natamani bunge la tz.....lingeendeshwa kingereza

PapoKwaPapo

JF-Expert Member
Jun 5, 2008
380
45
nimeona jinsi wabunge walivyokuwa wanapata shida kujieleza walipokuwa wanagomembea uwakilishi wa SADEC nimecheka kupita kiasi kwa watu walikuwa wanatumia nguvu kupita kiasi ili waweze jielezea..........
Walishindwa kabisa kusema nini watakachokifanyia tz huko sadec zaidi watu wanataja tuu vyeti vyao feki.....embu jaribu kuicheki kwenye youtube hii hapa, Wagombea wa uwakilishi SADC
 
IKO wapi hiyo clip ya you tube
 
OOOOOOOOOOps! Naamini ikiwekwa lazima wazungumze kiingereza zaidi ya nusu watakimbilia hospitali kuomba O.Ds, au kila siku watasingizia kufiliwa.
 
Kuongea kiingereza si ujanja, kikubwa ni IQ yako inavyofanya kazi, kama mtu hawezi kuongea kiingereza anaongea kiswahili translator atafanyakazi ya kutafasiri. kuna watu bongo wanaongea kiingereza kizuri lakini kichwani hamna kitu. Binafsi naona wanaosisitiza kiingereza wanakasumba ya kikoloni. unatakiwa kujua kiasi na kujiamini, so hata hao uliowaona wanatumia nguvu kujieleza kwangu natafsiri kuwa walikuwa hawajiamini tu-"lack of confidence" tu
 
Sijui ni ushamba , sijui ni ulimbukeni , sijui ndiyo ukoloni bado upo mpaka vichwani kwetu!. Mimi nashangaa sana mtu anapofikiri kujua kiingereza sijui ndiyo elimu ? . Hii kasumba inatusumbua sana, kama kiswahili tu watu kinawagonga unategemea mtu atakuwa na miujiza kuongea lugha ambayo siyo yake na haitumii mara kwa mara?. Mimi nafikiri kasumba hii inatutafuna na ndiyo inatufanya tusiendelee, hata wataalamu wetu huenda tunawalalamikia kuwa wamesaini mikataba mibaya, si wanajifanya wanajua kiingereza kumbe hawahjui wanaishia kusaini tu. Ukweli ni kwamba ni matatizo wa kuwatawaliwa na wakoloni, kwani hao wabunge walioongea kiingereza leo wanazidiwa kiingereza na Fabio Capelo -kocha wa Uingereza ? mbona waingereza tena ndiyo wenye lugha hawasemi hivyo na wala hata yeye haoni aibu. Mimi sijawahi sikia Marcio Maximo akichekwa kwa kiingereza chake kibaya, tena ni kibaya kuliko watanzania wengi wanavyooongea.

Tuache kiingereza kiwe lugha kama lugha zingine Kifaransa, kireno, kimatumbi n.k , hiyo sifa ya kiingereza kama ina maana hivyo je ni miongoni mwa sifa za kuwa Mbunge? kama siyo sifa kwanini sasa. Hiyo ni kutishana tu kunakotumiwa na wajanja wachache tena wasio na uwezo.

Nimesema kwamba kiswahili chenyewe ni shida kwa watu wengi mbona hatuchekani, mbona mzee wa kiraracha hawezi kutamka Nchi anasema NJI mbona hakuna anayemcheka au kwa sababu ni kiswahili?
 
Mosesk lazima uelewe nyakati na mazingira. Km umetakiwa uongee kiingereza ni lazima uongee kiufasaha si suala la kasumba au ukoloni. Kiingereza hata upinge vipi itaendelea kuwa lugha ya kimataifa na si lugha ya taifa kam kiswahili.

Mie kwa ushauri wangu tu ni kwamba, Watanzania tuongee kiswahili popote pale hata kama tunajua kiingereza , mbona mataifa mengi tu mfano warusi, wachina n.k wanaongea lugha zao hata km wanajua ung'eng'e? Tutumie wakalimani basi inatosha.

kiswahili nacho ni kigumu nakubali lakini angalau unakuwa unajua unaongea nini, maana suala la kuchanganya tenses ktk kiingereza ni critical mistake utake usitake.

ila tatizo jingine pia ni kuwa tukiambiwa tuongee kiswahili, sasa tuananza kuunda "KISWAHENGLISH" MAANA HATA MIE HAPO JUU NIMEJISAHAU.

Tuiheshimu lugha yetu mbona inaheshimika sana na watu na mataifa mengi yanatuheshimu na kuthamini kiswahili.

Nchi km Urusi ina mpaka chuo kikubwa kabisa kinafundisha kiswahili.

Thamini cha kwako
 
Sijui ni ushamba , sijui ni ulimbukeni , sijui ndiyo ukoloni bado upo mpaka vichwani kwetu!. Mimi nashangaa sana mtu anapofikiri kujua kiingereza sijui ndiyo elimu ? . Hii kasumba inatusumbua sana, kama kiswahili tu watu kinawagonga unategemea mtu atakuwa na miujiza kuongea lugha ambayo siyo yake na haitumii mara kwa mara?. Mimi nafikiri kasumba hii inatutafuna na ndiyo inatufanya tusiendelee, hata wataalamu wetu huenda tunawalalamikia kuwa wamesaini mikataba mibaya, si wanajifanya wanajua kiingereza kumbe hawahjui wanaishia kusaini tu. Ukweli ni kwamba ni matatizo wa kuwatawaliwa na wakoloni, kwani hao wabunge walioongea kiingereza leo wanazidiwa kiingereza na Fabio Capelo -kocha wa Uingereza ? mbona waingereza tena ndiyo wenye lugha hawasemi hivyo na wala hata yeye haoni aibu. Mimi sijawahi sikia Marcio Maximo akichekwa kwa kiingereza chake kibaya, tena ni kibaya kuliko watanzania wengi wanavyooongea.

Tuache kiingereza kiwe lugha kama lugha zingine Kifaransa, kireno, kimatumbi n.k , hiyo sifa ya kiingereza kama ina maana hivyo je ni miongoni mwa sifa za kuwa Mbunge? kama siyo sifa kwanini sasa. Hiyo ni kutishana tu kunakotumiwa na wajanja wachache tena wasio na uwezo.

Nimesema kwamba kiswahili chenyewe ni shida kwa watu wengi mbona hatuchekani, mbona mzee wa kiraracha hawezi kutamka Nchi anasema NJI mbona hakuna anayemcheka au kwa sababu ni kiswahili?
mkuu kama unakumbuka kwenye mdahalo wa dr wa ukweli alisema namnukuu " hata mimi nimeathirika kule kwangu karatu, kuna hoteli 20 za kitalii na hata mbeba mizigo ni kutoka nje ya nchi, na wanayo sababu kwani wanasema wageni wangu ni kutoka nje ya nchi na anapotembea anataka aulize swali hili na hili" mwisho wa kunukuu so kingereza kina umuhimu wake hususani dunia hii tunaishi sas ivi............
kuna mifano mingi tuu kama umeshawahi kwenda china utaona ...........kwenye kila mabango yao ya matangazo wanatumia lugha mbili yaani kichina na kingereza.....
asante
 
Hakuna anayekataza mtu kujua siyo kiingereza tu bali lugha za kigeni angalau moja, ninachojiuliza hapa kuna mtu alikuwa nashadadia kuwa wabunge walikuwa wanatokwa jasho, na akaaenda mbali zaidi na kusema kuwa wengine wangeugua. Lakini bahati nzuri sana mimi nimesikiliza bunge kupitia TV4africa kwa bahati mbaya naishi nje ya TZ na wabunge wetu wamejitahidi na sikuona tatizo mpaka mtu anashadadia kitu kama kile. Na ukiangalia vizuri nimetoa mfano wa kocha wa Taifa wa Uingereza anaongea kiingereza kibovu kabisa lakini ni kocha wa uingereza. Mbona haimpi shida. Zaidi ya yote kama ulifuatilia Maximo alikuwa naongea kiingereza kibovu kuliko kawaida lakini hakuna aliyeshangaa sasa iweje leo tuone kiingereza ndiyo kila kitu? na hapo ndiyo ajenda yangu! hata waingereza wenyewe wanasona lugha za kigeni. Wajerumani wengi wanajua kiingereza lakini shughuli zao zote za kiserikali ndani na nje ya nchi wanatumia lugha yao.

Zaidi ya yote ili kuonyesha jinsi ambavyo tunapaparika sana na kiinereza kuna mkutano mmoja wa wakuu wa nchi, Mhe. Mkapa akiwa rais aliongea Kiingereza lakini Rais wa msumbiji ambaye hawatumii kiswahili alitumia kiswahili.

Kwa hiyo kimsingi wabunge wameongea vizuri tu kiingereza kwa kadri ya uwezo wao. Nimetoa pia mifano kwamba mambo ya lugha siyo mambo rahisi ufasaha wa lugha ni ngumu kujua cha msingi je unaoongea nao wanaelewa?.

Kwa kifupi sipingi watu kujua kiingereza lakini ningependa watu wajifunze kiingereza na lugha zingine kama Kifaransa,Kireno, Kijerumani, Kichina , Kirusi n.k.

Nchi inatakiwa kuwa na watu wa aina zote siyo kiingereza tu, na ieleweke kuwa matamshi ya lugha yanaathiriwa sana na lugha mama!
 
Jamani,

Kwa kweli nami naunga mkono hoja kwamba tumeendekeza mno kutukuza kiingereza. Ndiyo maana hata watoto wetu darasani mambo hayapandi kwa sababu ya kung'ang'ania kiingereza. Hivi ni nani asiyejua kuwa hivi sasa kiswahili kinatambulika kama lugha rasmi ya Muungano wa Afrika (AU)? Inawezekana wengi hawajui. Lakini habari ndiyo hiyo. Hii ina maana kwamba kiongozi yeyote akiamua kuongea kiswahili ndani ya vikao vya AU atafanya bila zengwe na wajumbe wasioelewa kiswahili watatafsiriwa. Hivi sasa, nchi nyingi za kiafrika zimeingiza lugha kiswahili kwenye mitaala yake ili wananchi waanze kujifunza lugha inayochukuliwa kama ya Afrika.

Ajabu ni kwamba watanzania wenyewe tupo mstari wa mbele kukitupa kiswahili. Hata rais wetu mwenyewe jk sijawahi sikia anaongea kiswahili kwenye vikao vya AU pamoja na kwamba nae kiingereza achoongea ni 'plain' tu. Hakina mvuto kabisa. Kama ni kiongozi anayeongea kiingereza ni Mhe. Mkapa. Kiingereza chake ni clear hakina chengachenga na kizito siyo kama cha mkwele. Jamani si mnakumbuka wakati wa 'World Economic Forum'???
 
Great thinkers mwashangaa nini hao wabunge kushindwa kujieleza kiingera,ili hali wengi wao wanashahada feki,inakuwaje intellectual tena hata Mwenye PHD ashindwe kujieleza kiingereza,haiingii akilini kwangu mimi kama mwanazuoni.kiingereza ndio lugha itakayotumika huko kuiwakilisha nchi yetu,so how can Tanzanians be represented by VIHIYO who know nothing to express themselves in ENGLISH? Tunataka vichwa bwana sio viwiliwili bungeni.
 
SADC hawana mainterpreters, ndiyo maana ilimlazimu mh. Spika kuwaeleza wagombea wajieleze kwa kimombo, ambayo ndiyo lugha itakayotumika. Hivyo kujua kiingereza ni lazima na iwe moja ya vigezo vya qualification. Mbunge anatakiwa kujenga hoja kwa kuelezea kiufasaha. Kama itakuwa shida, CHADEMA wana wabunge wasomi kibao ambao hawajachakachua vyeti vyao. Wapo akina Lissu, Zitto, Kahigi, Mtema, Mnyika. Hawa jamaa hata IQ zao hakuna mtu ataquestion. Vilevile kama nilimwelewa mtoa mada, anasema na bunge letu liendeshwe kwa kimombo pale Dom, hiyo itakuwa ngumu kutokana na wabunge wengind wa CCM kuwa na elimu ya ngumbaru. Mfano Jah People, Maji Marefu, Airo, Lusinde nk.
 
Kuongea kiingereza si ujanja, kikubwa ni IQ yako inavyofanya kazi, kama mtu hawezi kuongea kiingereza anaongea kiswahili translator atafanyakazi ya kutafasiri. kuna watu bongo wanaongea kiingereza kizuri lakini kichwani hamna kitu. Binafsi naona wanaosisitiza kiingereza wanakasumba ya kikoloni. unatakiwa kujua kiasi na kujiamini, so hata hao uliowaona wanatumia nguvu kujieleza kwangu natafsiri kuwa walikuwa hawajiamini tu-"lack of confidence" tu

kweli kabisa but atlist kwa watu wa nyadhifa fulani waongee lugha hata mbili. kisw & kiingerza
 
Weee Weee, koma kabisa.

Unataka Sikonge Mbunge wetu awe Bubu milele?

Itabidi na Ndevu abadilishe kutoka Hitler na kuwa Mhandisi......

695bab71-39a8-4274-9fcb-3c1074443dd0.jpg

Mwalimu wa darasa la Tatu...........
 
Kuongea kiingereza si ujanja, kikubwa ni IQ yako inavyofanya kazi, kama mtu hawezi kuongea kiingereza anaongea kiswahili translator atafanyakazi ya kutafasiri. kuna watu bongo wanaongea kiingereza kizuri lakini kichwani hamna kitu. Binafsi naona wanaosisitiza kiingereza wanakasumba ya kikoloni. unatakiwa kujua kiasi na kujiamini, so hata hao uliowaona wanatumia nguvu kujieleza kwangu natafsiri kuwa walikuwa hawajiamini tu-"lack of confidence" tu

Huwezi ukadharau good command ya kiingereza, communication is key to any senior position tofauti na low cadre jobs. Watanzania tunaonekana stupid mara nyingi kwa kuwa tu we do not have a good command of spoken and written english.

It's funny though unapimwa utendaji wako wa kazi kwenye interview. Logic believes that good command of the language is part of intelligence.
 
Back
Top Bottom