Nataka nianze kula mjani

Nataka nianze kula mjani

Kwa hiyo conclusion yako ni watu wajizimue na mjani au mjani si kitu poa?
Uwepo umakini tu kwenye kutambua kiwango chako, ukizidisha mambo yenyewe ndo kama hayo.
 
Niwe mkweli..(I'm not promoting it though)

Sikuwahi kuvuta bhangi toka utotoni hadi mwaka huu mwezi juzi..nimevuta kama mara 4 kwa interval ya wiki 1 1.

Nimegundua vitu ambavyo pengine nisingevigundua au ingenichukua muda mrefu.
Umegundua nn

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
MREJESHO

Wakuu niliahidi nitaleta mrejesho wa experience yangu baada ya kutumia mjani kwa mara ya kwanza;

juzi nikiwa skonga kuna washkaji zangu kindaki ndaki walikua wakinieleza kwamba wanazo cookies ambazo zimetengenezwa kwa mjani. Ukiviangalia hivyo vi cookies ni vidogo tu na huwezi kufahamu kama zimetengenezwa kwa mjani ila ukila kuna vimbegu vidogo vidogo vile vya bangi.

Basi bwana! Juzi ijumaa tukiwa shuleni asubuhi mwamba akanikatia kipisi kidogo sana cha ile cookie nilikaa kwa muda wa kama nusu saa hivi ngoma ikakubali kichwani. Niliingia darasani nikiwa na wenge si la kitoto, mwalimu anafundisha unamsikia lakini baada ya sekunde 2 unasahau alicho kisema.

Najaribu kuandika lakini hata ninacho kiandika sikioni na hata hakieleweki, nikawa najikuta nacheka mno darasani bila hata sababu ya msingi, kitu kidogo ambacho hakiwezi kumchekesha mtu kwangu mimi Ilikua very funny.

Basi baada ya kuona sielewi kitu darasani nikachukua kitabu changu nikakiweka kwenye begi nikaenda nje huku nacheka kinoma yani, kufika nje nikakaa kwa dk 2 nikarudi tena darsani nikaona jau nikarudi tena nje mpaka chooni nikakaa chini nikaanza kucheka nisijue kama ni kazi ya mjani.

Nilichogundua kuhusu hii kitu sio kwamba unakua completely off hapana! Ila you don't have fully control over yourself by percent. Basi bhana baada ya kula chakula cha mchana ngoma ikapoa kichwani nikarudi kwenye hali ya kawaida. Na kila kitu kilichotokea nikiwa high Ilikua ni kama ndoto maana nilikua naongea na mshikaji wangu mmoja lakini baada ya hapo sikua nakumbuka hata niliongea nae nini.

Kesho yake ambayo ndo jumamosi ya jana ambayo kwa namna moja au nyingine ndiyo imenifanya nilete huu mrejesho hapa, nilifika skonga asubuhi sasa kwakua hii ndo wiki ya kwanza tangu shule zifunguliwe hakukua na wanafunzi wengi, kama kawaida nikaenda bwenini kwa washkaji tukagonga chai kisha tukatimba darasani.

Basi bwana! Kwakua siku iliyopita nilikula Ile cookie na haikuniendesha vibaya sana nikawaza naimudu, nikaamua kuongeza kipimo, nilikula kipande kikubwa karibia na kuimaliza, baada ya muda mfupi jau likaanza. Pale darsani tulikua mimi na washkaji zangu watatu pamoja na demu mmoja, aisee nilinyanyuka nikaanza kuzunguka zunguka bila hata sababu za msingi, nikawa nacheka kinoma yani.

Yani ubongo wangu ulikua ukifanya kazi kwa spidi ya ajabu na nikawa na zaidi ya vitu elfu moja navifikiria kwa wakati mmoja hali iliyonifanya niwe kama mtu aliyewehuka, nikawa siwezi kukaa nikafocus na kitu kimoja nitataka niandike at the same time nisimame, niende nje nirudi, ikafika kipindi mpaka nikataka nipige kelele I was running out of my mind.

Muda huo washkaji zangu hawana mbavu walicheka mnooo, mwamba mmoja akaniambia twende nikupeleke bwenini ukalale ukiamka utakua fresh. Shuleni kwetu mabweni ya wavulana yapo nje ya shule hivyo unaanza kutoka nje ya geti la shule ndo unaenda bwenini, basi bwana! Nje tu ya shule tukakutana na mdada mmoja akawa anatuuliza kuhusu performance ya shule kwakua anataka kumleta ndugu yake ambaye alikua anarudia.

Nikadakia na kuanza kujibu, aisee yule mwamba alikaa pembeni anashangaa anatamani acheke lakini anashindwa, kwa kifupi nilikua naongea pumba za hali ya juu sana alafu nilikilemba kingereza kana kwamba nipo redioni nafanya advertisement ya shule yetu, yule dada pia alishangaa na hata hakunijibu akajua kwamba kuna kitu hakipo sawa.

Basi tukafika bwenini nikavua viatu nikapanda kitandani, aisee maluwe luwe yakaongezeka na safari hii ikawa even worse, kumbuka nilikuwa nawaza karibia mambo mia kwa wakati mmoja hivyo sikuweza kufocus na kitu kimoja. Pale kitandani nikawa mara niamke mara nipige push-ups mara nirudi kitandani, kichwa kiliniuma ikafika muda nikapoteza kabisa kumbukumbu nikawa sijui kabisa hata nilipo.

Ikafika kipindi nikatamani nilie nikaanza kujutia, nikawa nakumbuka baadhi ya comments za wadau humu kwamba mjani ukikukataa unaweza ukawa mwendawazimu moja kwa moja basi kwa hali niliyokua nayo hapo kitandani nikawa naomba Dua kimoyo moyo.

Kuna muda nikawa nahisi kitu kinapanda kutoka chini kwenda kichwani, yani kwa kifupi hata ukiniona nilikuwa kama mtu aliyewehuka. Baadaye kabisa jioni kwenye mida ya saa 11 nikaanza kujisikia vizuri na nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida. Basi nikawaaga wadau pale nikaanza safari ya kurudi home, nakumbuka nilitembea ka distance kadogo nikaanza kuhisi kichwa kinaanza kuwa kizito na macho yanaanza tena kupoteza focus.

Nikasimamisha bodaboda nikawa namuelekeza ila anacho nijibu nikawa hata sisikii, basi bwana! Nikafika home mida ya saa 12 jioni, huku kichwani sipo sawa kabisa nikaangalia TV kidogo kwenye mida ya saa moja usiku nikaingia kulala ndo kushtuka mida hii ya saa 9 usiku kidogo najisikia vizuri ila maluwe luwe bado kwa mbaali nayasikia nikaona sio mbaya nikileta mrejesho Kwa watu wangu wa JF.

NB: ukila mjani sio kwamba unakua completely off hapana! unakua na ufahamu wako lakini hauwezi kujicontrol kwa asilimia mia moja na kingine akili yako inakua na work rate kubwa inayokufanya uwaze mambo hata zaidi ya 1000 kwa wakati mmoja kitu ambacho kinakuletea hallucinations. Niliahidi nitaleta mrejesho na nimefanya hivyo wassalam! ..
Oya wakusoma hzo cookie zinapatikana wap najambo nazo??
 
Pole sana kijana.

Nikiri kuwa nikiwa na Umri kama wako nilikuwa na uchu sana wa kujaribu kuvuta Bhangi kama wewe. Asilimia kubwa ya Rafiki zangu niliokuwa naambatana nao walikuwa wavutaji. Na kila jioni lazima tutoroke kwenda Nje ya Shule kuvuta.

Ajabu ni kwamba mmojawapo Wa wale Marafiki alikuwa mkali sana kwangu kuwa nisijaribu kabisa kuvuta, ilhali yeye alikuwa mvutaji. Kwa sababu yake nikawa Mpasishaji kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine ila sikuthubutu kabisa kuitia mdomoni. Jamaa aliniambia naweza kuchanganyikiwa kabisa nikijaribu kuvuta.

Tulipoingia kidato cha Pili kuna Bro alikuwa mbele yetu, yeye Form 4 akaanza kuonesha Dalili za kuwehuka,, Shule ikamrejesha nyumbani akajiuguze kwanza.

Wazazi wake (wakati huo Walikuwa Wanafundisha Chuo cha Ushirika) wakahangaika naye sana mpaka Mirembe lakini Jamaa hakurejea tena kwenye utimamu. Ikawa tukienda mtoni kufua tunamkuta kule analala tu Juu ya mawe.

Mwaka Jana nimeenda likizo Jamaa yupo yupo tu, hana Familia, anaishi kwenye Nyumba ya Mzee wake na akili sometimes yes, sometimes no. Shule hakuweza kuendelea nayo tena.

Mwingine tena, tukiwa likizo ya kuingia kidato cha tatu akavuta Bhangi akaenda kukabaka Katoto ka Darasa la sita huko kwao, Wazazi Wa yule mtoto wakamkazia Jamaa akapelekwa Jela za watoto zile, miaka miwili.. Aliporudi mtaani inasemekana akatishia kumwua Mamake na panga, akaswekwa Ndani tena (jela ya wakubwa sasa). Naye sasa hivi ni Baunsa kwenye makumbi ya starehe, anailaani Bhangi mpaka Leo.

Mpaka Leo Namshukuru yule Mwamba aliyekuwa ananiletea unoko nisijaribu kuvuta, ilhali Shule nzima ilikuwa inaniweka kwenye kundi la wavutaji kutokana na ile Kampani..
 
Niwe mkweli..(I'm not promoting it though)

Sikuwahi kuvuta bhangi toka utotoni hadi mwaka huu mwezi juzi..nimevuta kama mara 4 kwa interval ya wiki 1 1.

Nimegundua vitu ambavyo pengine nisingevigundua au ingenichukua muda mrefu.
Mama pretty ona watu wanavyoangamia..😂
 
I took a splif this morning..and it make me feel so groove man..thats why i cant refuse it man... INTERNATIONAL HERB-culture
 
Niwe mkweli..(I'm not promoting it though)

Sikuwahi kuvuta bhangi toka utotoni hadi mwaka huu mwezi juzi..nimevuta kama mara 4 kwa interval ya wiki 1 1.

Nimegundua vitu ambavyo pengine nisingevigundua au ingenichukua muda mrefu.
umegundua vitu gan bro tupe maujanja
 
Back
Top Bottom