Kwa Askofu Kakobe - Baada ya kufunga ndoa, maharusi wapanda daladala na pikipiki kwenda makwao

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
889
1,515
Ilikuwa siku ya Ijumaa 19.2.2021, ni siku nyingine ya kukumbukwa, katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Dar-Es-Salaam, lililoko Barabara ya Sam Nujoma; pale ambapo jumla ya wahusika 84 waliposhiriki katika kufungwa kwa Ndoa 21, zilizofungwa kwa pamoja katika Ibada ya Ndoa iliyoanza saa 5 asubuhi. Wahusika hao 84, walikuwa ni Mabwana Arusi 21, na Mabibi Arusi 21, ambao hawajawahi kuishi pamoja; na jumla ya Mashahidi 42 (waume 21 na wake zao 21).

Kama ilivyo ada, katika Arusi hizo, viwango vya mavazi ya Mabwana na Mabibi Arusi, vilikuwa ni vilevile ambavyo vimekuwa vikizingatiwa, katika Ndoa mamia kwa mamia, zilizofungwa katika Kanisa la FGBF, kwa miaka zaidi ya 30; hususan tangu Askofu Mkuu Zachary Kakobe alipoliasisi Kanisa hili, tarehe 30.4.1989.

Katika Ibada hiyo ya Ndoa, Askofu Kakobe alihubiri kwanza ujumbe wa Neno la Mungu lisiloghoshiwa, wenye kichwa, "WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII" (WARUMI 12:2); kisha ndipo alipofungisha Ndoa hizo 21 kwa pamoja.

Suala lililowavutia sana wageni, waliohudhuria kwa mara ya kwanza, katika Ibada za Ndoa za Kanisa la FGBF, ni jinsi walivyowashuhudia Maarusi hao, wakitumia usafiri uleule wa kawaida ambao wamekuwa wakiutumia, wanapokwenda Kanisani, katika Ibada nyingine za kawaida. Baada ya kufunga Ndoa zao, Bwana Arusi mmoja mwenye gari lake, alikwenda na mkewe, nyumbani kwake, na gari lake hilohilo, huku akiliendesha mwenyewe.

Baadhi ya Maarusi, walikwenda kwao, kwa kutembea tu kwa miguu, huku wameshikana mikono kwa upendo na furaha isiyoelezeka; na kuwasisimua watu wengi. Siyo hilo tu, Maarusi wengine wengi walitembea kwa miguu, huku wamejaa bashasha, mpaka kwenye kituo cha daladala kilichoko jirani na Kanisa hilo, na kupanda daladala hizo zilizowapeleka majumbani kwao. Taarifa zilizopatikana baadaye, zinaeleza jinsi baadhi yao walivyokuwa wakihubiri Injili ndani ya daladala hizo walizozipanda.


Bwana Arusi mmoja, ambaye hutumia pikipiki (bodaboda) yake kuja Kanisani, alimvisha helmet (kofia ngumu) mkewe, kisha akampakia mkewe (Bibi Arusi), kwenye bodaboda hiyo, na kuondoka naye kwenda nyumbani, huku watu wengi walioshuhudia tukio hilo, wakishangilia kwa nderemo, vifijo na vigelegele !

"Basi atukuzwe Yeye (Mungu) awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina" (WAEFESO 3:20-21). MARANATHA !!!

Tazama picha zao



1613959122848.png
1613959289702.png
1613959378054.png
1613959530369.png
1613960315815.png
1613960458811.png
1613960570090.png
1613960629292.png
1613960675530.png
1613960736877.png
1613960765263.png
1613960796192.png
1613960836015.png
1613960967955.png
1613961002956.png
1613961037576.png
1613961067977.png
1613961133841.png
1613961239306.png
1613961334397.png
1613961367783.png
1613961415108.png
1613961468287.png
1613961516307.png
1613961585372.png
1613961628157.png
1613961665952.png
1613961736399.png
1613961853443.png
 
Kwa hakika kuna funzo hapo kwa vijana wengine.

Mambo ya vikao vya harusi kwa miezi minne kutafuta michango kwa nguvu, kutumbua mamilioni lukuki kwa siku moja tu, na kisha kuanza maisha kukiwa na madeni ni shida.

Hongera Askofu Kakobe!
Hakika pmwasyoke ! Hili funzo kwa jamii na hasa wakristo kuliko dini nyingine duniani.
 
Ni Jambo jema lakini kwa Karne hii mtihani mkubwa ni kumpata mwanamke atakayekubali kufunga ndoa bila sherehe kubwa. Wengi wanataka sherehe ya kifahari, msafara wa magari na miosho mingi ili mji mzima wajue kuwa ameolewa. Ukigusia swala la ndoa bila sherehe wanakukimbia
 
Back
Top Bottom