Nawakwepa marafiki wasiojielewa

Nawakwepa marafiki wasiojielewa

msemakweli2

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
1,627
Reaction score
1,886
Salaaaaam bandugu, jamani katika maisha kila mtu anakuwa na mikakati ya kimaisha, katika mikakati yangu mimi nawakwepa marafiki wasiojielewa,

unakuta unakaa na lijamaa mahali mnapiga stori mbili tatu linaanza kuhadithia habari za mademu liliolala nao, afu ni jitu zima, mara lingine linaanza kulalamika mara hichi mara kile,

katika maongezi yote husikii akianza kuongelea jinsi ya kutatua matatizo, akitoka hapo anaanza kuparamia bia mara mchemsho, mara chips,unajiuliza hivi huyu jamaa nyumbani anaishi vipi na watoto na mkewe, na je familia yake ipo salama kweli.

TUBADILIKE WANAUME WENZANGU
 
Salaaaaam bandugu, jamani katika maisha kila mtu anakuwa na mikakati ya kimaisha, katika mikakati yangu mimi nawakwepa marafiki washenzi na wasiojielewa, unakuta unakaa na lijamaa mahali mnapiga stori mbili tatu linaanza kuhadithia habari za mademu liliolala nao, afu ni jitu zima, mara lingine linaanza kulalamika mara hichi mara kile, katika maongezi yote husikii akianza kuongelea jinsi ya kutatua matatizo, akitoka hapo anaanza kuparamia bia mara mchemsho, mara chips,unajiuliza hivi huyu jamaa nyumbani anaishi vipi na watoto na mkewe, na je familia yake ipo salama kweli. TUBADILIKE WANAUME WENZANGU
kama ushamba Fulani hiv
 
Wewe uko kama mimi, mtu kama huyo huwa siwezi kumuentartain..na wale wanaokuwa wambea wambea yaan kutwa kuongelea na kufatilia maisha ya watu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo wa hivyo yanatudhalilisha watumiaji kilaji. Unakuta familia yake inavyoishi ndani hovyo, kula na kuvaa shida. Kazi kuweka heshima bar.
 
Wapo pia wanaokukwepa kwa kua haujielewi ndivyo maisha yalivyo kama ambavyo hauwataki baadhi ya watu na wewe pia hautakiwi kwa kua unakwamisha maendeleo yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom