Wanajamvi, ni kama wiki tatu hivi tumebahatika kupata mtoto wa kwanza lkn kabla wife hajajifungua nilimpeleka kwa mama yangu kwaajili ya huduma baada ya kujifungua, ndo ilikua mara yake ya kwanza kwenda kuishi na mama mkwe, cha ajabu kwa kipindi chote alichokaa nae ameonesha utovu wa nidhamu mkubwa (japo mama haja lalamika wala kusema chochote mengi nimejionea mwenyewe maana nilikuwepo). Nikisema kuandika kila kitu naweza jaza zaidi ya page 2 maana show imeanza kitambo kidogo.
Hivyo nimedhamilia kuachananae muda tu atakapo pata nguvu. Hivyo wanaojua sheria za ndoa na jamii naomba mnijuze ni sheria gani inaweza kunibana ktk hayo maamuzi yangu.
Naomba kurudia tena NIMESHAFANYA MAAMUZI MWENYEWE sihitaji ushauri kwa hilo isipokua utaratibu wa kisheria tu
Asante nawasilisha tafadhali.
Ndugu Fedora!
Kila Jambo ni wakati!
Wakati wa tukio na wakati wa onyo ulilolitoa hadi kupelekea Mke kukujibu jeuri Haukuwa wakati sahihi!
Kwanza mwili wa mwanamke anapokuwa mjamzito na baada ya kujifungua kunakuwa na mabadiliko ya kibailojia ambayo hupelekea mabadiliko ya homoni.
Zingatia Mkeo amejifungua mtoto wa kwanza ambapo kwenye tafiti na hospitali nyingi imedhihirika kwamba wanawake wanaojifungua mara ya kwanza ni rahisi kupata aina ya mfadhaiko wa kiakili unaoitwa mtoto bluu(Babies Blue) ambayo ni kawaida na huchukua siku chache na hali ya mzazi kuimarika ,Lakini kuna wazazi wanaopata hali ya huzuni ya kujifungua(Postnatal Depression) na hujisikia wenye huzuni,kuchoka na mabadiliko ya kiakili na kuna wengine wanaoishia kupata mtindio wa kiakili baada ya kujifungua(Puerperal Psychosis)uliosababisha na mabadiliko ya kibaiolojia baada ya kujifungua.
Wanawake wakiwa ktk hali hii wanapambana kurudia hali yao ya kawaida lkn wanashidwa wanakuwa na huzuni,kuchoka,hasira na na hata kuwa kama kichaa na watu wa karibu wanaweza ona ni jeuri iliyopitiliza tu.
Nakuomba tafuta wakati wa kumpeleka Mkeo kwa Daktari wakamchunguze badala ya kufikiria talaka ndiyo suluhisho.Sisi wanaume tungebebeshwa mimba miezi mitatu nafikiri tungeona adha wanazopitia Mama zetu,dada zetu,wake zetu na wanawake wote na kuheshimu wake zetu wanaochukua jukumu hilo gumu na kutupa faraja kwa kuitwa baba na mzazi. Halafu kingine unapaswa kuelewa mkeo yuko ktk mazingira mapya vile vile ukweni na wewe unatakiwa uwe kiungo muhimu baina ya mkeo na mama yako,sio tena umeenda kwa mama basi mama anachukua madaraka ya kukuongoza wewe na mkeo,unatakiwa usimame na mkeo ili asijisikie mpweke ukweni na uwe kiunganishi kati familia yako mpya na ya asili.Tafuta wakati sahihi kaa na mkeo baada ya kujua kiini hasa cha tatizo na wewe na mkeo mumuombe mama msamaha hata kama yaliyotokea yalisababishwa na ugonjwa,Jukumu la kuomba msamaha kwa mama ni lenu wote na usijitenge ukajiona si kosa lako.Huyo ni mkeo na wewe ndiye uliyempeleka kwa mama yako na natumai wazazi ni waelewa na watasamehe!Nawaombea Kila la kheri na Mwenyezi Mungu awaongoze,Amen!
Swali la haraka kwanini ulingojea mpaka mkeo awe ktk siku za mwisho za kujifungua ndiyo umpeleke kwenu?Je tangu mmekuwa wana ndoa au wachumba ni mara ngapi ulimpeleka kwenu?