Natatizika mwenzenu. . .

Natatizika mwenzenu. . .

He he he he, hajali size aisee
Tena yeye anaona poa tu, si unajua tena wasukuma kwa Big size?

teh teh. Basi siku hzi una relax sana. Umekuwa Mrs Boss Zombie. No more stress kama zamani, full ac, site inasimamiwa na zombie mwenyewe,. Zombie hoyeeeeeeeeeeeeee
 
Asante, angalau kuna wengine kumbe wanajali uzito.

Nilidhani ni mie tu, ngoja nijaribu kupata wengine kama nitaweza.

Niliwahi kuwa na tatizo kama la kwako, kuwa nikianza mazoezi sidumu hata wiki, ila baadae nilikuja kupata suluhisho. Tulikubaliana marafiki watano kuanzisha "fat club" ya kufanya mazoezi kila jioni, siku 5 kwa wiki. Mtu usipofika unalipa faini ya sh elfu 5 kwa siku. Ukichelewa sh elfu 2. Kila nilipokuwa nawaza sh elfu 5 zangu uvivu uliniishia hadi baadae nikajikuta nimekuwa committed. Tulianza watu watano, but baadae wakaongezeka hadi tukafika 11. Ndani ya miezi 6 nilifanikiwa kupunguza kilo 12. Ela tulizokuwa tunakusanya tulizitumia kununua vifaa vya mazoezi vidogo vidogo kama kamba za kuruka nk. Kuna jamaa alipunguza kilo 20 kwa hiyo miezi 6...
Kwahiyo ninachoweza kukushauri kama una rafiki mmoja au wawili wenye nia kama hiyo anzisheni kikundi na mujiwekee sheria kabisa... Kufanya mazoezi mwenyewe inatia uvivu...
 
Hivi unajua wengine tukiwa na stress ndio tunakula sana?
Inaweza kuwa vice verse pia, yaani mie nahisi namzidi ng'ombe uzito.

una ngapi kwani?
manake si ajabu ukawa unalia lia hapa kumbe ulikuwa na 65 sa hz una 68
and hiyo miezi kumi nyuma kwa kumbukumbu zangu ndio zombie alitolewa kwenye uzombie sio!?
THE IDEA TU YA KUWA U'R IN LOVE INAKUFANYA URELAX!
its okeeeey!utapungua tu with time!
 
Ni wenge zangu tu, kuna size fulani nikifikia amani yote inatoweka
Sipendi nikiwa hivi, hata nikiwa na mtoko ziwezi vaa kata mikono, mkufu haukai shingoni?!

ahahhha sasa usipokuwa na mikono minene unavaaje kata mikono
mkufu usipokaa shngoni manake shingo yenyewe ndo mkufu!
we vipi!?
 
Hivi unajua wengine tukiwa na stress ndio tunakula sana?
Inaweza kuwa vice verse pia, yaani mie nahisi namzidi ng'ombe uzito.

MI MWENYWE HIVO HIVO
hapa nshapiga thupu,na tikiti maji.kuna juice inanisubiri muda si mrefu
 
Addiction mbaya jamani, roho I radhi lakini mwili dhaifu.

Msianze kuninanga, nahitaji kupewa moyo kuwa naweza kufanya na kufanikiwa. Natamani kuona ushuhuda kutoka kwa wenye tatizo kama langu na wanakabilianaje nalo.

Ni uzito wa mwili, umeanza kuninyima raha kabisa, nahisi nitakuwa depressed mwishowe. Nikifanya mazoezi wiki moja tu najikuta ratiba vululu vululu. Nikijaribu dayati ndio kabisaaa. Too much addicted to kyukyu, chapati, wali, soda and ice cream. Sijui mateja wa unga inawawia ngumu kiasi gani.

Natatizika, sina raha kabisa, msaada tafadhali.
Mazoezi peke yake kama yameshindwa kutatua tatizo lako , jaribu kutumia alternatives zingine. Moja ya alternatives hizo ni Slimming orange juice katika labels mbalimbali za biashara, kwa mfano Curvey slimming juice amabayo imetengenezwa kwa kutumia matunda ya asili n amboga mboga. Kuna ya coffee na ya orange. Ya Orange ina orange juice, water soluble pearl powder, dietary fibre, fluctoligose na vitamins. inanywewa ikiwa moto au baridi, mara moja kwa siku. Matokeo yake ni ndani ya siku 14. Hairuhusiwi kwa waja wazito, wanaonyonyesha na watoto. BE HAPPY.
 
muhanga mwenzio ni mimi
ila namshukuru mungu ninaendelea vizuri
kwanza nafanya mazoezi sana...nina miezi kadhaa sijawai kuweka soda mdomoni mwangu wala maicecream hayo...ila sijapungua sana cause nimegundua lately nalala sana ...yaani mi saa mbili nipo bed hadi saa moja kesho yake
kwa sasa nimeacha siku mbili hizi najikeep busy hadi saa tano
ila na raha za dunia nazo zimezidi my dear...mwili nao unashangilia
ila all in all nilishagundua ukitaka kupungua kuwa na mpenzi....khaa full stress....utakondaje
 
Asante, angalau kuna wengine kumbe wanajali uzito.

Nilidhani ni mie tu, ngoja nijaribu kupata wengine kama nitaweza.
Kiukweli watu wa kijijini ndio wanapenda kuwa wanene... Ukiona wa mjinj karizika nao ujue tu kakata tamaa...
 
Ukinenepa kama konnie ntakuadhbu walahi.. Unataka kile kikampuni uchwara cha ndege kgome kukupa tiket kwa sababu ya uzito mkubwa?

ahhaahhahahahhahahhahahahhah na hiv kinaniudhi udhi kwa kuniharibia ratiba zangu kikigoma ndo poa utapata hasira ya kuninulia jet yangu!
 
Imagine umeenda kwenye presentation kwenye majukwaa ya watu
Badala ya kukonsentret na jinsi gani utadeliver mada yako watu wakuelewe
Wee unawaza, sijui hii nguo imekaa vizuri, sijui naonekana mkubwa kama kiboko, full distraction.

Ila ukizubaa unakata tamaa, na mie ndio kuwa sikubali kuliacha tatizo hadi linikatishe tamaa.

Kiukweli watu wa kijijini ndio wanapenda kuwa wanene... Ukiona wa mjinj karizika nao ujue tu kakata tamaa...
 
ahahahahahha wat if zombie alimpata kwa kuongezeka uzito!
unajua mnakariri sana nyie!
shauri yenu!

Snowhite nakupa homework. Ukiweza nakununulia juice ya ukwaju.

Nieleze haya maneno hapo chini aliyasema nani na kwenye jukwaa gani:


"Falling in love at this age? God forbid"
 
Addiction mbaya jamani, roho I radhi lakini mwili dhaifu.

Msianze kuninanga, nahitaji kupewa moyo kuwa naweza kufanya na kufanikiwa. Natamani kuona ushuhuda kutoka kwa wenye tatizo kama langu na wanakabilianaje nalo.

Ni uzito wa mwili, umeanza kuninyima raha kabisa, nahisi nitakuwa depressed mwishowe. Nikifanya mazoezi wiki moja tu najikuta ratiba vululu vululu. Nikijaribu dayati ndio kabisaaa. Too much addicted to kyukyu, chapati, wali, soda and ice cream. Sijui mateja wa unga inawawia ngumu kiasi gani.

Natatizika, sina raha kabisa, msaada tafadhali.
Mimi naweza kukushauri labda njia moja mbili ambazo naona unaweza kutumia kuforge
a) Wanasema usinywe maji nusu saa kabla ama nusu saa baada ya mlo. Maji yanadilute enzymes zinazomeng'enya chakula na kusababisha useful sehemu ya chakula ulichokula kupungua.
So wewe ukigonga vyuku, wash them down with a lot of water ili kudisobey rules.


b) Vinywaji baridi: hivi hupunguza joto tumboni, enzymes huhitaji joto kidogo ili zafanye kazi vizuri.
Temperature elevates the rate of chemical reaction (Fiziks/Kemistry).
So wewe ukiongeza na cold drink useful food inapungua.


SIJUI mambo hayo vizuri ila I'm sure kuna backfire(Labda mbinu halali zikishindikana na ndo vile tena kuwa lazima kieleweke ndo utumie)
 
Mimi pia nina tatizo hili lakini nimepanga kuanza mazoezi kesho

Nimejitahidi kupunguza kula lakini wapi

Karibu tuwe pamoja

Kesho tu naanza!!!!!!!!!!!!
 
Basi tupeane mikakati ya kupungua hata 2 kg kwa mwezi, mie nshaanza.
Nimeamua kuondoa starch na mafuta kwenye menyu yangu, ni mboga mboga na matumba tu.

Daym, kuku ni zaidi ya kokein kwangu lol, but najitahidi.

Mimi pia nina tatizo hili lakini nimepanga kuanza mazoezi kesho

Nimejitahidi kupunguza kula lakini wapi

Karibu tuwe pamoja

Kesho tu naanza!!!!!!!!!!!!
 
Nimetumia hizi tatu za kwanza, and it's working

Japo siku tatu mwanzo ilikuwa ngumu sana, tena sana, kidogo nikate tamaa.

Sasa hivi nikigusa mifupa ya soap dish(clavicle) naihisi, nasubiri kwa hamu itokeze kwa nje.

Hii haijawahi kukosea. Nna uhakika kabisa

1. Panga mida maalum ya chakula kwa asubuhi, mchana na jioni (hakikisha mlo wa jioni haupangwi zaidi ya saa mbili usiku)

2. Usile chochote nje ya mida maalum ya chakula (unaweza kunywa maji, ila snacks za aina yoyote haziruhusiwi)

3. Milo yote mitatu hakika ina fungu la mbogamboga na matunda

4. Tembea (haraka) kwa walau dakika 30 kwa siku. (hata kwenda window shopping poa)

Ukifanya hivyo hutakaa unenepe 🙂
 
Tukikosa magauni ya china inabidi Boflo ajipinde na magauni ya marekani. Hivi unajua plus size shops moe na wewe hatupati size manake nguo ni kubwa sana?

Afu za marekani zikitushinda tunava madera.
Kongosho ushapungua kg ngapi? Ama ushamzoea zombie?
ngoja siku mi na King'asti tutakapokosa size ya magauni yale anayotununulia Boflo ndo nitaanza kuwa na low self esteem !
UNTIL FURTHER NOTICE
CC Madame B
 
Last edited by a moderator:
On a serious note: jiondoe kabisa kwenye menu za deep fried foods. Kama ni samaki weka kwenye oven ama mkaa ndo uunge. Kama ni kuku na nyama ziwe mchemsho ama za kuchoma. Ule dinner mapema walau saa moja. Ila sasa binge ndo sumu kabisaa. Pipi, soda, juice za viwandani, biskuti, chocolate havikuhusu...kama udokozi dokoa karanga na korosho na matunda.

Ukibadilisha lifestyle utafanikiwa zaidi kwa mida mrefu. Tatizo la diet unajikuta unahesabu siku ili urudie tabia zako mbovu.
Basi tupeane mikakati ya kupungua hata 2 kg kwa mwezi, mie nshaanza.
Nimeamua kuondoa starch na mafuta kwenye menyu yangu, ni mboga mboga na matumba tu.

Daym, kuku ni zaidi ya kokein kwangu lol, but najitahidi.
 
Achana na soda

Achana ana ice scream

Punguza sana sukari

Punguza sana vyakula vya wanga

Achana na chips mayai na jamii yote ya chips

Kula sana mboga za majani na samaki

Achana na mavyakula ya kukaanga au nazi shata shata

Chukuchuku ndo iwe chakula chako

Kama unashindwa kwenda gym nunua hata kama uwe unaruka asbh na jioni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom