Mtoa mada umewasilisha hoja kwa mapana na marefu yake, ila kuna takwimu hapa hazijakaa sawa: -
Umesema gharama kwa sasa ni 98% ya (9,000,000) mapato kwa siku kwa nauli ya Tsh 100. Na ukasema nauli ikiwa Tsh 200 salio litakuwa ni sh.333, 332 (laki tatu), badala ya Sh. 166,666? Si kweli. Nauli ikiwa Tsh. 200, Salio litakuwa ni Tsh. 166,666 ongeza 9,000,000 (itayotokana na ongezeko la tsh 100 ktk nauli mpya) mana gharama zitakuwa covered na ile 98% ya 9,000,000 ya mwanzo wakat nauli ni Tsh 100 na sio kuwa nauli ikiongezeka kuwa 200 gharama nazo ztaongezeka kuwa 98% ya (9,000,000+9,000,000).
Pia ungetueleza gharama za uendeshaji kwa kina, Makusanyo kutoka kwenye nauli na ruzuku/subsidy ya serikali kwa siku/mwezi kabla ya kusema kwamba nani yupo sahihi au yupo wrong. Na imani kupitia kivuko hicho serikali inatoa huduma na sio kuwa inafanyabiashara, hivyo hatutegemei serikali kuweka kiwango ambacho kitamuumiza mwananchi as if serikali inafanya biashara. Kama unasema katika uendeshaji wa kivuko hicho zaidi ya nauli wanazotozwa wananchi kuna ruzuku ya serikali. Nina imani kubwa either hiyo ruzuku ni ndogo sana au haipo kbs au kama ipo basi kuna ufisadi mkubwa unaofanyika. Na labda pengine ndio msingi wa kelele za Wabunge
Mana kwa harakaharaka nimegawanya hicho kiasi ulichokitaja cha gharama za uendeshaji (Tsh8.8m) kwa tsh 2000 ya diesel kwa lita. Nimepata jumla ya liter 4400 za diesel zinatumika kwa siku. Ila kwa kuwa kuna mahitaji mengine ktk kuendesha panton hizo, assume lita 500 i.e 1,000,000/= kwa siku itacover hayo mahitaj mengine km grease, mishahara n.k. Bado liter 3900 kwa siku ni nyingi mno kwa matumizi ya panton mbili labda kama kuna mengine ila siamin kwamba gharama za uendeshaji wa panton hizo mbili kwa siku ni tsh Tsh 8.8m.