Naumwa Mwili Mzima

komedi

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
204
17
Jamaa alifika kwa daktari akipiga yowe la maumivu makali na mazungumzo yakawa hivi:

Daktari: Tatizo nini ndugu?

Mgonjwa: Daktari hali ni mbaya sana, mwili mzima unauma yaani kila kiungo ninachokigusa kinauma.

Daktari akamgusa kama maeneo mawili hivi na kumuuliza kama anasikia maumivu akasema hasikii.

Daktari: Sasa kumbe huumwi?

Mgonjwa: Daktari ninaumwa sana siwezi hata kuelezea, yaani kila kiungo ninachokigusa kinauma mno daktari, labda huwezi kunitibu niambie, au kama huuoni ugonjwa inawezekana nimelogwa, niambie tu mi niende Loliondo.

Daktari: Ebu nionyeshe gusa nione unavyoumwa.

Mgonjwa akanyoosha kidole chake na kujigusa kichwani ''aaaagh'' akapiga kelele, kisha akanyoosha kidole akajigusa puani ''ooooohghhh!!'' akapiga yowe kwa maumivu, baadaye akajigusa begani ''aaaaaghhh''

Daktari: Umevunjika kidole ndugu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom