Nina hisia kali sana za huzuni nifanyeje hii hali iniondoke?

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari za wakati huu ndugu zangu

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30+ , sijaoa na wala sina mpenzi wakudumu yaani mwanamke wakuoa bado sijapata..

Nimekua nikikutana na hali ya huzuni sana na kuumia moyo au kusikia kama kulipuka ndani ya moyo wangu ninapo kutana na mazingira kama haya ndugu zangu na hali hii ilianzakunikuta miaka mitatu iliyopita baada ya kuachwa na mwanamke niliempenda sana kwa kweli

1: Nikiona na kusikia mwanamke analia napatwa na huzuni kuu moyoni na kujisikia kuumia sana kiasi kwamba naondoka eneo hilo na kama ni maeneo ninamo ishi na vaa earphone au kuweka sauti kubwa kwenye radio nisisikie chochote

2: Naumia sana kuona mwanamke akiwa anapigwa inaniuma sana moyoni mwangu

3: naumia sana kuona watu wa kigombaa hasa hasa watu wazima au wakiwa wanaongea kwa uchungu sana inaniuma kweli

4: Ninapopata taarifa za kuhuzunisha kama misiba, magonjwa kwa watu wanao nizunguka , ajali yeyote inaniuma sana nina huzunika sana

5: Moyoni wangu umekua unahuzunika sana hasa hasa pale ninapo ona mtu mzima analia kwa sauti au ninapo ona machozi ya mtu mzima na migogoro nakua na huzunika sana

6: nikiangalia movie au kusikiliza story zenye maudhui ya kusikitisha au ukorofi na patwa na huzuni kali pia

Nb.. Huzuni zinapo nijia muda mwingine zinaambatana na mwili mzima kutetemeka kama mtu aliepigwa na baridi kali na nakua naongea kwa kutetemeka sana ( kwa kung'ata meno)

NIMEHANGAIKA SANA NA WATAALAMU WA AFYA KUTATUA HILI TATIZ LAKINI KWA KWELI NAONA NAO WAMESHINDWA MPAKA WANAFIKIA MAHALI KUNIAMBIA NIWE NAOMBA SANA

Naombeni msaada ndugu zangu , nifanyeje ndugu zangu
 
Jitahidi Kuchamgamana na masela kwa Kuangalia mpira sana, kukaa kijiweni kidogo huko utakutana na washkaji ambao nadhani watabuti mood yako
 
Dah pole sana ndugu kiujumla sijui mazingira unayoishi na watu wanao kuzunguka yani km una marafiki au unaishi na ndugu, nafikiri tatizo lako linahitaji zaidi kua karibu na watu yani jamii yako, unapaswa kupata muda wa kuchanganyikana na watu muongee mfurahi, penda kufanya vitu vitakavyokupa furaha zaidi kuliko vitakavyokupa huzuni pia tambua maisha yako ni yako utamuonea huruma mtu lakini matatizo yake yakiisha akaondokana na huzuni yake wala hatokumbuka km uliumia au kuuzunika juu yake ataendelea na maisha yake , chagua kujipa furaha zaidi bila kujali matatizo ya mtu sababu matatizo tumeumbiwa wanandamu
 
Jifunze kuchukulia vitu kawaida yan mazingira mengi unyokumbana nayo yana matukio ya huzuni kutokana na maelezo yako, naona ujitahidi kuona n mambo ya kawaida kutokea kwenye jamii usijiruhusu kupata huzuni.
 
Naweza kujibu swali lako kwa NJIA 2

Kwanza nadharia ya ulimwengu usoonekana huenda ukawa una jini la kike/jini muoga hivyo anakuathiri mpk wewe.

Njia ya kawaida ni kwamba saikolojikal upo affected labda mwanamke wako ulimuumiza mpk unajiona mkosa kiasi Cha kukiathiri mwenyewe au Jambo jengine mwili unazalisha homoni ambazo hazistaili kitokana na kutofanya MAPENZI mda mrefu.

Fanya uoe.
 
Dah pole sana ndugu kiujumla sijui mazingira unayoishi na watu wanao kuzunguka yani km una marafiki au unaishi na ndugu, nafikiri tatizo lako linahitaji zaidi kua karibu na watu yani jamii yako, unapaswa kupata muda wa kuchanganyikana na watu muongee mfurahi, penda kufanya vitu vitakavyokupa furaha zaidi kuliko vitakavyokupa huzuni pia tambua maisha yako ni yako utamuonea huruma mtu lakini matatizo yake yakiisha akaondokana na huzuni yake wala hatokumbuka km uliumia au kuuzunika juu yake ataendelea na maisha yake , chagua kujipa furaha zaidi bila kujali matatizo ya mtu sababu matatizo tumeumbiwa wanandamu
Asante nashukuru ndugu yangu
 
Mkuu pita eneo la jeshi nenda kawachokoze ,wakupe kipondo kweli kweli ,...

Au pita sehemu za wavura bangi wazingue ili wakupe kipigo hatari ...

Hapo ndio roho ya huruma na kulia Lia itakutoka na kuona kawaida watu wakiwa wanalia ...
 
Naweza kujibu swali lako kwa NJIA 2

Kwanza nadharia ya ulimwengu usoonekana huenda ukawa una jini la kike/jini muoga hivyo anakuathiri mpk wewe.

Njia ya kawaida ni kwamba saikolojikal upo affected labda mwanamke wako ulimuumiza mpk unajiona mkosa kiasi Cha kukiathiri mwenyewe au Jambo jengine mwili unazalisha homoni ambazo hazistaili kitokana na kutofanya MAPENZI mda mrefu.

Fanya uoe.
Nashukuru
 
Back
Top Bottom