Nataka kuwa mwana usalama wa Taifa

Nataka kuwa mwana usalama wa Taifa

Kigezo cha jamaa kutoitwa huko haina maana kuwa yeye hana sifa, kwanza kuna mapungufu kadhaa kwenye enrollment yao.
Na kuepuka upendeleo undugu undugu nk nchi nyingi zilizoendelea siku hizi wanatoa matangazo ya ajira za usalama wa taifa, hivyo wote wenye uwezo unaotakiwa wanaapply kwa uwazi zaidi na wanapitia vetting na process nyingine.
Afadhali Mkuu umemwambia ukweli. Hivi mtu unaanzaje kumwambia mwenzako hauna vigezo, na ni jambo dhahiri kabisa idara kama hizi kuna kubebana sana, sio Tanzania tu ila karibia Afrika nzima. Na kutokana na nature ya kazi yenyewe, kubebana pia inachangia.

Lazima tujue kuwa hii Idara ni Idara nyeti mno kwa nchi zilizo serious.
 
Mimi swali langu kwenye hii mada ni Je,kuna uwezekano wa hao jamaa kukuidentify,wakakupitisha ktk michakato yao yote ikiwa ni pamoja na kukufanyia vetting zote na kisha wakakudump? kama kuna mwenye uelewa juu ya hili tafadhali......
Yah, na ni wengi tu.
 
I hope nia yako sio kusumbua wenzako mtaani na kuwauliza "unajua mimi ni nani"? au kugoma kulipa fine za traffic kisa wewe ni usalama wa taifa, au kuweka bastola kwenye meza bar!!!!...unatakiwa uwe mzalendo-humble/down to earth, msikivu, mwenye kifua kizito na 'fairly' intelligent...darasa sio kigezo prkeyake, wako mpaka darasa la saba...
Cha ziada, hakikisha hujawai kuiba hata kuku huko kijijini kwenu maana watakuja hadi huko kukufanyia screening/background check....goodluck
Asante
 
Pole sana Mkuu!

-Hongera kwa moyo wa kizalendo na nnakusihi usikate tamaa.

-Tambua ya kuwa kila jambo lina makusudi chini ya jua, kila unachokiona kiwe kibaya au kizuri basi tambua Mungu anafahamu. Huwezi jua ni nini hasa la Mungu mpaka sasa usiwe ktk hiko kitengo.

-Achana na wanaosema kuwa hauna vigezo, vigezo unavyo. Hakuna kigezo kikubwa kama nidhamu na uzalendo. Na hii sio Tanzania tu ila ni Afrika nzima kuwa vipaji halisi huwa vinasahaulika muda mwingine, hapo unapoishi hauna watu ambao unawaona wana vipaji flani ila hawapo sehemu husika!? Bila shaka watakuwepo, so Mkuu achana na maneno ya wanadamu.

-Kama unaweza ukafanya shughuli nyingine ya kukuingizia kipato basi fanya tu Mkuu! Katika maisha akili yako isifungwe sehemu moja au isifungwe tu ndani ya box na kushindwa kufikiria nje ya Box.
Asante sana kwa ushauri wako miuu,nimeuchukua na naufanyia kazi
 
Acha uvivu miaka 27 bado una mda wa kusoma nenda shule kasome utaonekana tu kama una vigezo. Hii tabia ya kukimbia shule na kuanza kupenda vya bure na kuchagua kazi itawagharimu siku moja.
Sijakimbia shule mkuu. Ni mfumo wa maisha tu.

Ila kuhusu ushauri wako wa kurudi shule nitaufanyia kazi
 
Habarini wakuu.

Mimi ni memba mpya(kwenye kuanzisha uzi) ila ni memba wa muda kama shabiki wa JF.
Huu ni uzi wangu wa kwanza kuuanzisha(mnisamehe kama kuna mahali nitakosea)

Turudi kwenye maada..

Siku nyingi(kabla sijawa memba wa jf) nimekuwa nikifuatilia sana masuala mazima ya kiusalama kupitia movie na magazeti,na baada ya kupakua app ya JF nilikutana na maada mbal mbal zinazohusu maswala mazima ama story zinazohusu usalama.

Baada ya kuendelea kufuatilia na kusoma kila nnachokutana nacho na kinahusu usalama,niliweza kufunguka kiakili na kimawazo kuhusu swala zima la usalama.

Miongon mwa vitu vilivyonifungua akili ni pamoja ya namna hawa watu(mashushushu) wanavyopatikana,ikiwa ni pamoja na mashulen na kupitia vyombo mbal mbal vya usalama kama JKT n.k

Baada ya kuwa nimefunguka kiakili kuhusu jambo hili ,nilikata tamaa na kuona siwez tena kuwa shushushu kwa sababu sipo shule,na siwez tena kwenda JKT kwa maana umri umeshaenda(nna miaka 27 na elimu yangu ni kidato cha 4).

Lakini nilijipa moyo na sikujidekeza kwa kuendelea kukata tamaa,na badala yake niliendela kufuatilia maada mbali mbali na historia mbali mbali za kijasusi kupitia hapa hapa JF kama maada za mkuu The bold na za watu wengine wengi.

Sasa bas leo nimeamua kuvunja ukimya na kuamua kuja kwenu wana jamvi na kuwaomba msaada wa kimawazo na ushauri wa nn nifanye ama nn nifuate ili niweze kuwa miongoni mwa hawa watu wa usalama(TISS) ama kama kuna kikosi kingine cha kiusalama. Nikimaanisha nitaingia vipi ndani ya 18 ya hawa jamaa ili wanichukue na mm?

Nafahamu kuwa ni ishu ya siri na ni ishu ambayo sio ya kuweka hadharan,kama kuna mambo ya hadharan mtanipatia,na kama kuna ushauri wa sir bas hata PM nitaupokea pia.

Mm ni mzarendo na ninafaham hii kazi inahitaji moyo na unahitaji uzarendo pia,katika hili hakuna shida.

Naipenda nchi yangu TANZANIA na nipo tayal kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote.

Nawasilisha hoja,naombeni msaada wenu.
Na naomba radhi sehemu yeyote nitakayokuwa nimekosea.

Ukitaka kuwa usalama wa Taifa. Uwe mnafiki mnafiki. Na unabidi kuangalia maana kwa siku hizi wanaweza wakakumaliza kabla ya kufikia ndoto zako. Ok. Kuwa usalama wa Taifa sio kitu cha kusomea moja kwa moja ukifika level flani ya uongozi kidogo kidogo unapelekwa kozi kwa ajili ya usalama na uongozi wa Nchi. So to be Usalama wa taifa mara nyingi ni Mchakato na sio post moja kwa moja kwenda kusomea.
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Tengeneza counterintelligence agency yako ujiajiri, labda unaweza kuwa Private Inspector Sherlock Holmes wa karne hii...au Joram Kiango.

Kuwa shushu ni zaidi ya kuwa na shauku kuajiriwa TISS, hii zaidi ipo katika character yako na maisha ya kila siku. Kamsome mtu anaitwa Sherlock Holmes wikipedia despite ni myth lakini utapata picha. I know people who are interested too (me included) ingawa sina interest tena, ilifika wakati nilipenda niache shule niende usalama na meeting ikawa arranged but my relative wakanishauri sana niache nikawasikiliza.

Kama waliochangia wengine, hii kazi ni ya kimatabaka zaidi. Mara chache sana wanachukua watu outside their cycle (relatives) ingawa nafasi ipo, inabid uwe distinctive in certain spheres maana kuna test huwa lazima ufanye wakati wa enrolment.

Bottom line: Kama kweli una moto ndani yako (desire) usiuache uzime, jipime pia unaweza kuwa unapenda kitu ila huwezi. Sio lazima uwe na elimu ya juu, tafiti zinaonyesha watu wenye akili sana huwa hawamalizi project wanayofanya ikiwa inatumia muda mrefu sana, mfano mzuri ni Edward Snowden kila aliefanya nae kazi anadai ni "genius among geniuses" lakini hajawai kupata degree wala masters maana alikua akiaanza kusoma ikifika katikati anaacha pia kuna majimbo marekani hayaajiri mtu mwenye IQ zaid ya 135 kitengo cha polisi kwasababu wana matatizo ya "concentration"- hawawezi kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu.

Asante
Bro leo umeniongezea kitu sana.
 
I hope nia yako sio kusumbua wenzako mtaani na kuwauliza "unajua mimi ni nani"? au kugoma kulipa fine za traffic kisa wewe ni usalama wa taifa, au kuweka bastola kwenye meza bar!!!!...unatakiwa uwe mzalendo-humble/down to earth, msikivu, mwenye kifua kizito na 'fairly' intelligent...darasa sio kigezo prkeyake, wako mpaka darasa la saba...
Cha ziada, hakikisha hujawai kuiba hata kuku huko kijijini kwenu maana watakuja hadi huko kukufanyia screening/background check....goodluck
Kama hii ipo niko disqualified nilikua Mwizi sana utotoni! ha!ha!
 
I hope nia yako sio kusumbua wenzako mtaani na kuwauliza "unajua mimi ni nani"? au kugoma kulipa fine za traffic kisa wewe ni usalama wa taifa, au kuweka bastola kwenye meza bar!!!!...unatakiwa uwe mzalendo-humble/down to earth, msikivu, mwenye kifua kizito na 'fairly' intelligent...darasa sio kigezo prkeyake, wako mpaka darasa la saba...
Cha ziada, hakikisha hujawai kuiba hata kuku huko kijijini kwenu maana watakuja hadi huko kukufanyia screening/background check....goodluck
Heheheh au awe hajawahi kubaka hata bata!![emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom