Nataka Serikali moja tu ya Muungano, sitaki mbili wala tatu

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,538
17,473
Utanganyika na uzanzibari imeanza kusikika, wenye mamlaka nao wamekaa kimya hawataki kukemea ubaguzi huu unaoendelea nchini.

Tulishaungana tangu 1964, hakuna serikali ya TANGANYIKA wala ya Zanzibarinatikiwa iwepo hadi leo,tumewezaje kuungana bila serikali kuungana, Zanzibar inakuaje na serikali!? wakati TANGANYIKA haina serikali kwanini kuwe na serikali ya zanzibar?

Mi nadhani kukubali uwepo wa serikali mbili au tatu ni kuvunja muungano wetu, Serikali unatakiwa iwe moja tu wala si vinginevyo.

Kinachoitwa kero za Muungano ni matokeo ya serikali mbili za kibaguzi zilizopo kwasababu mzanzibari anapaswa awe na haki sawa na mtanganyika ndani ya serikali ya muungano wa Tanzania hiki kizungumkuti ndio kinaleta ubaguzi!

Zanzibar wala Tanganyika hazikupaswa kuwa na serikali ili kuonyesha kuwa tumeungana na sio muungano nusu yaani wa serikali mbili!

Tunapaswa tuwe na Rais mmoja na makam wake kutokea mahali popote pa muungano bila kujali uzanzibari wala utanganyika!

Niwaombe viongozi wakuu wa mihimili ya dola waanze kufikiria serikali moja tu ya muungano na sio mbili wala tatu!

Asanteni.
 
Mimi nataka uwepo wa Serikali kamili ya Tanganyika (Tanzania), na pia serikali kamili ya Zanzibar. Na hivyo hicho kinachoitwa muungano, kisiwepo kabisa.

Yaani ifikie wakati hiyo Zanzibar iwe kama Comoro tu. Hatuwezi miaka nenda kuwa na muungano wa manung'uniko, muungano wa kubembelezana, muungano wenye kuipendelea zaidi nchi moja, muungano wa kibaguzi, nk. Ni bora usiwepo kabisa.
 
Dadeki kwamba huwataki kabisa hata kwa Mkopo. Mimi pia naona Waende tu ni Wasumbufu sana tukiweka Muungano wa Serkali moja watageuka Wapinzani wa Serkali na tukiweka Serkali 3 huu ni unafiki tu si Muungano. Hizi Serkali mbili ndo Uchafu kabisa Wakwende tu.
 
Utanganyika na uzanzibari imeanza kusikika, wenye mamlaka nao wamekaa kimya hawataki kukemea ubaguzi huu unaoendelea nchini.

Tulishaungana tangu 1964, hakuna serikali ya TANGANYIKA wala ya Zanzibarinatikiwa iwepo hadi leo,tumewezaje kuungana bila serikali kuungana, Zanzibar inakuaje na serikali!? wakati TANGANYIKA haina serikali kwanini kuwe na serikali ya zanzibar?

Mi nadhani kukubali uwepo wa serikali mbili au tatu ni kuvunja muungano wetu, Serikali unatakiwa iwe moja tu wala si vinginevyo.

Kinachoitwa kero za Muungano ni matokeo ya serikali mbili za kibaguzi zilizopo kwasababu mzanzibari anapaswa awe na haki sawa na mtanganyika ndani ya serikali ya muungano wa Tanzania hiki kizungumkuti ndio kinaleta ubaguzi!

Zanzibar wala Tanganyika hazikupaswa kuwa na serikali ili kuonyesha kuwa tumeungana na sio muungano nusu yaani wa serikali mbili!

Tunapaswa tuwe na Rais mmoja na makam wake kutokea mahali popote pa muungano bila kujali uzanzibari wala utanganyika!

Niwaombe viongozi wakuu wa mihimili ya dola waanze kufikiria serikali moja tu ya muungano na sio mbili wala tatu!

Asanteni.
Sasa wewe unataka chadema wasitawale daima?
 
Ishu sio chadema wala CCM,ishu tunatakiwa tuwe na serikali moja,taifa moja na nchi moja ya Tanzania,yenye Rais mmoja,Bunge mmoja,na dola moja!na sio mbili mbili kama sasa huyo ndio ubaguzi mkuu unatuletea kero za MUUNGANO!!

Tukiwa wamoja wenye haki sawa wote hakutakua na kero za MUUNGANO tena nchini!!!

Kero hizi ni matokeo ya serikali mbili,Bunge mbili,mahakama mfumo mbili yaani mbili mbili WAKATI wengine wanataka tatu tatu ambayo sio KABISA!!

Tukianza tatu tatu tunaua mawazo ya NYERERE na karume kuungana!!
 
Dadeki kwamba huwataki kabisa hata kwa Mkopo. Mimi pia naona Waende tu ni Wasumbufu sana tukiweka Muungano wa Serkali moja watageuka Wapinzani wa Serkali na tukiweka Serkali 3 huu ni unafiki tu si Muungano. Hizi Serkali mbili ndo Uchafu kabisa Wakwende tu.
Tatizo la huu muungano liko sehemu moja tu; kuipa Zanzibar mamlaka na kuubakiza utaifa wake! Halafu wakati huo huo kuiondolea Tanganyika mamlaka yake, na pia kuufuta utaifa wake.

Hili jambo limesababisha kero za huo muungano zisimalizike. Maana wenzetu kila siku huwa wanavutia kwao tu. Hivyo ni bora wakapewa tu mamlaka yao ya kujitawala na kujitegemea kwa 100%
 
Utasikia haya ni mambo ya sio ya kimuungano yanashughulikiwa na wazanzibar wenyewe je Huku Bara mambo yasiyo ya kimuungano yanashughulikiwa na nani? Tunataka Tanganyika yetu
Mbaya zaidi kwenye kipindi cha Bunge, hizo Wizara wanazosema sio za MUUNGANO na wao wanakuwepo na wengine huenda mbali kwa kuchangia..hivi Mtanganyika anaweza changia kwenye Baraza la Wawakilishi?

Pili wanakaa na kulipwa sitting allowances kwa wizara zisizo za kwao,hakika tunaibiwa Watanganyika

Mwisho ila sio kwa UMUHIMU, wapo wengi(kiidadi) bila sababu yoyote ya msingi na kanchi kao kadogo, wabunge 10 tu wangetosha kuwakilisha mawazo yao bungeni
 
Utanganyika na uzanzibari imeanza kusikika, wenye mamlaka nao wamekaa kimya hawataki kukemea ubaguzi huu unaoendelea nchini.

Tulishaungana tangu 1964, hakuna serikali ya TANGANYIKA wala ya Zanzibarinatikiwa iwepo hadi leo,tumewezaje kuungana bila serikali kuungana, Zanzibar inakuaje na serikali!? wakati TANGANYIKA haina serikali kwanini kuwe na serikali ya zanzibar?

Mi nadhani kukubali uwepo wa serikali mbili au tatu ni kuvunja muungano wetu, Serikali unatakiwa iwe moja tu wala si vinginevyo.

Kinachoitwa kero za Muungano ni matokeo ya serikali mbili za kibaguzi zilizopo kwasababu mzanzibari anapaswa awe na haki sawa na mtanganyika ndani ya serikali ya muungano wa Tanzania hiki kizungumkuti ndio kinaleta ubaguzi!

Zanzibar wala Tanganyika hazikupaswa kuwa na serikali ili kuonyesha kuwa tumeungana na sio muungano nusu yaani wa serikali mbili!

Tunapaswa tuwe na Rais mmoja na makam wake kutokea mahali popote pa muungano bila kujali uzanzibari wala utanganyika!

Niwaombe viongozi wakuu wa mihimili ya dola waanze kufikiria serikali moja tu ya muungano na sio mbili wala tatu!

Asanteni.
Wewe ni mtanganyika hujui Thamani ya Nchi ndio maana NChi yako Tanganyika huijui hata iko wapi
 
Back
Top Bottom