Nataka kununua mlima, taratibu zikoje?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,166
7,941
Ndugu wasomaji wa JF,

Kuna uwekezaji mmoja mkubwa naamini unaoweza kuleta manufaa makubwa siyo tu kwangu binafsi lakini pia kwa taifa kwa ujumla. Sitaeleza sana wazo lenyewe kwa sababu zinazoeleweka ila niseme tu ni uwekezaji unaohitajika kufanyikia mlimani.

Swali langu, taratibu za kununua na kumiliki mlima ziko sawa na zile za kununua na kumiliki ardhi ya kawaida au ziko tofauti? Tanzania tuna tatizo la kutoheshimu sana mawazo ya watu, yawe ya kibiashara au ya kiubunifu lakini hata mawazo binafsi ya kujieleza kwa hiyo hili wazo langu la uwekezaji badala ya kulipeleka huko serikalini ningependa kulitekeleza mwenyewe kwa nguvu zangu halafu tutajua mbele ya safari tutashirikiana vipi.

Nipeni mwongozo.
 
Unatufokea?
Milembeee kumevujwaa geti la njee jana usiku guyz tuwe makini sana nasisistiza tena guzsss tuwe makiniii........
Watu kama nyie ndiyo nimewaongelea hapo mwanzo wa uzi, wakwamishaji wa harakati za watu. Mtakuja na mizaha, kejeli na vikwazo vingine kisa tu mtu amekuja na mtazamo, wazo au mipango ya maisha tofauti na yako.
 
Watu kama nyie ndiyo nimewaongelea hapo mwanzo wa uzi, wakwamishaji wa harakati za watu. Mtakuja na mizaha, kejeli na vikwazo vingine kisa tu mtu amekuja na mtazamo, wazo au mipango ya maisha tofauti na yako.
Kabisa.
Badala ya ushauri ni kejeli.
 
Back
Top Bottom