Nauona ushindi wa Taifa Stars hapo kesho lakini Kamati ya Ushindi ina ukakasi. Kesho tunaandika historia mpya!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,267
25,817
Mungu wetu ni mwema sana. Ameiongoza na kuilinda timu yetu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) hadi ilipofikia. Ameipa alama ilizonazo sasa na kesho anaipa nafasi na baraka za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Kesho ni siku yetu.

Uwepo wa wachezaji wetu wanaocheza nje na ndani ya Tanzania kupambana na majirani zetu Uganda ni kiashiria tosha cha kufuzu kwetu na kuandika historia mpya ambayo itakumbushia kufuzu kwetu mwaka 1980,mwaka ambao sina hakika kama kuna mchezaji yeyote atakayecheza kesho alizaliwa. Nauona ushindi wetu kesho.

Imeundwa Kamati ya Kuhamasisha ushindi wetu hapo kesho. Kwakuwa mimi si rafiki wa unafiki,nauona ukakasi wa wazi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Paul Makonda,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kamati imejumuisha watu maarufu tu ambao hata danadana mbili hawajawahi kupiga.

Kamati ya Makonda inapoteza lengo. Ushindi wa timu huanzia kwa wachezaji na si watazamaji au mashabiki. Kutingwa na watazamaji na mashabiki badala ya wachezaji ni kupoteza uelekeo. Kesho unachezwa mpira. Mpira si kama siasa inayotegemea porojo,propaganda na utapeli. Soka ni muunganiko wa uwezo wa wachezaji na saikolojia yao.

Naamini Tanzania ina wachezaji wenye vipaji. Kati yao wanaunda timu ya Taifa. Kinachopungua miaka yote ni kukosekana kwa saikolojia ya kujiamini,kupambana kwa ajili ya taifa letu,kujitoa na kuwa makini kwa kila sekunde ya mchezo. Kamati ya Makonda ilipaswa kujielekeza huku.

Kamati ilipaswa kujumuisha baadhi ya mashujaa wetu wa 1980 walio hai ili kuwaaminisha watoto wao wanaocheza kesho kuwa kila jambo linawezekana. Wapi akina 'Computer'? Anaingiaje Haji Manara akaachwa Sunday Manara baba yake na mmoja wa mashujaa wa 1980? Isigeuzwe ni Kamati ya sherehe kabla ya ushindi!
 
Tuta toa sare inatutosha kututoa mashindanoni ili tuendelee na siasa zetu
Mungu wetu ni mwema sana. Ameiongoza na kuilinda timu yetu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) hadi ilipofikia. Aneipa alama ilizonazo sasa na kesho anaipa nafasi na baraka za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Kesho ni siku yetu.

Uwepo wa wachezaji wetu wanaocheza nje na ndani ya Tanzania kupambana na majirani zetu Uganda ni kiashiria tosha cha kufuzu kwetu na kuandika historia mpya ambayo itakumbushia kufuzu kwetu mwaka 1980,mwaka ambao sina hakika kama kuna mchezaji yeyote atakayecheza kesho alizaliwa. Nauona ushindi wetu kesho.

Imeundwa Kamati ya Kuhamasisha ushindi wetu hapo kesho. Kwakuwa mimi si rafiki wa unafiki,nauona ukakasi wa wazi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Paul Makonda,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kamati imejumuisha watu maarufu tu ambao hata danadana mbili hawajawahi kupiga.

Kamati ya Makonda inapoteza lengo. Ushindi wa timu huanzia kwa wachezaji na si watazamaji au mashabiki. Kutingwa na watazamaji na mashabiki badala ya wachezaji ni kupoteza uelekeo. Kesho unachezwa mpira. Mpira si kama siasa inayotegemea porojo,propaganda na utapeli. Soka ni muunganiko wa uwezo wa wachezaji na saikolojia yao.

Naamini Tanzania ina wachezaji wenye vipaji. Kati yao wanaunda timu ya Taifa. Kinachopungua miaka yote ni kukosekana kwa saikolojia ya kujiamini,kupambana kwa ajili ya taiga letu,kujitoa na kuwa makini kwa kila sekunde ya mchezo. Kamati ya Makonda ilipaswa kujielekeza huku.

Kamati ilipaswa kujumuisha baadhi ya mashujaa wetu wa 1980 walio hai ili kuwaaminisha watoto wao wanaocheza kesho kuwa kila jambo linawezekana. Wapi akina 'Computer'? Anaingiaje Haji Manara akaachwa Sunday Manara baba yake na mmoja wa mashujaa wa 1980? Isigeuzwe ni Kamati ya sherehe kabla ya ushindi!

In God we trust
 
Kwanza namshukuru alie juu MWENYEZI MUNGU kwa kuniwezesha kuandika uzi huu. Yaa rabbi nakuomba mechi ya kesho tufungwe nyingi ili mara nyingne tujue kuwekeza katika mpira. Ilikua tufuzu mechi iloyopita tukafanya madudu kocha akajaza mabeki badala ya kujaza viungo ili mpira unoge hatimae tukafungwa saivi tunaomba njaa kwa wenzetu wafungwe yaa rabbi tunakuomba tufungwe akili itukae vizur sifa zimezidi.
WABILLAH TAWFIQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza namshukuru alie juu MWENYEZI MUNGU kwa kuniwezesha kuandika uzi huu. Yaa rabbi nakuomba mechi ya kesho tufungwe nyingi ili mara nyingne tujue kuwekeza katika mpira. Ilikua tufuzu mechi iloyopita tukafanya madudu kocha akajaza mabeki badala ya kujaza viungo ili mpira unoge hatimae tukafungwa saivi tunaomba njaa kwa wenzetu wafungwe yaa rabbi tunakuomba tufungwe akili itukae vizur sifa zimezidi wote tuseme ""AMIN""

Sent using Jamii Forums mobile app
Tufungwe mabao 200 ikiwezekana!
 
Mimi hofu yangu kubwa ipo kwa kocha wetu Amunike! Ni vigumu sana kumtabiria huyu kocha kwenye upangaji wake wa timu.

Alichotufanyia kwenye mechi ya marudio dhidi ya Lesotho ambayo kimsingi tulitakiwa tufuzu siku ile, itabakia kuwa kumbukumbu tosha mioyoni mwa watanzania wengi wapenda soka.
 
Back
Top Bottom