voodoo au dini yoyote uwe Kwa lengo la kuifanya jamii iwe na Maadili.
Mambo ya ubaguzi kisa mmoja kasomea Ukristo au uislam ni Sawa na MTU anayembagua MTU aliyesomea Udsm na aliyesomea Oxford.
Kwenye Dini tumefundishwa kubagua Watu waovu, na wasio na Maadili.
Hatujafundishwa kubagua Watu Wema kisa wamesomea Chuo cha Uislam au Ukristo au Usabato.
Kufikia hapo sina la ziada.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam