Natamani hata kunywa sumu, mapenzi jamani...

Natamani hata kunywa sumu, mapenzi jamani...

mijanaume ya siku hz ndivyo ilivyo,uvumilivu na uaminifu ni zero kbs.
Achana nae huyo mshamba anaeshobokea mapenzi,tena fanya haraka kuhama hapo.
 
mimi ni msichana wa miaka 26, naishi arusha nilikua na mchuchumba wangu ambae tumedum nae kwa miaka 2 na kupanga mambo mengi ya kuoana wote tumepanga nyumba moja japo kila mmoja anakaa chumbani kwake dec nilisafiri kwenda likizo nyumbani mwanza nimerudi jan 10 nimekuta kaanzisha mahusiano na dada jirani tena tumepanga nae nyumba moja nifanyeje wana JF yaani wanapika na kupakua yule dada ananiwekee nyimbo za mafumbo. taarabu, mpaka nakosa ham ya kuishi nilipomtaka nimuulize mchumba wangu imekuaje maana hatukukosana kabisa hataki kupokea cm yangu ananisalimia tu basi nampenda sana jamani naumia nashindwa niongee na nani anisaidie mimi niende wp jaman haaa kwel dunia haina huruma


Pole dada,wanaume wengi ndivyo walivyo ila sio wote,saizi usimpende mwanaume ukawekeza na moyo wako wote kwake, madhra yake huwa hayo. Cha msingi hama nyumba,futa namba yake kama unavizawadi vyake choma moto yan kumbukumbu zake zote poteza halafu anza maisha upya, utampata tu wako. na mawazo ya kujiua ni ujinga,ujiue kwa sababu ya mwanaume?:israel:
 
Naumia sana kuona wasichana wanaumizwa hivyo kimapenzi,hebu ni-PM ili niokoe jahazi niwe mbadala wa huyo jamaa
 
Ngoja kwanza...huyo ni mchumba au Bf???
Anyway..akunyimae mbaazi kakupunguzia mashuzi...life has to go on
 
Jack1 achana na huyo na wewe mletee mwanaume mwingine hapohapo awe anakubeba kukupeleka uwani ndiyo jamaa litalia kilio kibaya maana hajawahi kukubeba kwenda kukuogesha
 
Pole dada ila nakushauri achana na maamuzi unayotaka kuchukua ,usitake kuondoka kwa sababu ya mtu mwingine hata hivyo mbona wanaume single tuko wengi achana nae huyo asikuumize kichwa.
 
Pole sana, najiskia kukuhurumia, huyo mwanamke ni shetani, na huyo mwanamme akili zake sio timamu. Fikiria mtu mwenye akili timamu anaweza kumfanyia binadam wengine kama hivo?

Hapo ndio mungu kakupenda kakuonesha kabla hamjafanya makubwa.

1. Pengine huyo mchumba wako kadanganywa una mpenzi mwingine mwanza,
2. Au huyo mchumba wako akili yake kama kuku kila jike alie karibu nae ni chakula yake.

how old is he?


Au wewe mwenyewe unamuonaje binadam kama huyo? atakufaa?
Hapo kama si kifo cha sumu, kifo cha mawazo, na kama si cha mawazo basi hata HIV.

Dont forgive him
 
Leo nimekumbuka dada nzuri wa kinyamwezi alikunjwa sumu akiwa mjamzito.
Kisa alimpenda sana jamaa mmoja, ningependa kumuita "shenzi"
Jamaa alimuambia akibeba mimba tu atakuoa. Mwanamke akabeba, alipokuwa na mimba ya miezi 7, bwana akaenda kwao akarudi na mke wa kabila lao.

Mwanamke akanywa sumu. Wanaume walio mpenda kweli pale mtaani walipiga kilio.

Ujiue kwa mtu asie kupenda, anae taka kukuaribia maisha yako. poleni akina dada na mama.
 
hama hiyo nyumba kapange pengine! halafu usimfuatilie tena, achana nae! mshukuru Mungu kwa kila jambo ipo siku utashuhudia gharama za usaliti uliofanyiwa. kwa usahuri zaid ni-pm!
 
Pole sana, lakini usifikiri kunywa sumu kwaajili ya mtu! Piga moyo konde na usonge mbele tanzania ina watu wengi sana ambao wanaweza kukupenda kwa dhati!
 
mimi ni msichana wa miaka 26, naishi arusha nilikua na mchuchumba wangu ambae tumedum nae kwa miaka 2 na kupanga mambo mengi ya kuoana wote tumepanga nyumba moja japo kila mmoja anakaa chumbani kwake dec nilisafiri kwenda likizo nyumbani mwanza nimerudi jan 10 nimekuta kaanzisha mahusiano na dada jirani tena tumepanga nae nyumba moja nifanyeje wana jf yaani wanapika na kupakua yule dada ananiwekee nyimbo za mafumbo. Taarabu, mpaka nakosa ham ya kuishi nilipomtaka nimuulize mchumba wangu imekuaje maana hatukukosana kabisa hataki kupokea cm yangu ananisalimia tu basi nampenda sana jamani naumia nashindwa niongee na nani anisaidie mimi niende wp jaman haaa kwel dunia haina huruma

wahi kwa babu fasta, teh teh umezidiwa kete, wakipanga wewe pangua. Lakini akili za kuambiwa changanya na zako eeeeehhhhhh
 
hama hiyo nyumba kapange pengine! halafu usimfuatilie tena, achana nae! mshukuru Mungu kwa kila jambo ipo siku utashuhudia gharama za usaliti uliofanyiwa. kwa usahuri zaid ni-pm!

Sasa si um PM tu, hadi yeye aku PM ndipo umshauri?kamanda bwana
 
Imenikumbusha nyimbo moja ya zamani(jina sikumbuki)kama mapenzi yaua!,kufa sioni buhari oooh!
 
Nenda unapoabudu ukatoe sadaka kwa muumba wako kwani kakuonesha SIDE b ya huyo kaka.Jiulize ungekuwa tayari kwenye ndoa ndo yakakukuta,ingekuwaje?
 
Pole sana dada, jaribu kusahau, ka mbal nao pia jiweke bize na mambo yako assume hukuwah kukutana na m2 huyo
 
duuh!pole sana ila mshukuru mungu umeona mapema,jipe moyo songa mbele na huyo anekuwekea mafumbo fanya kama vile husikii,move on with your life coz hujazaliwa na huyo jamaa,mapenzi ndivyo yalivyo,mungu akutie ujasiri usitamani kufa utampata uliepangiwa na mungu,huyo hakua wa kwako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom