Nauona ushindi wa Taifa Stars hapo kesho lakini Kamati ya Ushindi ina ukakasi. Kesho tunaandika historia mpya!

Mungu wetu ni mwema sana. Ameiongoza na kuilinda timu yetu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) hadi ilipofikia. Ameipa alama ilizonazo sasa na kesho anaipa nafasi na baraka za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Kesho ni siku yetu.

Uwepo wa wachezaji wetu wanaocheza nje na ndani ya Tanzania kupambana na majirani zetu Uganda ni kiashiria tosha cha kufuzu kwetu na kuandika historia mpya ambayo itakumbushia kufuzu kwetu mwaka 1980,mwaka ambao sina hakika kama kuna mchezaji yeyote atakayecheza kesho alizaliwa. Nauona ushindi wetu kesho.

Imeundwa Kamati ya Kuhamasisha ushindi wetu hapo kesho. Kwakuwa mimi si rafiki wa unafiki,nauona ukakasi wa wazi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Paul Makonda,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kamati imejumuisha watu maarufu tu ambao hata danadana mbili hawajawahi kupiga.

Kamati ya Makonda inapoteza lengo. Ushindi wa timu huanzia kwa wachezaji na si watazamaji au mashabiki. Kutingwa na watazamaji na mashabiki badala ya wachezaji ni kupoteza uelekeo. Kesho unachezwa mpira. Mpira si kama siasa inayotegemea porojo,propaganda na utapeli. Soka ni muunganiko wa uwezo wa wachezaji na saikolojia yao.

Naamini Tanzania ina wachezaji wenye vipaji. Kati yao wanaunda timu ya Taifa. Kinachopungua miaka yote ni kukosekana kwa saikolojia ya kujiamini,kupambana kwa ajili ya taifa letu,kujitoa na kuwa makini kwa kila sekunde ya mchezo. Kamati ya Makonda ilipaswa kujielekeza huku.

Kamati ilipaswa kujumuisha baadhi ya mashujaa wetu wa 1980 walio hai ili kuwaaminisha watoto wao wanaocheza kesho kuwa kila jambo linawezekana. Wapi akina 'Computer'? Anaingiaje Haji Manara akaachwa Sunday Manara baba yake na mmoja wa mashujaa wa 1980? Isigeuzwe ni Kamati ya sherehe kabla ya ushindi!
Yaani hiyo kamati ni kichefuchefu aisee. Watu wasio na msaada ndo wameingizwa.
 
If..
>Tanzania 2-1Uganda [55%]
>Tanzania 1-1Uganda [75%]
>Tanzania 2-2Uganda [25%]
>Tanzania 1-0Uganda [80%]
>Tanzania 0-1Uganda [85%]
>Tanzania 0-0Uganda [10%]

Calibration..
Pass accuracy.. [error!]
Short on target accuracy..[error]
Expected Outcome: W/D/L.....
Political Outcome: W
Hint:Wachezaji mjitume Uganda hawataki masihara.
 
If..
>Tanzania 2-1Uganda [55%]
>Tanzania 1-1Uganda [75%]
>Tanzania 2-2Uganda [25%]
>Tanzania 1-0Uganda [80%]
>Tanzania 0-1Uganda [85%]
>Tanzania 0-0Uganda [10%]

Calibration..
Pass accuracy.. [error!]
Short on target accuracy..[error]
Expected Outcome: W/D/L.....
Political Outcome: W
Hint:Wachezaji mjitume Uganda hawataki masihara.
IMG-20190323-WA0022.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stars itashinda na Lesotho atadraw au kufungwa hivyo njia ya stars kwenda Misri kushiriki Afcon 2019 haina kikwazo.
 
Kamati ya Makonda inapoteza lengo. Ushindi wa timu huanzia kwa wachezaji na si watazamaji au mashabiki. Kutingwa na watazamaji na mashabiki badala ya wachezaji ni kupoteza uelekeo. Kesho unachezwa mpira. Mpira si kama siasa inayotegemea porojo,propaganda na utapeli. Soka ni muunganiko wa uwezo wa wachezaji na saikolojia yao.
Naogopa kuongeza neno, wacha nipigie mistari na kubadili rangi!!
 
Binafsi huwa sina imani sana na Taifa stars, na huyu Amunike ndo simuelewi kabisa. Bado nafkiria mara mbili mbili kuhusu kwenda taifa leo

the Legend☆
Mm Amunike alishaganikosesha amani huwa sikosi International game iwe Taifa stars au Simba ila ile game ya Lesotho anawapanga akina mwantika na ally sonso mtoni sijui nn akina Yondani bench basi nikajua Amunike kabeti Leo nitaangalia Kwa TV tu matokeo yoyote yale sawa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwa jezi ni zile za msalaba sitaishangilia Taifa stars. Uzalendo wa misalaba siuwezi.
Na rangi nyeupe huwa inaingiaje kwenye jezi za Stars wakati si sehemu ya rangi bendera ya taifa?Lazima kuna umikia mikia FC kwa hisani ya Tifua tifua??
 
Back
Top Bottom