Taifa Stars gari limewaka

Moshi25

JF-Expert Member
May 6, 2022
1,810
2,892
Mechi ya Morocco tulianza kushanga shangaa tu hatujielewi kama tuko Afcon, baada ya kupigwa Goli moja tukaamka na kutandaza boli kama Brazil tukawabana Morocco REFA akatukandamiza kama kawaida yao kuonea underdogs akamtoa Miroshi Novatus kwa red card na kukataa kuangalia VAR ili asibadili maamuzi.

Na hapa lawama zote ziende kwa benchi la ufundi nyie mshaona Miroshi mchezaji wenu ghali mchezo umemshinda kamrukia mwenzake wa League ya Ufaransa viwili akamkosa na kupewa yellow card kwanini hamkumtoa mkamuweka Mzamiru au Bajana nyie bado mnae tu! Hapa tujifunze kuwatoa wenye yellow cards ili kuondoa hatari ya kucheza nusu maana underdogs huwa tunawindwa sana Afcon!

Mechi ya Zambia tukawapiga goli safi na kwakuwa hatujazoea kushinda tukazembea hatukujituma tena wakatupiga goli la kizembe wakiwa kumi uwanjani. hili hatutawasemehe nyie wachezaji, hili halikubaliki!

Mechi ya tatu DR Congo tuliwabana sana na leo nimejua kumbe Taifa Stars tuko vizuri mno kuzuia, jamaa hawakuonekana kabisa boli lao. Tukaamua tu tusifungwe , hatuendi mbele wala nini, hata kusema tujilipue hamna, eti tunalinda rekodi tusifungwe mechi mbili, nikashangaa sana tunachezea mpira kwetu muda wote wakati tulikuwa na uwezo wa kujaribu ku force goli ambalo lingetupeleka raundi ya pili! hapa mwalimu wa saikolojia anahitajika pale Taifa Stars kusaidia viongozi na wachezaji maana haikubaliki wachezaji kukaa nyuma kuzuia na kulinda ili tupate droo wakati tunahitaji ushindi ili kusonga mbele, timu yetu ilitakiwa kujilipua kusaka goli na kutojali kufungwa maana droo waliyoilinda haikuwa na faida yoyote! huu ni ujuha! hii haikubaliki!

Timu ya Taifa Stars safari hii imepiga hatua kubwa, inachokosa ni psychologist!

Timu inahitaji kucheza mpira wa kibabe (aggressiveness) kwenda mbele kushambulia na si kukaa nyuma kutengeneza rekodi za droo zisizotusaidia!

Sasa tuanze kushindana na si kushiriki!

Tukutane tena ile Afcon ya kwa Mkapa !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom