Naumia sana; nifanyeje?

Naumia sana; nifanyeje?

Wewe ni msiri ambao haukusaidii kitu. Mfano ulipoenda kuonana na huyo jamaa ili akupe hela hukumwambia mpz wako ndio maana hakukuelewa laiti ungemwambia isingekuwa hivyo.
Tulia mpz achana nae na wala kwenye harusi usiende hana mpz mema nawe.
Usijilaumu coz uwezi jua km ungeolewa nawe kingetokea nin?
Maamuzi sahihi ni yale ambayo baada ya maamuzi unakuwa salama km ulivyo salama saaa.
 
kweli mwanamke akipenda anapenda vibaya, yaani mwaka na nusu bado ulikuwa unamngoja arudi, pole sana jaribu kukubali situation, tafuta mwingine.

Hili ndo tatizo tukipenda tunapenda kweli.
Namwonea HURUMA.akubali matokeo asonge mbele.inauma sana
 
pole sana kwa yaliyo kusibu mrembo..
cha muhim cool down kwanza maana inaelekea una speed saana ya kumaliza hili swala..
kikubwa tambua kwamba limeshatokea na kubaliana na matokeo..kama ameshafikia hatua ya kuoa jua kashagive up na wewe na hauna thaman tena maisha mwake..
pia waweza badilisha mfumo wa maisha na jiamin na kujiheahim maana wanaume wako weng huwez kukosa wa kukuoa kama una maadili mazuri..
pia iwe fundisho yaan ukiwa kweny deep relationship usikubal kujiingiza kweny mazingira ambayo mwenzio kwa namna yeyote atahis una mdanganya..
mwisho huyo jamaa ako inaelekea uwezo wake wa akil na wakhpambanua mambo ni mdogo maana kuambiwa tuu kua wewe unatoka na mbaba flan sio kigezo cha kukuacha ila angetakiwa kufanya uchunguz yeye kama yeye na sio kuambiwa kwa hiyo hakufai atakuja kukupa shida huko mbeleni..
asante.....

Thanks. Kweli ningependa nilimalize sitaki tena kuwaza mume wa mtu huyu
 
Nikisoma maandiko yako napata wazo kuwa HUENDA REAL LOVE EXISIST
 
Wewe sio wa kwanza kupatwa na mambo kama hayo. Wapo walioachwa tena kwa kutukanwa na kudharauliwa, wapo walioondokewa na wapendwa wao na wakavumilia wakasahau. Chukulia hayo ni mapito na mitihan......

Thanks. Pengine sikujiandaa na huu mtihani. Natafuta madesa 🙁
 
kwa hio anataka uende
danban.gif
kwenye harusi yake ama vipi?

please
nono.gif
go there, utaishia
crying.gif
huku wenzio waki
kiss.gif
!!!

kitendo cha
broken-heart.gif
wako, ni dhahiri kuwa alidhamiria kukuacha makusudi ili akaoe kwingine...

usishangae ukienda huko ukaishia
slapping.gif
......

Hapana siwezi kwenda kwenye hiyo harusi.
 
Wewe ni msiri ambao haukusaidii kitu. Mfano ulipoenda kuonana na huyo jamaa ili akupe hela hukumwambia mpz wako ndio maana hakukuelewa laiti ungemwambia isingekuwa hivyo.
Tulia mpz achana nae na wala kwenye harusi usiende hana mpz mema nawe.
Usijilaumu coz uwezi jua km ungeolewa nawe kingetokea nin?
Maamuzi sahihi ni yale ambayo baada ya maamuzi unakuwa salama km ulivyo salama saaa.

Sio usiri ndugu..Anyways ilishatokea na sikwenda pale kwa nia mbaya. Nipijieleza sana na sikueleweka. Shida ni kwamba taarifa zilifika kuwa tulikuwa tukipapasana na mwisho tukaongozana na huyo rafiki. Ikabidi nimwambie hadi niliyekutana naye japo alikua willing kumtafuta jamaa amwambie ukweli ila jamaa hakutaka hata kusikia.
 
Hii ni ngumu kumeza maana ni chungu kama "Ngoroti". Ambia mama Yoyoo tengenezea yeye Kloriti!
 
Saiv anaitwa mume wa mtu mtarajiwa
potezea hayo mawazo ya kuwa nae unless useme kama unataka kuwa mchepuko wake.

lakn pia sidhan kama nawewe utaendelea kuishi maisha ya kuwa mchepuko miaka yote.

hvyo basi 2liza akili utapata mwenza wako pekeako na sio wa kushare. kila la kheri ndugu
 
Pole dada. Unavyojiskia ni kawaida tena ushukuru hata kazi unaweza kufanya mpaka muda wa ziada. Huo ni mwanzo mzuri. Jipe muda wa kulia maana ni hatua ya kawaida ya kukabiliana na machungu, ila katika kulia kwako usijipe nafasi ya kujilaumu kuwa ulikosea ulipoenda kukutana na yule mtu. Hicho kilikuwa ni kisingizio, maamuzi alishayafanya. Kubali tu kuwa likuepukalo lina heri. Hii kauli utaithibitisha ukishapona majeraha. Lakini ukiruhusu kulia kwa muda mrefu utajiharibia maisha yaliyobaki kwani utapoteza muda na fursa nyingi. Kwanza kinachokusumbua ni wivu kwa sababu mlishaachana kwa mwaka na nusu. Huo mwaka na nusu uliishije bila yeye? Au ni lile tumaini la kuwa kuna siku atarudi ndo huamini kama limekufa?. Usipoangalia utaendelea kuwa na matumaini kuwa huyo mke atakufa halafu mtaoana. Hakuna namna ya kumfariji mtu akaelewa maana wengi husema sisi wafariji hatuelewi namna mnavyoumia, ila amini kuwa lililokupata ni la kawaida na huwezi kupewa jaribu kubwa kukushinda. Kuna mtu aliachwa wiki 1 kabla ya harusi na mpaka leo hajawahi kupewa sababu lakini alivuka na sasa anaishi maisha yake kama kawaida.
 
Habari zenu wana MMU!
Nilikua na bf wangu tulianza naye mahusiano 2010 bahati mbaya tulikua tukigombana mara nyingi kwasababu yeye alikua anaamini mimi nina michepuko( jambo ambalo halikuwahi kuwa la kweli). Siku moja( miaka ishapita sasa) nikakutana na a friend sehemu. Tulikutana kwa nia njema ili anikabidhi hela flani sema akachelewa kufika ikapelekea mimi kusubiri hapo mpaka giza. Anyways jamaa alikuja akanikabidhi mzigo huo, kila mmoja akamalizia kinywaji chake na kila mtu akaenda na njia zake. Bahati mbaya sana siku hii hii kuna mtu wa karibu wa huyo bf wangu aliniona( ndio alivyonambia) lakini ms aliyopeleka kwa mshikaji ni kwamba nipikuwa mahala pale na sugadaddy ambaye tulikuwa tukipapasana hadharani na mwisho wa siku tukaondoka na gari lake. Dah hii ilinistua haswa sababu kweli nilikwenda mahala pale na siwezagi kusema uongo. Nilijitajidi kumweleza jamaa hakunielewa sanasana akanitusi sana na kunambia tayari ana mtu na kwamba mi nayeye basi. Niliumia sana sababu kama ilipaswa tuachane basi ningependa yaishe kwa jinsi ya tofauti. Nami nikaona haviwezekani nikakubali yaishe na mawasiliano nikakata.

Anyhow habari yenyewe ni hii...juzi kati hapa kanitumia ms kuwa anaoa na kwamba angependa nishiriki. Niliumia sana ikabidi kuonana hadi na wachungaji nipate maombi na faraja. Niliumia mno zaidi ya kipindi alichoniacha ambapo ni zaidi ya mwaka na nusu sasa. Nakosa raha sana, ninapatwa baridi, hata sielewi naumwa wapi ila naumwa tuu dah! Najikuta nipo kazini sana zaidi ya muda wa kazi hadi weekend nakuwa huko. Hili nashindwa elezea marafiki zangu sababu naona watanipa habari za 'haikuwa mpango wa Mungu', 'subiri wako yupo' etc.Nimeshafikiria hadi kuhama nchi ila kikwazo ni fedha tu. Nafikiri muda wote nilitaraji jamaa angerudi kwangu lakini doh! Salaleee huyu si wangu milele maana sote wakristo. Nishaurini wana jamvi nifanyeje?
Kua na moyo wa subira
Utampata wako na kumsahau jamaa.utasema bora nigempata huyu mapema
 
kwa hio anataka uende
danban.gif
kwenye harusi yake ama vipi?

please
nono.gif
go there, utaishia
crying.gif
huku wenzio waki
kiss.gif
!!!

kitendo cha
broken-heart.gif
wako, ni dhahiri kuwa alidhamiria kukuacha makusudi ili akaoe kwingine...

usishangae ukienda huko ukaishia
slapping.gif
......

Jamaa unatisha duh!!!!
Like a Milion.
 
Pole dada. Unavyojiskia ni kawaida tena ushukuru hata kazi unaweza kufanya mpaka muda wa ziada. Huo ni mwanzo mzuri. Jipe muda wa kulia maana ni hatua ya kawaida ya kukabiliana na machungu, ila katika kulia kwako usijipe nafasi ya kujilaumu kuwa ulikosea ulipoenda kukutana na yule mtu. Hicho kilikuwa ni kisingizio, maamuzi alishayafanya. Kubali tu kuwa likuepukalo lina heri. Hii kauli utaithibitisha ukishapona majeraha. Lakini ukiruhusu kulia kwa muda mrefu utajiharibia maisha yaliyobaki kwani utapoteza muda na fursa nyingi. Kwanza kinachokusumbua ni wivu kwa sababu mlishaachana kwa mwaka na nusu. Huo mwaka na nusu uliishije bila yeye? Au ni lile tumaini la kuwa kuna siku atarudi ndo huamini kama limekufa?. Usipoangalia utaendelea kuwa na matumaini kuwa huyo mke atakufa halafu mtaoana. Hakuna namna ya kumfariji mtu akaelewa maana wengi husema sisi wafariji hatuelewi namna mnavyoumia, ila amini kuwa lililokupata ni la kawaida na huwezi kupewa jaribu kubwa kukushinda. Kuna mtu aliachwa wiki 1 kabla ya harusi na mpaka leo hajawahi kupewa sababu lakini alivuka na sasa anaishi maisha yake kama kawaida.

Asante sana Nandera. Yaani ushauri wako umeingia moyoni moja-kwa-zote. Mpaka nimeshangaa maan narudiarudia ujumbe hapa. Baadhi ya uliyoyaandika ni mawazo ambayo nishayawaza sana. Mapenzi kweli ni kizungumkuti
 
Kama kuna kitu ambacho huwa nakipinga sana ni kutopeana taarifa kuhusu movement zako kwa mpenzi wako. Kwa nini hukumwambia unaenda wapi na kufanya nini. Maybe hata angekusindikiza....
 
Una tatizo moja tu na hamna kingine, upweke unakuumiza. Ungepata mwingine hakika ungeshasahau ya ex wako. Kitendo cha kwenda kazini na kukaa huko hadi kupitiliza mda, mwisho wa wiki pia upo huko, ni dhahiri kuwa moyo wako unahitaji kipoozeo.

Jichanganye, kama ni makongamano, kanisani na mashostito zako, na mwisho jaribu kuwa simba jike, fanya mawindo na omba Mungu akupe anayekufaa.
 
thats just the way it is....a broken heart,a broken soul.kuachwa noma sana.be strong
 
Back
Top Bottom