Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe?

Yeah right!! ... lol.
 
Tatizo langiu ni Nauli ya GUTA linalo beba, VIAZI, MAGIMBI, EMBE na mazao mengine kuja huku soko la TANDALE kwa nauli ya kutoka 300 mpaka 1800 , sijuhi bei itapanda vipi?

I think jamaa wanafikiri vizuri, sisi ndio bado tuko usingizini; which will be cheaper to wananchi wa Kigamboni; viazi vilivyovushwa na lori tani 7 (Kg. 7000) (linalolipa nadhani sio zaidi ya 3,000); au viazi vilivyovushwa na GUPTA (sema Kg 300) linalolipa 1800TZS, in short they are discuraging using GUPTA kusafirisha hiyo mizigo which economically makes a lot of sense.

Jamani GUPTA sio inter-city transport; let be carefully guys
 
Umetoa maneno mengi sana!!
Lakini Fact moja tu kwamba picha yako iko ki-ccm zaidi wakati mashambulizi umempelekea mnyika zaidi inafanya yoooteeee uliyoyaandika yawe kishabiki zaidi kuliko kimantiki
 

Mchambuzi,

Asante, nilishazungumza na wanahabari; unaweza kusoma tamko nililotoa ambalo linajibu pia baadhi ya hoja ulizozitaja; https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ficha-udhaifu-wa-serikali-na-wizara-yake.html

Mathalani; kuhusu hoja hii ya ongezeko la kutoka shilingi 100 mpaka 200; nimefafanua:

Waziri Magufuli ameamua kupotosha kwamba nilichompinga na kupanda kwa nauli kutoka shilingi 100 mpaka 200, na kuacha kujibu hoja kuu ambazo nilitaka azitolee maelezo na vielelezo. Ukweli ni kuwa nilichotaka kisitishwe ni utekelezaji wa agizo kupitia gazeti la serikali (GN 367) ya tarehe 4 Novemba 2011 na kuanza kutumika kwa nauli mpya kwa ujumla wake kutokana na kukiukwa kwa misingi ya utawala bora na pia baadhi ya viwango kutokuzingatia hali halisi. Kwa upande wa kupanda kwa nauli nilisisitiza kuwa kero kuu sio kupanda nauli ya mtu mzima toka shilingi 100 mpaka 200 bali kupandishwa kupindukia kwa nauli za vyombo vya usafiri na usafirishaji hali ambayo itasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa katika eneo la Kigamboni na kuathiri watu wengi zaidi. Mathalani Baskeli za matairi matatu (Guta) toka Tsh 200 hadi Tsh 1800 (Asilimia 800); bei ambayo ni kubwa kuliko ya gari ndogo; bajaj zimepanda toka Tsh 300 hadi Tsh 1300 (Asilimia 333); mikokoteni imeongezeka toka Tsh 200 hadi Tsh 1500 (Asilimia 650) na mizigo nayo inatozwa kati ya shilingi 200 mpaka 500. Sasa kwa kuwa utekelezaji wa agizo unafanyika kwa ujumla, nikataka viwango vipya kwa ujumla wake visitishwe mpaka kwanza serikali itoe maelezo na vielezo vya msingi wa kufanya ongezeko kubwa la kiwango hicho. Nilitaka serikali itoe maelezo ikizingatia kwamba vivuko ni huduma sio biashara kwa kuwa maeneo mengi yenye vivuko yalipaswa kuwa na madaraja kwa ajili ya vyombo hivyo vya usafiri na wananchi kuweza kupita. Nilieleza wazi kwamba kazi ya msingi ya Wizara ya Ujenzi ni kujenga barabara, madaraja na miundombinu mingine sio kufanya biashara ya vivuko hivyo, ongezeko la kuangalia soko linaweza kushawishi ucheleweshaji wa ujenzi wa madaraja. Ieleweke kwamba kazi kuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) sio kuendesha vivuko na kama tunataka suala hili kuwa ndio kipaumbele tunayo Wizara ya Uchukuzi ambayo inahusika pia na uchukuzi majini na inashirika la meli. Kumekuwepo na kukosekana na uwazi na udhibiti wa kutosha wa mapato na matumizi ya kivuko hivyo tulitaka serikali ieleze kwa mchanguo badala ya kauli za ujumla kuhusu suala hili ili kujenga uhalali wa kupandisha nauli husika kwa hoja ya kupanda kwa gharama za uendeshaji. Nilipinga ongezeko kubwa la bei ya umeme kwa kisingizio hicho hicho, kwa kuwa mchakato ulikuwa shirikishi naamini kutokana na maoni ya wadau yako ambayo yatarekebishwa na TANESCO tofauti na mapendekezo yao ya awali. Haiwezekani suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha kwa wabunge ikawa kujiongezea posho za vikao na suluhisho kwa taasisi za umma kama Wizara ya Ujenzi na TEMESA ikiwa ni kijiongeza mapato kwa kuongeza nauli bila kuzingatia kubana matumizi na kumjali mtanzania wa kipato cha chini ambaye anabeba mzigo mkubwa wa kupanda kwa gharama za maisha na sasa anapindishiwa hata na serikali yake nauli za vyombo vya usafiri kuvuka tu kwenye kivuko. Hivyo, Wizara ya Ujenzi kupitia vyombo vyake inapaswa kuhusisha mapato yanayokusanywa kwenye barabara na ujenzi wa miundombinu na uendeshaji wa vivuko vya muda wakati miundombinu inasubiriwa. Pia, pamoja na nauli, msingi wa uendeshaji wa vivuko unapaswa pia kuwa mapato kutoka kwenye barabara na vyanzo vingine. Badala ya kujibu hoja ya msingi, Waziri Magufuli amejikita katika ongezeko la shilingi 100 mpaka 200 na kulinganisha pia na mazingira yasiyoendana baina ya kivuko cha Kigamboni na vivuko vingine nchini ambavyo vinatofautiana umbali, muda na gharama za uendeshaji.

Unaweza kulipitia tamko zima hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ficha-udhaifu-wa-serikali-na-wizara-yake.html na kama kuna masuala mengine ambayo ungependa niyatolee majibu hapa nitafanya hivyo.

JJ
 

Mchambuzi,

Asante kwa maoni yako ingawa naona umeingia mtego wa Waziri Magufuli wa kuhamisha mjadala wa Kivuko kuwa Mjadala wa Ubungo. Hata hivyo, naomba niweke kumbukumbu sahihi kuhusu suala la Kituo cha Ubungo ili turudi kwenye mjadala wa msingi wa Kivuko. Waziri Magufuli amezusha na kupotosha kwamba sijawahi kuhoji kupandishwa kwa kiingilio katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT) cha 200. Ukweli ni kwamba kama ambavyo napinga ongezeko holela la nauli za vivuko nchini, nilipinga ongezeko la kiingilio katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kwa maslahi ya wananchi wa jimbo letu na ya wasafiri wote nchini wanaotumia kituo hicho. Ukweli zaidi ni kwamba viingilio vya Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo pamoja na ongezeko lake vilipitishwa kwa kutungiwa sheria ndogo (by law) na jiji kabla ya mimi kuchaguliwa kuwa mbunge. Hata hivyo, pamoja na kuwa sikuwa mbunge wakati kiingilio kinawekwa mara baada ya kuwa mbunge niliendelea na harakati nilizozianza kabla ya kuwa mbunge za kupinga ufisadi wa mapato katika kituo hicho. Tarehe 28 Januari 2011 nilifanya ziara ya kituoni hapo kama sehemu ya kutimiza wajibu wa kibunge ambapo pamoja na mambo mengine nilikutana na mawakala wa kituo kusikiliza malalamiko yao ikiwemo kuhusu kiingilio. Kufuatia kupinga huko Tarehe 11 Mei 2011 Kamati ya Fedha na Uongozi ya Jiji la Dar es salaam ilipitisha azimio la kupendekeza kwamba utekelezaji wa sheria ndogo iliyoongeza kiingilio usitishwe. Kwa kuwa sheria ndogo imetungwa na baraza la madiwani, nilikwenda mbele zaidi kupinga kiwango cha kiingilio na ufisadi katika Kituo cha Mabasi Ubungo kwa kuwasilisha hoja binafsi Tarehe 15 Mei 2011. Kutokana na ukubwa wa hoja ya ufisadi katika kituo hicho kwa mujibu wa vyanzo vyetu na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali suala hilo limekuwa likichukua muda kushughulikiwa na nimeendelea kupinga na kuhoji kwenye vikao vya jiji, kupitia vyombo vya habari na hata bungeni Waziri Magufuli akisikia. Kwa sasa tayari jiji limekubaliana na hoja hiyo kinachofuata ni baraza la madiwani kupitisha azimio la kufanya mabadiliko husika. Hivyo, Waziri Magufuli hakusema ukweli alipodai kwamba sijawahi kupinga ongezeko la kiingilio katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo. Jaribio lake dhaifu la kutaka kuonyesha kwamba nimeacha ya kwetu nakwenda kushughulikia ya wengine hatimaye litashindwa ukweli utakapotamalaki. Tuendelee kujadili kuhusu agizo la serikali la kupandisha nauli za vivuko ambalo nimelitolea kauli hapa:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ficha-udhaifu-wa-serikali-na-wizara-yake.html
 
...kivuko nisawa na daraja ...

Kivuko ni sawa na daraja? Huo usawa unatoka wapi wakati kivuko kinatumia mafuta na daraja halitumii mafuta? Hata Mjengwa amefananisha kivuko na daraja la salenda kana kwamba kuna mafuta na wafanyakazi pale darajani wanaoruhusu magari yapite!
 
Kwa mujibu wa Magufuli either apige mbizi au azungukie Kongowe.

mbizi nimesema hawezi kwenye dimbwi ti seuze bahari...atakufa.
kuzunguka kongowe safari ya kwenda na kurudi (kwa mguu) inachukua masaa karibu 8-10....

naomba solution please.
 
Mnyika naye katupeleka chaka... du! wanasiasa mko juuu....


1. Ume-miss big picture; jiulize kwa nini mumetoa vipanya mjini? na sasa ni 26 seater buses tu zinaingia mjini -CBD? na kwa nini mnaleta mabasi makubwa kwenye mradi DARTS? Jibu ni moja tunahitaji vyombo vya kubeba bidhaa in bulk kupunguza gharama, msongamano etc... e.g. GUTA moja linachukua nafasi ya abiria wangapi? mkokoteni mmoja je?

2. Umenena vizuri sana kwamba kazi ya wizara sio kufanya biashara which I fully agree with you; sasa swali TCRA wanafanya biashara, EWURA wanafanya biashara, SUMATRA wanafanya biashara? mbona wanafees kwenye kutoa huduma zao.... rudi ni jibu haraka sana, acha kuchezea wapiga kura wako eeeh.
 

We jamaa wa wapi? au unafikiria kutuimia MASABURI? aliyekuambia kwetu KIMBIJI tunauwezo wakumiliki hilo gari ni nani? uwezo wetu ni baiskeli na guta kama hujuhi.
hona hapa!
 
Kivuko ni sawa na daraja? Huo usawa unatoka wapi wakati kivuko kinatumia mafuta na daraja halitumii mafuta? Hata Mjengwa amefananisha kivuko na daraja la salenda kana kwamba kuna mafuta na wafanyakazi pale darajani wanaoruhusu magari yapite!

Kasome tena, hajamaanisha hivyo, kasema ni sawa na DARAJA kwa maana ya HUDUMA. Mimi nasema ni SAWA na BARABARA. Upoo?
 
Thank YOU... yaaani umeona mbali sana mkuu wangu na ndicho nilichosema mimi.. Watanzania tatizo letu hatutaki kutazama mbele zaidi ya urefu wa mkono unaoingia kinywani kwa sababu hatujui maendeleo ni kitu gani na yanapatikana vipi...
 

Nahisi hulijuhi GUTA, GUTA ni baiskeli ya miguu mitatu kwa ajili ya kubeba MIZIGO na sio ABIRIA.

Ni kama hili hapa chini
i.
 
halafu ndugu mchambuzi, kwa nini ulifanya ceteris peribus ukabakia na nauli ya binadamu tu? Kwenye uzi wako kuna 100, 200 na 300 tu. Kwa kuacha variables nyingine (guta, bajaji, gari n.k.) unadhani hoja yako sahihi?
 
Kibanga Mpinga ukoloni,
Hao ulowaonyesha wote ni usafiri wa sokoni hadi dukani, dukani hadi nyumbani kwa mtu.. na swala la Kivuko cha Kigamboni ni mtu anayetoka huko Kimbiji kuleta mazao yake Kigamboni ndiye anatakiwa kutumia lori la mizigo au itafutwe njia nyingine ya kumsaidia mkulima huyu.

Mh.Mnyika,
Mkuu kaa na wabunge wenzako mzungumzie swala la kufungua SOKO au masoko ya kukusanya vyakula toka kwa wakulima (ilivyokuwa Kariakoo zamani) na hapo ndipo mnada unafanyika kwa wafanya biashara wa masoko ya majimbo au kata (kwa jumla). Kila jimbo au wilaya iwe na soko lake kuu na wafanyabiashara kwa pamoja watatumia usafiri wa malori yanayokwenda majimboni kusambaza biidhaa sokoni au madukani.. Na Hizi Guta zitatumiwa within jimbo au kata yaani mtu ananunua mali zake toka soko la Kigamboni kupeleka dukani kwake au nyumbani.

Jaribuni sana kufikiria kuboresha huduma ya usambazaji chakula maana kusema kweli binafsi huona ni utumwa mamboleo kumwona mtu mwenye Guta anatoka Kimbiji hadi Kigamboni na alnalipwa Tz 5,000..halafu tunalalamikia Pantoni wakati sisi wenyewe malipo yetu ni madogo. Pia ongezeni nguvu kubwa kutaka mishahara ipande kwa wananchi hivyo maana wanashindwa kumudu maisha ..Tatu swala la usafiri lazima liwekewe mkazo sana kwa picha kubwa zaidi ya kivuko hiki maana Tsh 200 sisi tunaiona ndogo lakini kusema kweli tuna tatizo kubwa la usafiri kwa mji wa Dar, ukijumlisha na nauli za usafiri kwa siku mtu hutumia Tsh 1,000 kwa usafiri tu wakati mshahara wake ni chini ya laki..
 
that's my question too. tusaidiane kutafuta jawabu...
Swali lako ni kuhusu 200, kwni kabla ya 200 alikuwaanafanya nini akiwa hana hela?

Sio lazima mje mjini.
 
Je, unaonaje nauli kutoka 100 mpaka 200 ni sawa?
 
Heading yako kwanini isiwe Nauli Feri: Mtemvu, Hata Wewe? au Nauli Feri: Ndungulile, Hata Wewe? au Nauli Feri: Zungu, Hata Wewe? au Nauli Feri: Wabunge, Hata nyie?, ,

Umeona eeh??mchambuzi ana lake jambo hapa bila shaka..alafu hapo anataka watu waweze kutofautisha mijadala ya masuala ya msingi na ushabiki wa kisiasa,,,
 
Umeona eeh??mchambuzi ana lake jambo hapa bila shaka..alafu hapo anataka watu waweze kutofautisha mijadala ya masuala ya msingi na ushabiki wa kisiasa,,,
Hapana sisi ndio tunamsoma vibaya kwa sababu majibu yale tuliyategemea kutoka kwa hao wabunge na sababu zao tunazijua, lakini Mchambuzi kashindwa kuelewa kwa nini Mnyika kajiunga na kundi hili..aidha wakati yeye anamuona Mnyika ni Kichwa zaidi yao au vita ya panzi awaachie wenyewe.. (Politics game).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…