Sijui ni ushamba , sijui ni ulimbukeni , sijui ndiyo ukoloni bado upo mpaka vichwani kwetu!. Mimi nashangaa sana mtu anapofikiri kujua kiingereza sijui ndiyo elimu ? . Hii kasumba inatusumbua sana, kama kiswahili tu watu kinawagonga unategemea mtu atakuwa na miujiza kuongea lugha ambayo siyo yake na haitumii mara kwa mara?. Mimi nafikiri kasumba hii inatutafuna na ndiyo inatufanya tusiendelee, hata wataalamu wetu huenda tunawalalamikia kuwa wamesaini mikataba mibaya, si wanajifanya wanajua kiingereza kumbe hawahjui wanaishia kusaini tu. Ukweli ni kwamba ni matatizo wa kuwatawaliwa na wakoloni, kwani hao wabunge walioongea kiingereza leo wanazidiwa kiingereza na Fabio Capelo -kocha wa Uingereza ? mbona waingereza tena ndiyo wenye lugha hawasemi hivyo na wala hata yeye haoni aibu. Mimi sijawahi sikia Marcio Maximo akichekwa kwa kiingereza chake kibaya, tena ni kibaya kuliko watanzania wengi wanavyooongea.
Tuache kiingereza kiwe lugha kama lugha zingine Kifaransa, kireno, kimatumbi n.k , hiyo sifa ya kiingereza kama ina maana hivyo je ni miongoni mwa sifa za kuwa Mbunge? kama siyo sifa kwanini sasa. Hiyo ni kutishana tu kunakotumiwa na wajanja wachache tena wasio na uwezo.
Nimesema kwamba kiswahili chenyewe ni shida kwa watu wengi mbona hatuchekani, mbona mzee wa kiraracha hawezi kutamka Nchi anasema NJI mbona hakuna anayemcheka au kwa sababu ni kiswahili?
Huyo Capello na Maurinho wanatoka mataifa makubwa na yanayojitosheleza sana hasa kimaendeleo. Hivyo wana lugha zao.Na hata akienda uingereza akaongea kwa kuunga unga bado wanamuadmire sana kwa sababu at least yeye ni multilingual kuliko waingereza wengi ambao ni bilingual?
Kuna debate kubwa uingereza kwa wao kutokuwa na uwezo wa kuongea lugha zingine while everybody in the world can speak a bit of english.
Sasa tukirudi kwenye point, demand ya sisi watanzania ni kujua kiingereza. Kwetu hii language ni very strategic kwa sababu tunazungukwa na mataifa karibu yote ambayo yana very good command ya english (except a few). Sasa hii inatupa challenge sana kupata kazi ambazo ni open pia kwa majirani zetu.
Mkikutana na mkenya au mganda na the same qualifications au hata kama umemzidi lakini akaweza kuwaimpress potential employers kwa lugha ya kiingereza basi ni likely watapata hiyo kazi kuliko wewe unayehangaika kuelezea point kisa lugha inakugonga.
Hata akija muitaliano au mjerumani muwekezaji japo hajui vizuri kiIngereza lakini ataprefer mfanyakazi anayejua kiingereza kuliko ambae hajui.
Sasa wakati huu tunapofungua mipaka kiingereza ni very strategic language than any other time in the history of Tanzania.