Mr Suggestion
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 605
- 317
Umeona mbali yaani wananchi wana haki ya kumvunjia waziri heshima ila wao ndio waheshimiwe,hakuna haja ya kuomba msamaha aliyetuambia atanunua ndege hata kama wananchi watakula majani alishawahi omba msamaha?wapi na lipi?Magufuri fanya kazi ww ndio kioo cha mawazir wote wa Jk,lakusimamia madaraja yaliyoharibiwa wakat wa mafuriko hawalioni wanaliona la feri tu watu wa dar acheni Mtemvu acha unafiki,mi siamini kama wazaramo wana jina linaloanzia na mtemvuHapa ndio mnapokosea....Magufuli alitoa kauli ile baada ya kuzomewa! hakuna anayesema wananchi waombe msamaha kwa kuzomea.......
So, unadhani kwa wananchi wa Kigamboni ni fair kabisa kuchangishwa nauli kusaidia usafiri wa watu wa Bagamoyo? Kwa nini wasichangishwe hizo nauli ziwajengee daraja ili kuepukana na kero ya usafiri? Which fair: Wananchi wa Kigamboni kuchangishwa ili kununua kivuko cha watu wa Bagamoyo au kuchangishwa ili kujengewa daraja na kuachana na karaa za pantoni?
It doesn't matter whether is doing business or delivering services. A responsible government should gradually increase the price of its services to equate it to the economic cost of running them. A gradual increase in prices to allows the consumers to adjust to the changes and also provide time for consumers to find alternatives. Siyo unakaa miaka 14 kimya, halafu unapandisha bei ghafla bila hata transparency and effective participation. Au kwa vile wananchi wa Kigamboni wana limited alternatives za usafiri ndio wabambikiwe nauli mpya ghafla?
Hapana mkuu sio absurd hata kidogo ikiwa umenielewa nadhani wewe umechukulia hivyo..Kwa nini tuna-avoid maswali magumu? Comparison yako ya kutopandisha nauli kwa miaka 14 na kutojenga daraja kwa miaka hamsimi naona kama ni absurd. Hapa serikali ilikuwa na uwezo wa kupandisha nauli kulingana na gharama za uendeshaji lakini haikufanya hivyo kwa muda wa miaka 14.
Hivi unafananisha vipi Hiace na Bus? Ni watu wangapi wanavuka Pangani kwa kila trip moja na ni watu wangapi wanavuka Kigamboni? Naamini hiyo 100 kwa Kigamboni ni sawsawa na na hiyo 200 kwa Pangani itakuwa sawa kwa sababu kuna muda hiko cha pangani Kinavuka tupu kwenda upande wa pili kufuata abiria likini hiki cha Kigamboini kikienda ni NYOMI na kiki rudi pia ni NYOMI.
Mchambuzi,
Ahsante kwa mada 'serious' na sio sensitive kama ulivyosema. Wakati mjadala ukipamba moto naomba niweke kumbu kumbu sawa kwasababu kuna mambo tunayasahau au kuyafumbia macho.
1. Hoja ya awali ya mbunge wa Kigamboni ilikuwa kueleza kuwa magufuli hakufuata taratibu kupandisha nauli na kwamba hilo ni jukumu la SUMATRA. Hoja haikuwa kiwango bali utaratibu.
2. Magufuli amenukuliwa na gazeti moja akisema dhumuni hasa ni kukusanya pesa ili ziweze kununua boti itakayohudumia Bagamoyo na Dar kupunguza msongamano. Hajasema kuna tatizo kivukoni bali ana 'source' vyanzo vingine kwa ajili ya Bagamoyo
3.Hakuna anayejua pesa za maegesho za Kingunge zilitumika kuhudumia nini hadi leo, watu walilipa.
Ubungo terminal bado tunalipa tukiingia bila ruzuku
4. Tunatumia usafiri wa dala dala usio na ruzuku ya serikalini. UDA ilikuwa na ruzuku kama shirika la umma.
Kwahiyo mkazi wa mbagala anayefanya kazi ubungo hana ruzuku ya usafiri kama mkazi wa kigamboni anayefanya kazi Ilala,Temeke,Kinondoni
5. Tulikubali bilioni 100 alipwe mtu, hatukuona mshikamano wa wabunge kimkoa au kitaifa.
6. Ongezeko la posho za wabunge katika malaki ni asilimia 200. Ongezeko la nauli za feri katika mia ni asilimia 100.
Ikumbukwe 'charity begins at home'. Hatujaona mshikamano wa wabunge kwenye posho
7. Kuna vivuko vingine nchini vina nauli kubwa kuliko ya feri Kigamboni.
Ukiongea kwa mantiki hiyo unataka Kigamboni walipe tshs 50? Hoja yako ni kwamba kwasababu Kigamboni kinajaza mapato yanayakusanywa ni mengi na yanakidhi gharama za uendeshaji? Ukisema hivyo wananchi wa sehemu ambao walipa zaidi wanaweza kudai kwasababu wao wanapungufu ya shughuli za kiuchumi kitu ambacho serikali imechangia kwa kiasi kikubwa wasifiri bure; hivi labda nikuulize hiyo tsh 200 ina thamani gani sasa hivi? Ukiangalia thamani ya shs ni kama bado wanavuka bure.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Tatizo langiu ni Nauli ya GUTA linalo beba, VIAZI, MAGIMBI, EMBE na mazao mengine kuja huku soko la TANDALE kwa nauli ya kutoka 300 mpaka 1800 , sijuhi bei itapanda vipi?Mkuu vivuko vingi hapa nchini vimenunuliwa kwa mkopo toka World Bank. Ni vichache sana tumenunue kwa pesa zetu. Lakini jamani mbona hatujiulizi ni kwa nini bei ya sukari imepanda kutoka 500 hadi 2,000 kwa kilo ma hatukugoma. Watu wa kigamboni waligoma kulipa bei ya sukari baada ya kupanda? Sishangilii kupanda kwa nauli kwa kuwa kuna kiloo kwamba kuna ivujaji wa mapato hapo feri. Serikali ingeziba kwanza mianya kisha ikapandisha nauli
Itabidi wafanya biashara mbadilishe utamaduni wa kutumia guta badala yake mtumie usafiri wa magari yanayobeba vyakula na kusambaza sehemu hizo...Wakulima waunde Union au cooperative ambayo watakuwa wakikusanya mazao yao tuseme soko la Kariakoo na wanunuzi wanatoa Order zao za vyakula kisha magari yatasambaza mji mzima hadi Kigamboni.Tatizo langiu ni Nauli ya GUTA linalo beba, VIAZI, MAGIMBI, EMBE na mazao mengine kuja huku soko la TANDALE kwa nauli ya kutoka 300 mpaka 1800 , sijuhi bei itapanda vipi?
Mkuu wangu unajua vizuri sana kwamba nyumba za Msajili au NHC zinapangishwa chini ya kiwango chake na watu wengi sana wana abuse mteremko waliopewa wakipangisha nyumba hizo hizo kwa wahindi in dollars up to 1,500 a month..Mchambuzi,
..nadhani kivuko cha Kigamboni kina wateja wengi zaidi na ndiyo maana it makes sense kutoza nauli ndogo zaidi ya huko Pangani au Kilombero. naamini hata mtu binafsi atapenda kufanya biashara Kigamboni as compared to Kilombero.
..nauli zilizopanda siyo za abiria tu, bali hata za maguta, magari makubwa na madogo etc etc. sijui kwani watu wameshikana mashati kwenye nauli za abiria tu.
..kinachotakiwa kufanyika ni uhakiki wa mapato na gharama za uendeshaji wa kivuko cha kigamboni. Wabunge wamependekeza kufanyike uhakiki huo kabla ya kupandisha nauli lakini Magufuli amekataa.
NB:
..MAGUFULI AACHE LUGHA ZA KEJELI NA DHARAU KWA WALE WANAOTOFAUTIANA NAYE. MIMI NI MTU MZIMA KIDOGO NA NAKUHAKIKISHIA SIJAWAHI KUONA WAZIRI ASIYE MSIKIVU NA ALIYEKOSA STAHA KTK MAJIBU YAKE KAMA JOHN POMBE MAGUFULI.
embu tuliweke hili suala kwenye context ifuatayo, maana tufike mahali tuwe tunalinganisha maembe kwa maembe (samahani kama input ya namna hii tayari imekwishatolewa na mchangiaji mwingine)...........
mimi ni mkazi wa dar, naishi manzese. sina uwezo wa kulipa nauli ya daladala kila siku kwenda kariakoo ambako ndipo ipo maskani ya kupatia riziki yangu. kutokana na bajeti yangu kutomudu daladala kila siku, nina option ya tz11 (kwenda kwa miguu), na nimekuwa nikiitumia miaka nenda rudi. suits me ok.
binamu yangu kombo anaishi kigamboni. ndiyo mdau mwenzangu kwenye maskani yetu pale kariakoo. nauli ya kivuko ndiyo hiyo imependa na bajeti haimruhusu ku-accomodate hii rise. kwa bahati mbaya, binamu kombo hana option ya tz11 kama yangu na (btw) hajui kuogelea hata kwenye dimbwi achilia mbali bahari.
sa naomba mnisaidie nimshauri vipi ndugu yangu kombo!?
Je angekuwa hana 100 angefanyaje?embu tuliweke hili suala kwenye context ifuatayo, maana tufike mahali tuwe tunalinganisha maembe kwa maembe (samahani kama input ya namna hii tayari imekwishatolewa na mchangiaji mwingine)...........
mimi ni mkazi wa dar, naishi manzese. sina uwezo wa kulipa nauli ya daladala kila siku kwenda kariakoo ambako ndipo ipo maskani ya kupatia riziki yangu. kutokana na bajeti yangu kutomudu daladala kila siku, nina option ya tz11 (kwenda kwa miguu), na nimekuwa nikiitumia miaka nenda rudi. suits me ok.
binamu yangu kombo anaishi kigamboni. ndiyo mdau mwenzangu kwenye maskani yetu pale kariakoo. nauli ya kivuko ndiyo hiyo imependa na bajeti haimruhusu ku-accomodate hii rise. kwa bahati mbaya, binamu kombo hana option ya tz11 kama yangu na (btw) hajui kuogelea hata kwenye dimbwi achilia mbali bahari.
sa naomba mnisaidie nimshauri vipi ndugu yangu kombo!?
Wabunge wapo sahihi,na unapozungumzia juu ya nauli usiishie tu kuitaja ile 200,angalia pia gharama za mizigo,bajaji,gari n.k.pia usisahau na nauli nyingine kutoka pale feri kwenda maeneo mengine mara kurudi,yaani mfano mwenge,mabibo n.k,inawezekana wanaopingana na wabunge hawa upeo wao wa kufikiri ndio umeishia hapo,tunawasamehe.