Nauona ushindi wa Taifa Stars hapo kesho lakini Kamati ya Ushindi ina ukakasi. Kesho tunaandika historia mpya!

Mm nilishasema hii nchi ina wajinga wengi mno ndo maana ipo hivi ilivyo. Mpira hauhitaji maombi..hata huyo Mungu(kama yupo) atakuwa wa ajabu,yaani aache kushughulika na wagonjwa na wenye uhitaji ashughulikie burudani!??

Halafu watu ni wajinga kwelikweli,hata akili za kawaida tu mnakosa,huyo Mungu si atakuwa kibarua wenu!?? Yaani mumuombe awasaidie muifunge Uganda,halafu wakati huohuo muombe Lesotho afungwe au atoe sare. Huyo Mungu si bora ahamie Tanzania tu...!! Mpira unachezwa hadharani bhaana,hakuna cha maombi hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nshamuambia huyu mwanasheria kanjanja aache kumuhusisha Mungu na upuuzi

Watu wanaozungumza mambo wasiyoyajua kimbilio lao la kwanza huwa ni kujificha kwa Mungu.
 
Mungu wetu ni mwema sana. Ameiongoza na kuilinda timu yetu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) hadi ilipofikia. Ameipa alama ilizonazo sasa na kesho anaipa nafasi na baraka za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Kesho ni siku yetu.

Uwepo wa wachezaji wetu wanaocheza nje na ndani ya Tanzania kupambana na majirani zetu Uganda ni kiashiria tosha cha kufuzu kwetu na kuandika historia mpya ambayo itakumbushia kufuzu kwetu mwaka 1980,mwaka ambao sina hakika kama kuna mchezaji yeyote atakayecheza kesho alizaliwa. Nauona ushindi wetu kesho.

Imeundwa Kamati ya Kuhamasisha ushindi wetu hapo kesho. Kwakuwa mimi si rafiki wa unafiki,nauona ukakasi wa wazi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Paul Makonda,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kamati imejumuisha watu maarufu tu ambao hata danadana mbili hawajawahi kupiga.

Kamati ya Makonda inapoteza lengo. Ushindi wa timu huanzia kwa wachezaji na si watazamaji au mashabiki. Kutingwa na watazamaji na mashabiki badala ya wachezaji ni kupoteza uelekeo. Kesho unachezwa mpira. Mpira si kama siasa inayotegemea porojo,propaganda na utapeli. Soka ni muunganiko wa uwezo wa wachezaji na saikolojia yao.

Naamini Tanzania ina wachezaji wenye vipaji. Kati yao wanaunda timu ya Taifa. Kinachopungua miaka yote ni kukosekana kwa saikolojia ya kujiamini,kupambana kwa ajili ya taifa letu,kujitoa na kuwa makini kwa kila sekunde ya mchezo. Kamati ya Makonda ilipaswa kujielekeza huku.

Kamati ilipaswa kujumuisha baadhi ya mashujaa wetu wa 1980 walio hai ili kuwaaminisha watoto wao wanaocheza kesho kuwa kila jambo linawezekana. Wapi akina 'Computer'? Anaingiaje Haji Manara akaachwa Sunday Manara baba yake na mmoja wa mashujaa wa 1980? Isigeuzwe ni Kamati ya sherehe kabla ya ushindi!
Motisha ya bia only in tanzania
 
Hakuna nilipomhusisha Mungu na upuuzi kama unavyodai.
"Mungu wetu ni mwema sana. Ameiongoza na kuilinda timu yetu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) hadi ilipofikia. Ameipa alama ilizonazo sasa na kesho anaipa nafasi na baraka za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Kesho ni siku yetu."


Unaweza thibitisha hayo maneno yako?
 
Msisahau tu kuwa hakuna project aliyogusa bashite ikafanikiwa.Kesho kipigo tu.tukijitahidi sana basi itakuwa sare tu.
Nasikiaga bwana yule kwenye kamati ana Waganga km Laki tatu hivi nadhani ndo maana wanajiamini watashinda na Lesotho atafungwa ili tufuzu na bia ziwe nusu bei japo hapo kwenye nusu Bei Nani atafidia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi huwa sina imani sana na Taifa stars, na huyu Amunike ndo simuelewi kabisa. Bado nafkiria mara mbili mbili kuhusu kwenda taifa leo

the Legend☆
 
Binafsi huwa sina imani sana na Taifa stars, na huyu Amunike ndo simuelewi kabisa. Bado nafkiria mara mbili mbili kuhusu kwenda taifa leo

the Legend☆
C'mooon twenzetu...! Mimi leo naenda kushuhudia historia. Leo tunashinda na amunike hawezi kuchezea shillingi chooni tutashuka hata jukwaani kumnasa makofi akipanga mambugila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
C'mooon twenzetu...! Mimi leo naenda kushuhudia historia. Leo tunashinda na amunike hawezi kuchezea shillingi chooni tutashuka hata jukwaani kumnasa makofi akipanga mambugila.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna game ambayo iliniuma kama tuliyocheza na Lesotho Taifa, nlijuta kwenda uwanjani. Nshazoea burudani kwenye game za Simba, inauma sana kwenda uwanjani afu kurudi nyumbani kinyonge. Mungu atusaidie mambo yawe tofauti leo, na wakati huo huo tukimuombea Cape Verde awe na mchezo mzuri

the Legend☆
 
Back
Top Bottom