Naumia sana; nifanyeje?

Naumia sana; nifanyeje?

Evagrace

Member
Joined
Feb 2, 2014
Posts
45
Reaction score
13
Habari zenu wana MMU!
Nilikua na bf wangu tulianza naye mahusiano 2010 bahati mbaya tulikua tukigombana mara nyingi kwasababu yeye alikua anaamini mimi nina michepuko( jambo ambalo halikuwahi kuwa la kweli). Siku moja( miaka ishapita sasa) nikakutana na a friend sehemu. Tulikutana kwa nia njema ili anikabidhi hela flani sema akachelewa kufika ikapelekea mimi kusubiri hapo mpaka giza. Anyways jamaa alikuja akanikabidhi mzigo huo, kila mmoja akamalizia kinywaji chake na kila mtu akaenda na njia zake. Bahati mbaya sana siku hii hii kuna mtu wa karibu wa huyo bf wangu aliniona( ndio alivyonambia) lakini ms aliyopeleka kwa mshikaji ni kwamba nipikuwa mahala pale na sugadaddy ambaye tulikuwa tukipapasana hadharani na mwisho wa siku tukaondoka na gari lake. Dah hii ilinistua haswa sababu kweli nilikwenda mahala pale na siwezagi kusema uongo. Nilijitajidi kumweleza jamaa hakunielewa sanasana akanitusi sana na kunambia tayari ana mtu na kwamba mi nayeye basi. Niliumia sana sababu kama ilipaswa tuachane basi ningependa yaishe kwa jinsi ya tofauti. Nami nikaona haviwezekani nikakubali yaishe na mawasiliano nikakata.

Anyhow habari yenyewe ni hii...juzi kati hapa kanitumia ms kuwa anaoa na kwamba angependa nishiriki. Niliumia sana ikabidi kuonana hadi na wachungaji nipate maombi na faraja. Niliumia mno zaidi ya kipindi alichoniacha ambapo ni zaidi ya mwaka na nusu sasa. Nakosa raha sana, ninapatwa baridi, hata sielewi naumwa wapi ila naumwa tuu dah! Najikuta nipo kazini sana zaidi ya muda wa kazi hadi weekend nakuwa huko. Hili nashindwa elezea marafiki zangu sababu naona watanipa habari za 'haikuwa mpango wa Mungu', 'subiri wako yupo' etc.Nimeshafikiria hadi kuhama nchi ila kikwazo ni fedha tu. Nafikiri muda wote nilitaraji jamaa angerudi kwangu lakini doh! Salaleee huyu si wangu milele maana sote wakristo. Nishaurini wana jamvi nifanyeje?
 
Pole...jaribu kubadili jinsi unavyoishi itakusaidia sana.
 
kwa hio anataka uende
danban.gif
kwenye harusi yake ama vipi?

please
nono.gif
go there, utaishia
crying.gif
huku wenzio waki
kiss.gif
!!!

kitendo cha
broken-heart.gif
wako, ni dhahiri kuwa alidhamiria kukuacha makusudi ili akaoe kwingine...

usishangae ukienda huko ukaishia
slapping.gif
......
 
hahaha mkuu nimeipenda hiyo asee
kwa hio anataka uende
danban.gif
kwenye harusi yake ama vipi?

please
nono.gif
go there, utaishia
crying.gif
huku wenzio waki
kiss.gif
!!!

kitendo cha
broken-heart.gif
wako, ni dhahiri kuwa alidhamiria kukuacha makusudi ili akaoe kwingine...

usishangae ukienda huko ukaishia
slapping.gif
......
 
ukihama nchi ndo mawazo nayo yatabaki Tz?J
Huko si ku-file tatizo?kwani utakapolifungua hilo faili utayakuta hayo unayoyakimbia ww fanya maombi na tiba ya kisaikolojia tu ndo ukombozi wa kweli!Ujue ni wengi tu wanaoachika hata mie yalinikuta ,kikubwa nilifunga stronger shock absobers ili kusahau.
 
Excel mbona una makachumbalg, kama uko cngo mfariji mwenzio
 
Last edited by a moderator:
Be strong bhana,yaache yapite,utampata wa ukweli vuta subira wangu....
 
Kila kitu kinatokea kwa makusudi, we tulia endelea kumwomba Mungu utamsahau na maisha yataenda
 
LOVE WITH A GAPE. Usilalie mlalo wa ukuta. Je mvua zikizidi si utaanguka na huo ukuta? Haya kaondoka, weye huli, hulali ati nimeachwa! We wa kwanza? Amka uangaze weye mwanamke. Hajaondoka na chako wala hakukuachia chake, shida iko wapi? Mjibu vizuri tu kuwa weye upo tu, ya kale hayanukii.
Mwambie bado moyo wako upo wazi kwake. Akijichokea huko aje tu ila akikuta mwingine kwako asiumie. Ngoma droo hiyo.
 
Excel mbona una makachumbalg, kama uko cngo mfariji mwenzio
Evagrace sidhani kama atakubali mwaya!!... si keshaumizwa huko na playboy.. sasa mi straika nikiimbisha sijui ataachia goli nitie nyavu?.. ngoja nijae kwenye 18 zake, akinitema narudisha feedback MMU..! lols..
 
Last edited by a moderator:
pole sana kwa yaliyo kusibu mrembo..
cha muhim cool down kwanza maana inaelekea una speed saana ya kumaliza hili swala..
kikubwa tambua kwamba limeshatokea na kubaliana na matokeo..kama ameshafikia hatua ya kuoa jua kashagive up na wewe na hauna thaman tena maisha mwake..
pia waweza badilisha mfumo wa maisha na jiamin na kujiheahim maana wanaume wako weng huwez kukosa wa kukuoa kama una maadili mazuri..
pia iwe fundisho yaan ukiwa kweny deep relationship usikubal kujiingiza kweny mazingira ambayo mwenzio kwa namna yeyote atahis una mdanganya..
mwisho huyo jamaa ako inaelekea uwezo wake wa akil na wakhpambanua mambo ni mdogo maana kuambiwa tuu kua wewe unatoka na mbaba flan sio kigezo cha kukuacha ila angetakiwa kufanya uchunguz yeye kama yeye na sio kuambiwa kwa hiyo hakufai atakuja kukupa shida huko mbeleni..
asante.....
 
Back
Top Bottom