Jason Statham2
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 692
- 1,009
Labda ni mbegu za CHAI alikosea tu kuandika.
Unaonaje kama ungeandika faida za hizo mbegu
Kwenye maisha yetu ya sasa hizi mbegu ni supplements nzuri kwa afya ya familia zetu
Ahsante kwenye post faida zake zimewekwa kwenye link ikiwa ukiziona hizi ndizo faida ya mbegu za Chia.
Moja Ina virutubisho vingi vinavyohitajitaka mwilini na madini , vitamini na Protein pia ina omega 3 na omega 6
Mbili Inaimarisha Mifupa kutokana na kuwepo kwa madini mengi na hasa ya calcium inasaidia kuwa na afya bora ya mifupa na inasahidia kwa watoto na vilevile wakinamama kutosababisha mifupa kuwa mepesi hasa baada ya kukoma siku zao
Tatu Inaimarisha Afya ya ubongo kutokana na kupatikana kwa omega 3 na 6 yaani kama kwenye samaki inasaidia seli za ubongo kuwa vizuri na hiyo kufanya kazi sawa sawa.
Nne inasaidia katika mmeng'enyo wa chakula kwa kuwa zina fiber nyingi kwa wale ambao pia wananenepa kwa kuwa wanashidwa kumeng'enya chakula vizuri mbegu za chia zina fiber nyijngi sana ambazo zinasaidia hilo na vilevile watu wanapendelea kupunguza uzito ukila vijiko viwili vya chia seeds unaweza kutojisikia njaa kabisa siku nzima kwa sababu nazo zinatanuka karibu mara kumi zaidi.
Tano Huimarisha afya ya moyo kwa kuweka kwenye uwiano sawa kiwango cha lehemu mwilini
Sita NI Antoxidants ambayo inasaidia sana katika kurepair sell za mwili na hivyo kukufanya uwe na muonekano mzuri kwa kuwa seli zinaishi muda mrefu na hivyo kupunguza dalili za kuzeeka kwa kuongoa makunyazi ya ngozi.
Saba inasaidia kubalance na kuweka vyema (Kuregulate) sukari mwilini hivyo kuwasaidia watu mwenye kisukari wasipate madhara yanayoletwa na kisukari lakini vile vile inasaidia watu walio kwenye hatari kutopata ugonjwa huo
Na kama unataka kuangalia video nayo click kwenye link hapo chini
Nakushurukuru Tena
Nimepata kitu changu cha Chia iliyosagwa napiga kwenye mtindi wangu baridi kwenye saa tano asubuhi vijiko viwili kwa kweli ilibidi niskip lunch leo jinisi nilivyokuwa nimeshiba hii kitu. Kiboko kwa wale tuliobahatika kula ugali wa uwele naamini hivi vimbegu vidogo vidogo vinakaa sana tumboni. Nimeelewa ni kwanini inasaidia kukuata uzito maana kitu kidogo tuu tumbo linakaa vizuri. Kweli maarifa yataongezeka siku hizi
ZINASAIDIA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME?
Mayai ya Kware mlikua mnasemaga hivi hivi,sasa hivi yako wapi tena? msitumie umaskini wa watanzania kuwaingiza chaka....kesho kwa Mungu kuna motoHeri ya mwaka mpya. Katika kufikia moja ya malengo yako ya kuwa na afya njema katika mwaka 2019 ongeza Chia Seeds kwenye milo yako na vilevile upate faida ya kupunguza uzito uliopitiliza. Karibu