Nataka kuwa mwana usalama wa Taifa

mkuu kuajiriwa ndani ya idara ya usalama wa taifa huwa kuna vigezo huwa vinaangaliwa lakini katika hivo vigezo vinatofautiana maana usalama kigezo cha kwanza huangaliwa una kipaji cha aina gani.

ili uweze kufanya usalama kitu cha kwanza ujiangalie una kipaji cha aina gani na jee hicho kipaji chako unakitumia vipi .
 
Umegundua nini kwenye hiyo kazi? Soma sana uwe expatriate upate mshara hadi milioni 17 Kwa mwezi uachane na mawazo ya TISS.
 
Nimejikuta tu narudia tena kusoma uzi mzima pamoja na maoni yenu.
Nimefarijika na kujipa moyo kuwa IPO SIKU TU.
Ngoja niendelee kufanyia kazi baadhi ya maoni yenu wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mimi ninaipenda sana kazi hiyo, Elimu Yangu Nina Diploma ya Civics and Kiswahili, Nina Bachelors Degree in English and Kiswahili Language -UPPER SECOND CLASS (HONNOURS). Kama yupo MTU wa kuniwezesha kutimiza ndoto Yangu Hii naomba anisaidie .
 
Habarini wakuu.

Mimi ni memba mpya(kwenye kuanzisha uzi) ila ni memba wa muda kama shabiki wa JF.
Huu ni uzi wangu wa kwanza kuuanzisha(mnisamehe kama kuna mahali nitakosea)

Turudi kwenye maada..

Siku nyingi(kabla sijawa memba wa jf) nimekuwa nikifuatilia sana masuala mazima ya kiusalama kupitia movie na magazeti,na baada ya kupakua app ya JF nilikutana na maada mbal mbal zinazohusu maswala mazima ama story zinazohusu usalama.

Baada ya kuendelea kufuatilia na kusoma kila nnachokutana nacho na kinahusu usalama,niliweza kufunguka kiakili na kimawazo kuhusu swala zima la usalama.

Miongon mwa vitu vilivyonifungua akili ni pamoja ya namna hawa watu(mashushushu) wanavyopatikana,ikiwa ni pamoja na mashulen na kupitia vyombo mbal mbal vya usalama kama JKT n.k

Baada ya kuwa nimefunguka kiakili kuhusu jambo hili ,nilikata tamaa na kuona siwez tena kuwa shushushu kwa sababu sipo shule,na siwez tena kwenda JKT kwa maana umri umeshaenda(nna miaka 27 na elimu yangu ni kidato cha 4).

Lakini nilijipa moyo na sikujidekeza kwa kuendelea kukata tamaa,na badala yake niliendela kufuatilia maada mbali mbali na historia mbali mbali za kijasusi kupitia hapa hapa JF kama maada za mkuu The bold na za watu wengine wengi.

Sasa bas leo nimeamua kuvunja ukimya na kuamua kuja kwenu wana jamvi na kuwaomba msaada wa kimawazo na ushauri wa nn nifanye ama nn nifuate ili niweze kuwa miongoni mwa hawa watu wa usalama(TISS) ama kama kuna kikosi kingine cha kiusalama. Nikimaanisha nitaingia vipi ndani ya 18 ya hawa jamaa ili wanichukue na mm?

Nafahamu kuwa ni ishu ya siri na ni ishu ambayo sio ya kuweka hadharan,kama kuna mambo ya hadharan mtanipatia,na kama kuna ushauri wa sir bas hata PM nitaupokea pia.

Mm ni mzarendo na ninafaham hii kazi inahitaji moyo na unahitaji uzarendo pia,katika hili hakuna shida.

Naipenda nchi yangu TANZANIA na nipo tayal kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote.



Nawasilisha hoja,naombeni msaada wenu.
Na naomba radhi sehemu yeyote nitakayokuwa nimekosea.
HABARI KIONGOZI WW UTAKUWA MKURYA....SASA UKIPATA NA MIMI NIUNGANISHE NAO MANA UZALENDO WANGU HAUNA CHEMBE YOYOTE YA UKAKASI.
 
Back
Top Bottom