Natamani hata kunywa sumu, mapenzi jamani...

Natamani hata kunywa sumu, mapenzi jamani...

Pole sana,everything happens for a reason!!muombe mungu akupe ujasili na uvumilivu
 
pole dada yangu! Arusha unaishi sehemu gani? mie nipo mitaa ya nane nane!
 
asee hama hiyo nyumba otherwise utakufa kwa presha kabla ya kunywa sumu,pole! next time penda kwa akili!:target:
 
shukuru mungu kakufungulia mapema katimiza malengo yenu chukulia hivyo kama mngekuwa mmefunga ndoa ingekuaje hajakupunguzi kiungo chochote we anza tena tafuta chumba kingine na kama kuna mtu alikua anakusumbua sumbua mtafute mueleze yaliojili ikiwezekana muanze maisha yenu mapya huyo bwana alikuwa anakula huku na huku wakikorofishana atakuja omba msamaha na akina mama kwa kusamehe hamjambo mtarudiana tena fikiria ya maisha ya mbele siku hizi ndoa ni uasanii mtupu kaza buti.halafu nyiwe ni watu wazima bila shaka na kazi zenu kwanini mpange vyumba tofauti siku hizi ndoa zinaanza kwa majalibio ,majalibioyakijibu utasikia maandalizi ya harusi
 
Tutatoana Roho Yarabiii! Kwa hivi Vibuzi!!!!

Acha Usengery ukifa sasa si ndo unwaachia uhuru wa Kujinafasi?????? Embu hama hiyo nyumba mara moja na ujifunze Kupenda KIDIGITALI

"A wise girl kisses but doesn't love, listens but doesnt believe, and leaves before she is leftby Marlyin Monroe


wewe lara 1 huyo Marlyin Monroe aliishia kujiua tu kwa kujioverdose baada ya kuwa na low self-esteem mkuu!

sometime haya mambo hayana ufundi ,,,,, i have seen strong people with strong character wakikneel ,cry ,tryng to attempt suicide n.k kisa haya haya mapenzi.
 
Last edited by a moderator:
Kunywa tu mwanangu, labda huko utakakoenda utapata mapenzi unayoyataka
 
Ni vizuri kujua kila kitu kina mwisho na huo ndio mwisho wa hiyo relationship ingawa hukutarajia ila ndio ukweli. Hiyo ni changamoto katika maisha hivyo pambana nayo uishinde kama unavyozishinda nyingine ila kwa kuanzia nakushauri uhame ili ukae nao mbali ili usahau yaliyotokea.
 
shukuru muumba wako kwa kukuonyesha mapema kuwa mwanaume huyo hakufai kama mume!!! hama katika nyumba kapange kwingine!! nafurahi lara 1 amekuambia penda kidigitali!!! ina maana kuwa una uhuru wa kuchagua kind of a bundle unataka at a particular time na ukiona halifai unahamia lingine!!! Mem/women are like buses, you missed one, you catch the next one!!! Ujiue kwa ajili ya mtu, why? Angekuwa anakupenda asingechukua mwanamke mwingine in just too short a time'!!! kwake anakupenda ukiwa machoni pake tu!! huyo si mume bali ni m--a---l---a--y---a.
 
jack 1 achana na mawazo ya Kunywa Sumu...Muombe Mungu akujaalie uhame hapo haraka uendelee na maisha yako, utampata anayekupenda kiukweli. Miaka 2 sio mingi ya kuguarantee kuwa hamtaachana. watu wanaachana wamekaa kwenye ndoa miaka zaidi ya 20, itakuwa wewe kwenye uchumba?
 
mimi ni msichana wa miaka 26, naishi arusha nilikua na mchuchumba wangu ambae tumedum nae kwa miaka 2 na kupanga mambo mengi ya kuoana wote tumepanga nyumba moja japo kila mmoja anakaa chumbani kwake dec nilisafiri kwenda likizo nyumbani mwanza nimerudi jan 10 nimekuta kaanzisha mahusiano na dada jirani tena tumepanga nae nyumba moja nifanyeje wana JF yaani wanapika na kupakua yule dada ananiwekee nyimbo za mafumbo. taarabu, mpaka nakosa ham ya kuishi nilipomtaka nimuulize mchumba wangu imekuaje maana hatukukosana kabisa hataki kupokea cm yangu ananisalimia tu basi nampenda sana jamani naumia nashindwa niongee na nani anisaidie mimi niende wp jaman haaa kwel dunia haina huruma

Ukionwa umetendwa . . . . . .We achana na huyo,hama huko rudi Mwanza maisha yatasonga tu . . . . . . . . .Ukiona umeboreka sana nitafute . . .Lol!
 
pole sana wanaume wa siku hizi pasua kichwa kweli

Maji unayoweza kujua ladha ni yale uliyofanikiwa kuyanywa . . . . . . . . . . Apart from that,u know nothing!
 
Ujiue kwa sababu ya dushelele? Hapana, maisha ni lazima yaendelee.
Tulia tu, utampata mwenye mapenzi ya kweli!
 
Last edited by a moderator:
Sikiliza Jack 1, dawa ya moto ni moto, hakuna kuhama hapo, kaza moyo, jipe moyo, wakiwa wanafanya mambo yao usiwajali, kama huna cha kufanya tafuta ili uwe busy, kikubwa na wewe tafuta mwanaume wa kukuliwaza, na pia nenda naye hapo hapo kwa chumba chako naye amuone, lakini hakikisha unachagua mwanaume mzuri kuliko yeye. Nakwambia nyodo zao zooooote zitakwisha na watakaa kimyaaaaaaaaaaaaaaa! KIKUBWA HATA WAKIKUSALIMU USIWAITIKE WEWE KAAA KIMYAAAAAAA FANYA MAMBO YAKO WATAOGOPA NA KUJIULIZA MASWALI MENGI NA HATIMAE WATAHAMA WAO KWA HOFU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom