#COVID19 Natamani kufungua kesi dhidi ya WHO. Kwanini ugonjwa mmoja una chanjo zaidi ya 24?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Tunaposema tuwe makini siyo kwamba ni ujinga. WHO imeruhusu chanjo zaidi ya 24 kwa ugonjwa mmoja tu.Hii maana yake chanjo bado ziko kwenye utafiti na zimetolewa kwa hati ya dharula (soma masharti). Na kama zimeshakuwa fully approved maana yake ni kuwa zinazidiana ubora au uwezo ni sawa na dawa tunazotumia kujitibu magonjwa ya kawaida kulingana na uelewa wa mtoa huduma na hali ya ugonjwa, anaweza kukuandikia dawa tofauti tofauti.

Kuna tofauti kubwa kati ya dawa na chanjo. Kwanza dawa ina half life na kazi yake ni kupambana na ugonjwa kisha end products ya dawa inatolewa mwilini kwa njia ya mkojo.asilimia kubwa ya dawa inakaa mwilini si zaidi ya masaa 24.

Chanjo kazi yake ni kuuambia mwili utengeneze kinga (antibodies) ambayo itakaa mwiki kwa miezi au miaka mingi sana ikipambana na ujio wa ugonjwa maalum. Ndiyo maana chanjo inapatikana baada ya miaka mingi kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa kwa miaka mingi ya badae.kwa mfano unaweza kukuta madhara kwa kinamama mimba kuharibika, kuzaa watoto wenye ulemavu, watoto kufia matumboni, etc.

Watalaam wanaelewa kuwa kuna kitu kinaitwa drug interaction ambapo unakuta dawa mbili zikikutana mwilini zinafanya kazi kwa pamoja au kwa kushindana na kuleta madhara makubwa mwilini. Nimeona humu JamiiForums kuwa wenzetu kule Zanzibar wameambiwa kuwa chanjo waliyochanja haitambuliki huko wanakokwenda kuhiji. Hivyo kama wanataka kwenda Makka wachanje chanjo nyengine. Nawashauri wasifanye hivyo labda kama watakuwa wamejiridhisha kuwa hakuna drug interaction. Lakini watajuaje?

Swali kwa WHO, ni kuwa kwanini wameruhusu matumizi ya chanjo zaidi ya 24 kwa ugonjwa mmoja bila kutoa maelezo zaidi namna ya utumiaji wa chanjo hizo? Kwa sababu kila nchi imeamua yenyewe kutumia chanjo inayoona inafaa, lakini wananchi wake kwa uelewa mdogo wanaweza kujipatia chanjo zaidi ya aina moja na kuleta madhara makubwa kwa afya zao

Swali la pili, wanitajie ugonjwa gani ambao watu wametumia chanjo zaidi ya aina moja kujikinga na ugonjwa huo?

Tatu, WHO inafahamu kuwa chanjo za Covid-19 zimetolewa kwa hati ya dharura, ni kwa nini wameachia wanasiasa kuzungumzia chanjo ya Covid-19 wakati siyo watalaam. Chukulia mfano yule mbunge wa kigoma ambaye nimemuona akimshupalia Askofu Gwajima kuwa ati amefanya kitu cha kutaka kuipindua serikali wakati hana uelewa wa chanjo?

WHO Ina wawakilishi humu nchini. Naomba mnijibu otherwise najiandaa kuwapeleka Mahakama ya kimataifa yamakosa ya jinai
 
Chanjo zote unazotaja ni za COVID 19. Unaposema ugonjwa mmoja unatumia chanjo 24 maana yake nini?

Kwamba chanjo kwa ajili ya homa ya Ini inatumika kwenye COVID 19? Kwamba chanjo ya surua inatumika kwenye COVID 19?

Utofauti wa makampuni, utofauti wa majina ya chanjo za COVID 19 na wingi wa Nchi zinazozalisha chanjo ya COVID 19 hakuifanyi kuwa chanjo aina 24.

Zote hizo formula yake inashabihiana..na inapitishwa kutumika baada ya Wataalamu wa WHO kujiridhisha usalama wake.

Hujiulizi kwa nini dawa jamii ya pain killer zipo za aina nyingi kwa ugonjwa mmoja?

Ukizichunguza karibu zote zinafanana.
 
Chanjo zote unazotaja ni za COVID 19. Unaposema ugonjwa mmoja unatumia chanjo 24 maana yake nini? Kwamba chanjo kwa ajili ya homa ya Ini inatumika kwenye COVID 19? Kwamba chanjo ya surua inatumika kwenye COVID 19?...
Ni kama tu panadol
,Paracetamol,hedex, action,dawa tatu n.k zote unaweza tumia kwa maumivu ya kichwa..isipokuwa hawa watu vichwa vigumu hawaelewi wanapoambiwa chanjo ni hiari sio lazima..
 
Soma kwenye dashboard ya WHO ,covid vaccine then urudi hapa unipe jibu
 
Ni kama tu panadol
,Paracetamol,hedex, action,dawa tatu n.k zote unaweza tumia kwa maumivu ya kichwa..isipokuwa hawa watu vichwa vigumu hawaelewi wanapoambiwa chanjo ni hiari sio lazima..
Si dhani kama wewe ni mtalaam au kama unaelewa tofauti ya Dawa na chanjo.kwa kukisaidia some : the difference between drug and vaccine.
 
wazee hiii chanjo tumepigwa. New World Order lazima itimizwe na hao mashetani wa hiii program wanafanyakaz kwa kasi coz wako nyuma ya mda wanapush kwa kasi sana kukimbizana na mda.
 
Tunaposema tuwe makini siyo kwamba ni ujinga. WHO imeruhusu chanjo zaidi ya 24 kwa ugonjwa mmoja tu.Hii maana yake chanjo bado ziko kwenye utafiti na zimetolewa kwa hati ya dharula (soma masharti)...
Ukiwa hujui…. Ni hujui tu
 
Si dhani kama wewe ni mtaalam au kama unaelewa tofauti ya Dawa na chanjo.kwa kukisaidia some : the difference between drug and vaccine.
Ni kweli sina utaalam wowote lkn siwezi kukosa mawazo kwasababu naishi ktk ulimwengu wa COVID19 kwa sasa,kama ilivyo kwa Gwajima anapinga chanjo kuwa sio salama na hana utaalam wowote juu ya utengenezaji wa chanjo

I'm sure chanjo zote zina same content,ila tu zinatengenezwa na kampuni tofauti kama ilivyo kwa madawa...

Sijafanya research lkn siamini kwamba hizi chanjo za magonjwa mengine ambazo tayari zipo na hata hatuoni watu kuzijadili usalama wake kwamba zote zinatengenezwa na kampuni moja tu Dunia nzima

Ikumbukwe COVID19 haina hata miaka 3 kwenye hii Dunia,wataalam kila pembe wanapambana.Hauhitaji mtu kukwambia kuwa baada ya miaka kadhaa mbele zitabaki chanjo chache sana zenye kuaminika na chanjo zingine zitapotea kabisa.Hauhitaji mtu kukwambia kuwa kwakuwa hawa wote wanaojaribu kutengeneza chanjo WHO wanawatambua,na wao wanatumia nafasi hiyo ya kutambuliwa na WHO kupiga pesa kupitia chanjo...kwahiyo mambo mengi hapa yatatokea na kawaida ili hali ya aina hii kuja kutulia itachukua miaka kadhaa.

Naamini pia hata utafutaji wa chanjo za magonjwa mengine miaka ya nyuma Dunia ilipitia kashikashi kama hizi za machanjo mengi kwa ajili ya ugonjwa mmoja,ila baadae Dunia ika stick na chanjo chache.
 
Hii ni biashara kama biashara zingine, ndio maana hata magari yapo ya aina mbalimbali, kila mzalishaji anakaribu kuliteka soko.
 
Ni kweli sina utaalam wowote lkn siwezi kukosa mawazo kwasababu naishi ktk ulimwengu wa COVID19 kwa sasa,kama ilivyo kwa Gwajima anapinga chanjo kuwa sio salama na hana utaalam wowote juu ya utengenezaji wa chanjo

I'm sure chanjo zote zina same content,ila tu zinatengenezwa na kampuni tofauti kama ilivyo kwa madawa...

Sijafanya research lkn siamini kwamba hizi chanjo za magonjwa mengine ambazo tayari zipo na hata hatuoni watu kuzijadili usalama wake kwamba zote zinatengenezwa na kampuni moja tu Dunia nzima

Ikumbukwe COVID19 haina hata miaka 3 kwenye hii Dunia,wataalam kila pembe wanapambana.Hauhitaji mtu kukwambia kuwa baada ya miaka kadhaa mbele zitabaki chanjo chache sana zenye kuaminika na chanjo zingine zitapotea kabisa.Hauhitaji mtu kukwambia kuwa kwakuwa hawa wote wanaojaribu kutengeneza chanjo WHO wanawatambua,na wao wanatumia nafasi hiyo ya kutambuliwa na WHO kupiga pesa kupitia chanjo...kwahiyo mambo mengi hapa yatatokea na kawaida ili hali ya aina hii kuja kutulia itachukua miaka kadhaa.

Naamini pia hata utafutaji wa chanjo za magonjwa mengine miaka ya nyuma Dunia ilipitia kashikashi kama hizi za machanjo mengi kwa ajili ya ugonjwa mmoja,ila baadae Dunia ika stick na chanjo chache.
Umejaribu kujibu.asante sana.lakini cha kukuongezea hizi chanjo za covid hazina same contents.so mechanism of action ziko tofauti
 
WHO Ina wawakilishi humu nchini. Naomba mnijibu otherwise najiandaa kuwapeleka Mahakama ya kimataifa yamakosa ya jinai
WHO ni shirika la Umoja wa Mataifa, ambalo hata watumishi wake sio rahisi kushitakiwa kwa sababu wanakuwa na kinga ya kidiplomasia. Sasa kama unafikiri unaweza kuushitaki Umoja wa Mataifa endelea.

Kuna siku utataka kumshitaki balozi wa USA nchini.
 
Sikiliza hapa then chagua kuchanja au hapana

Bonyeza tu:
VACCINATIONS AS A ...
6 days ago — House Bill 4471 PROHIBITS VACCINATIONS AS A CONDITION OF EMPLOYMENT

Quote
 
Back
Top Bottom