Nawaasa wanaotaka kuandamana

Oct 6, 2020
27
50
Na Thadei Ole Mushi.

Kipindi hiki Cha uchaguzi mkuu niuhimu kuwakumbusha watu Mambo muhimu ambayo yanaweza kuwaletea shida wasipoyajua. Kuna baadhi ya wanasiasa wameaacha kunadi sera wao wanasema tusiposhinda tutaandamana na kuleta vurugu. Ni vizuri vijana kufahamu kuwa kuandamana bila ruhusa ni Kujaribu kumpindua Rais aliyepo madarakani na kwa mujibu wa Sheria zetu huo ni uhaini na adhabu yake ni kifo. Vijana wafahamu pia kwamba kumshawishi au Kuchochea vurugu ni uhaini.

Sheria za nchi zinasemaje?

Sheria ya jeshi la Polisi ya mwaka 1961 na marekebisho yake ya mwaka 1995 ambayo kwayo ndio tunayoifuata hadi sasa inatoa njia na namna ya kuendesha maandamano nchini. Inasema nanukuu:-..

(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-

(a) Sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;

(b) Dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na

(c) Maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.

(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa.

(3) Afisa polisi ambaye taarifa imewasilishwa kwake kulingana na kifungu kidogo cha (1), hatatoa amri ya kusitisha chini ya kifungu kidogo cha(2) kulingana na taarifa isipokuwa ameridhika kwamba kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kuna uwezekano wa kusababisha kuvunjika kwa amani au kuathiri usalama wa taifa au kudumisha amri kwa umma au kutumika kwa dhumuni lolote lisilokuwa halali."

Hiyo ndio sheria inayoliongoza jeshi letu la polisi.Kwa maana rahisi maandamano ni mpaka jeshi la polisi likubali na litoe kibali baada ya waandamanaji kuomba kibali hicho.

Kwa vyovyote vile maandamano hayo yanapaswa jeshi la Polisi lijiridhishe pasipo na Shaka kuwa hayatasababisha madhara yoyote na hayata ingilia haki za watu wengine ambao hawataki kuandamana. Huu ni mtego niliokuwa nawaambia...

NINI KINAWEZA KUTOKEA?

Kinachoweza kutokea baada ya katazo la jeshi la Polisi ni watu wenye nia ya kuandamana kutaka kuandamana kwa nguvu. Ukifanya hivyo moja kwa moja utakuwa unatenda kosa la UHAIN ambalo ndio kosa kubwa kuliko yote nchini kwa mujibu wa ibara ya 28 ya katiba yetu.

Sheria inatuambia kwamba kama ukifanya yafuatayo utakuwa umefanya uhaini katika nchi yako.

( a ) Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya muungano au popote akajaribu kumuua rais atakuwa ametenda uhaini.

( b ) Pia mtu yeyote aliye ndani ya Jamhuri ya muungano au popote na akaanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya muungano atakuwa naye ametenda kosa la uhaini.

( c ) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa rais atakuwa ametenda uhaini.

( d ) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondoa rais madarakani visivyo halali atakuwa ametenda uhaini.

( e ) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano au popote ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kumwondolea rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali atakuwa ametenda kosa la uhaini.

( f ) Mtu yeyote ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya muungano ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini.

Rudia kusoma kipengele D Hadi ukielewe ukishindwa mwite na Mwenzako mkisome kwa pamoja.

Aidha ifahamike kuwa kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.

Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya jinai dhidi ya nchi yetu.

Wale wanaowachochea kwenye kampeni waambieni Siku hiyo wanayotaka kuandamana waje na familia zao wake Mbele kabisa maana Hao wakishapata Vyeo hulia kivulini, wanasoma shule Bora kabisa, Wana Mali mpaka nje ya nchi, wakiumwa wanatibiwa hospital Bora kabisa. Ukiona familia zao zipo Mbele waungeni mkono.

Ole Mushi.
0712702602
 
Mtawatisha sana watu mwaka huu ila jueni tu Watu tumechoka na tumeshasema liwalo la liwe mwaka huu.

Uzuri Mungu ameshawaweka watetezi wetu mwaka huu, tupigeni risasi, tuueni ila jueni Mamarekani kawashikia kooni mwaka huu, nimesikia anafikiria Military options endapo mtatumia majeshi na polisi.

CCM lazima mjue hamjui mwaka huu, watu hawaogopi vitisho vyenu mwaka huu!!

Kwa iyo na nyie jiandaeni tu mwaka huu!!
 
Sikio la kufa, wanatafuta tu sababu! Ila wajue mchuma janga hula na wakwao, afu muhimu zaidi jamaa ana return ticket.
 
Ujinga wa watanzania sasa basi Nigeria umeona kinacho endelea kwa wewe hapa duniani utaishi milele mbona kuna watu wanakufa kila siku kwa ajali kwa nini nisitete haki na Uhuru wa mtanzania sasa Niko tayari kwa lolote msitutie uoga wewe fungia ukoo wako ndani acha wasaka haki wafanye yao
 
Zanzibar kidooogo wanaweza kuingia barabarani (nature haidanganyi, DNA za baadhi yao zina ukaribu na kule Yemen) bara hata Lissu mwenyewe hawezi kutia mguu barabarani maana bado ana risasi kwenye uti wa mgongo hivyo akisikia mlio tu wa bunduki, ile risasi ina react wenzake wa nje na kuanza kuuma.

Hakuna mtu bara wa kuingia barabarani hata Mange Kimambi amethibitisha hilo....chapati na supu ya utumbo mtaani vitamu wewe! nani aviache kisa Lissu na Amsterdam?
 
Mtawatisha sana watu mwaka huu ila jueni tu Watu tumechoka na tumeshasema liwalo la liwe mwaka huu.

Uzuri Mungu ameshawaweka watetezi wetu mwaka huu, tupigeni risasi, tuueni ila jueni Mamarekani kawashikia kooni mwaka huu, nimesikia anafikiria Military options endapo mtatumia majeshi na polisi.

CCM lazima mjue hamjui mwaka huu, watu hawaogopi vitisho vyenu mwaka huu!!

Kwa iyo na nyie jiandaeni tu mwaka huu!!
Hahahahaha kwamba military options dah
 
Ujinga wa watanzania sasa basi Nigeria umeona kinacho endelea kwa we we hapa duniani utaishi milele mbona kuna watu wanakufa kila siku kwa ajali kwa nini nisitete haki na Uhuru wa mtanzania sasa Niko tayari kwa lolote msitutie uoga we fungia ukoo wako ndani acha wasaka haki wafanye yao
Endelea ku-rap hapo kwenye keyboard, au toka nje uone kama kesho yake hautakuimbia" ...lango, lango, lango...lango ni Yesuuuuu!
 
Bora zako wewe umekuwa mkweli
Zanzibar kidooogo wanawezakuingia barabarani (nature haidanganyi, dna za baadhi yao zina ukaribu na kule Yemen) bara hata Lissu mwenyewe hawezi kutia mguu barabarani maana bado ana risasi kwenye uti wa mgongo hivyo akisikia mlio tu wa bunduki, ile risasi ina react wenzake wa nje na kuanza kuuma.
Hakuna mtu bara wa kuingia barabarani hata Mange Kimambi amethibitisha hilo....chapati na supu ya utumbo mtaani vitamu wewe! nani aviache kisa Lissu na Amsterdam?
 
Mwandishi unapoteza muda kuandika LITANIA ndefu. Kwani ni nani ataishi milele bila kufa? Kuna watu wanaokufa kwenye MAHOSPITALI yetu kwa kukosa hela ya dawa wala HAWAJAANDAMANA.

Kuna watu wanaokufa kwenye ajali za barabarani kutokana na barabara mbovu wala HAWAJAANDAMANA!!
Kuna watu waliuliwa na TPDF kule Rufiji na Kibiti wakiwa majumbani kwao wala HAWAJAANDAMANA.

Last week kule Kijiji cha Kitaya Mtwara kuna watu wameuliwa na ALSHABAB wala HAWAKUANDAMANA.

Wanaoleta mapinduzi ya kisiasa na kiuongozi siyo watu LEGELEGE au WAOGA kama wewe mwandishi, bali ni watu waliojitolea ajili ya kuiokoa JAMII inayonyanyaswa. Mfano wa hao ndiyo akina JK Nyerere, Nelson Mandela, Ernesto Che Guevara, Fidel Castro, Tundu Lissu etc.

Wao hawafikiri kama wewe unayekumbuka mke na watoto, bali wai wanaangalia matokeo ya kuuuondoa utawala dhalimu na kuleta uhuru, haki na usawa.

Kama huwezi KUSHIRIKI, basi USIKATISHE tamaa MASHUJAA wetu.
 
Kuna baadhi ya wanasiasa wameaacha kunadi sera wao wanasema tusiposhinda tutaandamana na kuleta vurugu.
Hapo kwenye maneno meusi Ole Thade hujasema kweli kama ilivyo kawaida yako.

Sijui ni kwanini umeamua kuuvua uadilifu wako na kufanya upotoshaji huu.

Hakuna mgombea yeyote aliyewahi kutamka maneno hayo. Wote tunafuatilia na kushiriki kampeni hizi.

Wanachosema Ni kwamba Tusiposhinda KWA HAKI. Kwahiyo ktk maandishi yako umeacha neno HAKI sijui ni kwa bahati mbaya ama makusudi?
 
Back
Top Bottom