Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe?


hatukuchagua viongozi ili tuwatukane na kuwadhalilisha, sifa moja ya kiongozi ni kutokuonewa, wao ni watu wanatokana na jamii yetu, kama tunafanya mambo ya kijinga tunategemea nini? hiyo ni 1-1, sitoe haki kwa mtu kumtukana kiongozi matusi ya nguoni.
kama kuna umuhimu wa yeye kuomba Radhi basi na walio mtukana wachukuliwe hatua, tubadilike wote, sio kutimuana kiasa mwingine kiongozi basi aingizwe vidole mpaka machoni hapana.
 

Serikali ikisema haina ruzuku kwa Kigamboni, tutawauliza mbona mnapandishiana posho Bungeni? Mbona mna wabunge wa viti maalum 100 bungeni tunaowalipa kwa kuzaliwa wanawake tu? Mbona safari za viongozi zinakuwa na msururu wa watu, kisha first class, na hatuelewi faida yake? ...
 
Reactions: EMT
Na mimi mlalahoi naomba kutoa hoja kidogo, kama hiki kivuko kinaendeshwa na serikali naomba sisi waenda kwa miguu tusilipe kitu. Swali la nyongeza ni je ikijengwa daraja, itakuwapo na njia ya wapita kwa miguu na ikiwepo je tutatozwa nauli ?

iwapo ferry hadi posta ni umbali wa kutembea kwa miguu wa kama km 3, lakini wengi wanalipa nauli ya daladala sh 300,badala ya kutembea, kwa mtazamo wako, unadhani kweli wananchi watatembea juu ya daraja lile kwa umbali wa km sio chini ya saba kutoka kurasini hadi kibada? personally, i doubt it;
 
Mkuu mchambuzi,
Hilo daraja feasibility yake siyo kwa usafiri wa wakazi wa Dar tu.
Pamoja na mambo mengine ni upanuzi wa container terminal ya Dar port, kitu ambacho ni muhimu sana as stipulated in the Southern corridor development schemes.
Very very economically feasible. I stand to be corrected but I'm for it!
 

nakubaliana na wewe katika hilo, ingawa in the long run; nilikuwa naongelea economics zetu hizi za sasa za magari, sijui maguta, wapita kwa miguu;
 

Ni muhimu kuwa iwekwe japo kama itatumika kwa watu wachache sana. Pia ninadhani pantoni liendelee kuwepo japo daraja likijengwa ili kurahisisha hali ya usafiri jijini
 
Totally agree with your angle.
Ila, ni afadhali tuachane na ruzuku kwa watu ambao kiukweli wanaweza kumudu 200 shs.
Na hayo mafedha ya posho yaelekezwe kwenye ruzuku za social services.. eg Healthcare and Education for the needy.
 
Totally agree with your angle.
Ila, ni afadhali tuachane na ruzuku kwa watu ambao kiukweli wanaweza kumudu 200 shs.
Na hayo mafedha ya posho yaelekezwe kwenye ruzuku za social services.. eg Healthcare and Education for the needy.

Totally.

But the government needs to come with other austerity measures. Sio watuambie Kigamboni tu
 

Nimesoma mahali kuwa kwenye kivuko cha Likoni huko Mombasa ambacho ni sawa na cha Kigamboni, abiria wanavuka bure. Eti kinachotozwa kodi ya kuvuka ni vyombo vya moto tuu ikiwamo magari na pikipiki. Hivyo, gharama za kuendeshea kivuko hicho zinatokana na kodi za vyombo vya moto. Hili linawezekana kwa kivuko cha Kigamboni?
 
Totally.

But the government needs to come with other austerity measures. Sio watuambie Kigamboni tu
Yep,
Hawa wabunge na viongozi wa ngazi za juu serikalini lazima tuwakabe!... ikibidi mtu afikirie mara kumi kama anataka uongozi wa nchi hii.
We don't need to play games with them... kuna watu humu wanapenda kuwachekeachekea hawa wabunge.. I hate that!
They need to be against the ropes all the time, ikiwezekana wawe wanakaa mabwenini wakati wa vikao...
Mbona US wabunge wanakaa hostel?, personally naijua hostel moja ipo K street, DC... hapo ma congressmen hujibanza wakitoka kwao. Real talk.
 

Hili linawezekana sana!
Tatizo kubwa la nchi yetu, kitu ambacho nishawahi kumuandikia mpaka January ni efficiency.
Hawa wabunge wetu vijana hawataki kuwaudhi wananchi. Hawataki kuwaambia kuwa Tanzania is the least efficient country in the world after Uzbekistan.
We really need to address this, but oh well.... kuna uchaguzi wa madiwani Arusha, mabbe Wawi, Morogoro, Kigoma etc... wataanza umbea muda si mrefu.
Yaani wananitia kichefuchefu!!
 
Reactions: EMT

Technically sirahisi kulinganisha tu kama hivyo, kuna vitu vingi vinachangia

Kwa mfano traffic ya magari na vyombo vyengine kwenye pantoni ni kubwa kiasi gani ukilinganisha na gharama za usafiri? Traffic ya magari na vyombo vyengine ipo wakati wote au ni wakati wa kwenda na kutoka makazini tu?

Juu ya kusema hayo, kuna vingi ambayo Tanzania inaweza kufanya lakini haifanyi kwa sababu wananchi hatupo tayari. Tukiwa tayari serikali itatekeleza
 
Reactions: EMT

Hivi unafananisha vipi Hiace na Bus? Ni watu wangapi wanavuka Pangani kwa kila trip moja na ni watu wangapi wanavuka Kigamboni? Naamini hiyo 100 kwa Kigamboni ni sawsawa na na hiyo 200 kwa Pangani itakuwa sawa kwa sababu kuna muda hiko cha pangani Kinavuka tupu kwenda upande wa pili kufuata abiria likini hiki cha Kigamboini kikienda ni NYOMI na kiki rudi pia ni NYOMI.
 

Ukweli ni kuwa Kigamboni ni Nyomi Nyomi wakati wote( Na ndio maana wakajenga kipya kikubwa zaidi na mara nyingi vina operate Viviwili kimoja ngambo na kingine ngambo nyingine vinapishana katikati), watu kibao, Magari Kibao sasa inakuwaje wanakifananisha na cha Kilomberro, Ambacho mara nyingi kinaenda Tupu?
 

Bongo TAMBARARE, Kigam,boni unaweza ukakuta kuna wafanyakazi zaidi ya 200, na uchakachuaji wa mafuta ni kitu cha kawaida kabisa, sasa unategemea nini?
 
Reactions: EMT
Totally agree with your angle.
Ila, ni afadhali tuachane na ruzuku kwa watu ambao kiukweli wanaweza kumudu 200 shs.
Na hayo mafedha ya posho yaelekezwe kwenye ruzuku za social services.. eg Healthcare and Education for the needy.

Hivi tatizo ni 200? au Tatizo ni UBADHIRIFU?
 
Tatizo lipo hapa, Wengi wakina nani? Vibopa wenzio wa CCM? AU? Tuwe wa kweli wakazi wakigamboni majority hawawezi kulipa hiyo 300 kwa km 3, Tuache huongo, Mnaolipa hiyo nauli ni Nyie wahuko Mwenge, Masaki na Mbezi, Ili kugeuza na hayo magari mpate siti.
 
Ni muhimu kuwa iwekwe japo kama itatumika kwa watu wachache sana. Pia ninadhani pantoni liendelee kuwepo japo daraja likijengwa ili kurahisisha hali ya usafiri jijini
Mkuu daraja likijengwa panton itaendelea kuwepo kama kawaida. Mkuu nina shaka kwamba hilo daraja litakuwa la kulipia kwa kuwa huu ni mpango wa (PPP). Tutasikia wiki ijayo kwa kuwa ndio ujenzi wa daraja utakuwa unazinduliwa rasmi. Lakini asilimia kubwa ni kwamba hilo daraja litakuwa la kulipia.
 
Mkuu vivuko vingi hapa nchini vimenunuliwa kwa mkopo toka World Bank. Ni vichache sana tumenunue kwa pesa zetu. Lakini jamani mbona hatujiulizi ni kwa nini bei ya sukari imepanda kutoka 500 hadi 2,000 kwa kilo ma hatukugoma. Watu wa kigamboni waligoma kulipa bei ya sukari baada ya kupanda? Sishangilii kupanda kwa nauli kwa kuwa kuna kiloo kwamba kuna ivujaji wa mapato hapo feri. Serikali ingeziba kwanza mianya kisha ikapandisha nauli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…