Nataka kuoa lakini sijapata wa kunifaa………….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,331
Bila shaka hata wewe umeshawahi kukutana na kauli kama hii kutoka kwa wanaume, wengi wao wakiwa ni wale ambao umri unazidi kusonga lakini wakiwa bado hawajapata wenza wa kuoa na kujenga familia. Wengi huamini kwamba, kuna mwanamke mahali, ambaye hana kasoro na atakuja kutana naye siku moja.

Wengine wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto. Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilvyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza , tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa. Kwa baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa.

Zamani, kuoa ilikuwa ni kama lazima na mtu ambaye angefikisha umri fulani bila kuoa angelaumiwa na kulaumiwa sana na jamii. Hata kuaminika kwake kungekuwa ni kwa mashaka. Siku hizi suala hili ni la mtu binafsi, siyo la jamii tena. Kwenye miaka ya 1970 wanaume wote wenye umri wa miaka 25 walikuwa tayari wameoa. Siku hizi, umri wa kuoa umefikia miaka kati ya 28 dadi 30. Hata wanaooa katika umri huo, ni chini kabisa ya nusu.

Wale wanaokaa pamoja kwa muda mrefu kama wapenzi , imebainika kwamba, huwa hawaji kuoana baadaye. Kinachotokea ni mwanaume kuoa mwanamke mwingine. Tafiti zinaonesha kwamba,wanawake wengi hivi sasa huishi kwanza na hawara au rafiki zao wa kiume kabla hawajaolewa. Kisa ni kwamba, wanaume hao wanaoishi nao, wanajaribu ndoa, au kufanya ndoa ya majaribio kama wanavyoita.
Wanapoishi pamoja bila ndoa, kichwani kwa mwanamke kuna kitu kinamwambia kwamba, 'huo ni ushindi, kwani ndoa itafungwa,' wakati kwa mwanaume anajua basi, maisha ndiyo hayo na hakuna haja ya ndoa tena.
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,331
Kwanini wanaokaa wapenzi muda mrefu hawaoani?

Kukujibu swali lako inahitaji thread inayojitegemea..............lakini naweza tu kutoa angalizo:
Kama ukikuta mwanaume amekaa na mwanamke kinyumba muda mrefu bila kufunga ndoa. na mwanaume huyo anao uwezo huo ila hataki tu, kwa sababu anazozijua mwenyewe, basi hapo ujue kwamba kuna walakini........... inawezekana huyo bwana kuna sifa au vigezo anavitafuta na huyo mwanamke hana au mwanamke kwa upande wake ana walakini, kwa maana ameshindwa kukidhi sifa na vigezo anayotaka huyo mpenzi wake...
Mkumbuke kwamba mara nyingi wanaume hutongoza wanawake kwa sifa za nje kwanza na wanapoingia kwenye uhusiano ndipo anapoanza kuziona kasoro na hii inatokana na wanaume wengi kupenda kuwaoa mama zao!............... ajabu eh!
Ni hivi, wanaume wengi huvutiwa na wanawake wenye sifa kama za mama zao, inawezekana ikawa ni tabia au umbile au kitu chochote, lakini kwa kifupi ni kwamba kuna sifa za mama zao ambazo huzitumia kama reference katika kuchagua mwenza..............lakini wengi huwa hawajui kwamba huwa wanafanya hivyo......... hawajui kwa sababu hilo ni swala la kimaumbile zaidi........... na ndio maana watu husema watu wakioana na kuishi muda mrefu hufanana........... hapo itategemea mwanaume alimchangua mkewe kwa kuzingatia vigezo gani kutoka kwa mama yake........... kama ni sura, inawezekana wakafanana somehow na kama ni tabia hivyo hivyo................

We chunguza tu, utauona ukweli huu......... hata kwa wanawake ni hivyo hivyo..........rejea thread yangu ya "Mabinti hawa huolewa na Baba zao"
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Ukiona mtu mzima anakuambia bado anachagua wa kumwoa ujue huyo ana wapenzi wengi kama mbunzi, tena utakuta wengi wao wake za watu!
 

the grate

JF-Expert Member
Sep 24, 2011
204
36
kuoa hakuhitaji papara jaman ni moja kati ya maamuzi mazito ambayo 2napaswa kufanya maishani thats why watu wengi nowadays inawachukua muda mrefu kuoa..mie after 4years naoa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom