Espy_
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 91,951
- 183,439
Yawezekana misingi yao haikuwa bora ila ilifanya kazi vizuri kwa wakati wao.Hapana tujitahidi kuchukua mazuri yao na mazuri ya haya yalokuja tuchanganye we can get something good.
Japo misingi yao ya kimalezi ilikuwa bora kuliko yetu ya sasa.
Shida inakuja tunataka kwenda na wakati kwa mawazo ya kizamani bila kuyaboresha. Hilo haliwezekani, mwanaume wa sasa anataka mke kama bibi yake ilihali yeye sio babu yake na kinyume chake. Sawa bibi alimfanyia babu 1 2 3 4 5....., kwasababu alikuwa mama wa nyumbani, lakini je, mkeo ambae ni mfanya kazi mnaeondoka wote na kurudi wote anaweza kukufanyia the same?!!!!
Je mumeo ambae ana kipato kidogo kuliko wewe kwakuwa mfumo umekuruhusu kuwa nacho zaidi na amebaki kuwa mumeo mwaminifu unamuheshimu inavyopaswa!!!! Nk nk nk nk, msingi ni upendo na heshima tu. Hayo mengine mbwembwe tu za kunogesha.