Nataka kumuacha mke wangu

Nataka kumuacha mke wangu

mwenzangu kama amezidi bwaga manyanga......wote tuna tabia mbaya ila wengine ni extreme....anayway mie nakubaliana na huyo aliesema mkae ndugu wa pande zote mbili mtafute suluhu ikishindikana ndio muachane,ila umetuambia udhaifu wa mkeo, wa mama yako unaujua??? au ndio unakuwa loyal hata kama unajua kabisaa mama yako ndie chanzo hapa?:lol::lol::lol::lol:
 
Siku nyingine ukitulia unaandika mambo ya maana sana yaliyojaa hekima na busara tele. Sijui kwanini hupenda kujitoa ufahamu ulionao.

Hebu kaa nae chini uzungumze nae..na umueleze ukweli alipo kosea na ikiwezekana ajirekebishe na akaombe msamaha! Naona kama umeharakisha sana labda kama hii si sababu ya pekee!Unajuaje hayo matatizo hayaku sababishwa na hali yake?

Yani unataka kuvunja ndoa kwa sababu rahisi namna hii? Mbona ndoa yenu inarekebishika kama sababu ni hii pekee? Tafuta wakubwa wako ,baba,mama na wakwe na mkeo mkae muongee myamalize! Kuvunja ndoa si rahisi namna hii..hatu ukienda popote wata shangaa sana kama hii ndio sababu!

Hebu kaa na mkeo muongee hii ni sababu dhaifu sana kuvunja ndoa msamehe msonge mbele..yani nguvu uliyotumia kufunga ndoa ivunjwe kwa sababu hii?Utatumia miaka kumi kuvunja ndoa kwa sababu hii!

Kaa chini myaongee!
 
FEDORA Uamuzi wako ndio mbaya sana/ mgumu sana lakini kwa baadhi tu ya majibu yako niliyoyapitia inonekana kuwa kichwani ZIMO,, Busara yako inonekana sana tu,, ebu tafakari ikibidi kabla ya huo uamuzi washirikishe ndugu wa karibu pande zote kwanza uone matokeo ikiwem onyo kali mbele ya wadau wote

Asante kwa muda wako, hii nimei-note mahali kwaajili ya reference baadae
 
naona unafanya maskhara na uzazi eeh. Mimba na uzazi ni kitu kikubwa. vinakuja na hormones kubadilika badilika na usipoangalia zina-create long term problems. hapo mkeo anahitaji support ya kisaikolojia, emotional, etc. tatizo mijianaume ya kibongo haitaki kujielimisha na mambo haya. MSAIDIE MKEO ACHA KUBWABWAJA!

Excellent!
 
Kwenda zako ukute mama yako ndio moto anauwasha ukiwa haupo ukiwepo anauzima,mama wakwe na wifi hua na midomo sana hata wake pia sikatai

Hapa naona unajaji kwa kutumia general concept, Tafadhali ukipata muda naomba upitie post chache za nyuma, unaweza kupata picha.
 
we una sababu zako tu zingine
iyo unayotwambia siyo sababu ya kumuacha mke
hata mahakama aiwezi kutoa talaka kwa sababu kama yako
labda umwache kienyeji lakini kisheria ngumu

Ntarudi kwako baada ya siku mbili au tatu acha niingie chimbo kwanza
 
Sawa weka hapa watu wakusome Mkuu, usikimbilie kuvunja ndoa kirahisi rahisi. Mke haachwi kwa kosa moja.

Nimeshafunguka kwenye post za nyuma ngoja ni copy na kupest kwako
 
nyie hamjui wanawake wenye midomo walivyo eeh
mimba kisingizio tu
mimi nkibeba mimba nakuaga kisirani nagombana na mme kila mda hadi nyumba nahama simtaki
ila si kufkia kutukana wakubwa zangu jamani
mnatetea ujinga!! hv wangetukanwa wazazi wenu mngejiskiaje...?!!
 
Ulioa kwa ajili ya mama yako? Acha ufala

Hebu Jaribuni kuwa waungwana. Kwani hata kama hajaona kwa ajili ya mama yake ndio aone mama yake anatukanwa afurahie? Mnachokifanya ni kujaribu kuinusuru ndoa ya mwenzenu sio kitu kibaya ni sawa kabisa ingawaje hajaomba ushauri isipokuwa ameuliza sheria inasemaje katika hilo la kumuacha mke kwa makosa aliyoyataja.

Jambo alilolifanya mkeo kweli sio la busara kabisa. Maana wote wenye akili timamu tunaelewa kuwa mzazi wa mwenzio ni kama mzazi wako kwa hiyo unatakiwa kumpa heshima tena ya ziada. Na ili familia yako iwe na amani ni lazima heshima iwepo. Je mapenzi yatatoka wapi utakapoona mama yako anatusiwa mbele yako? Lazima tukubaliane kuwa alilolifanya sio jambo jema.

Kama mtaombana msamaha ni sawa. Lakini pia kwenda kumwangukia mkwewe ni lazima.

Lakini pia ukimuacha sitashangaa kwa kuwa yapo mengi ambayo umesema mkeo ameyafanya lakini hujayaweka wazi hiyo ni kutokana na sababu unazozijua mwenyewe. Lakini katika kufanya maamuzi hayo pia uwe makini ukizingatia vigezo vyote vilivyopo na vile vile hakikisha umejua sheria inasemaje.

Ushauri wangu kwa wanawake: tubadilike zamani wanaume ndio walikuwa wana kila sifa mbaya unazozijua lakini sasa hivi ni wanawake. Wanawake tumekuwa tunajiamini sana hasa tunapokuwa tayari tumeingia katika ndoa ndio mtu anafyatua kucha alizokuwa amezificha.

Na wachangiaji mada hebu someni mada kwa ufasaha kabla hujachangia uelewe kwanza. Sio watu wanaropoka tu.
 
hiyo tabia aliyoionesha huwa ni kipindi alichokuwa na mimba tu au hata kabla?
 
Hebu Jaribuni kuwa waungwana. Kwani hata kama hajaona kwa ajili ya mama yake ndio aone mama yake anatukanwa afurahie? Mnachokifanya ni kujaribu kuinusuru ndoa ya mwenzenu sio kitu kibaya ni sawa kabisa ingawaje hajaomba ushauri isipokuwa ameuliza sheria inasemaje katika hilo la kumuacha mke kwa makosa aliyoyataja.

Jambo alilolifanya mkeo kweli sio la busara kabisa. Maana wote wenye akili timamu tunaelewa kuwa mzazi wa mwenzio ni kama mzazi wako kwa hiyo unatakiwa kumpa heshima tena ya ziada. Na ili familia yako iwe na amani ni lazima heshima iwepo. Je mapenzi yatatoka wapi utakapoona mama yako anatusiwa mbele yako? Lazima tukubaliane kuwa alilolifanya sio jambo jema.

Lakini pia ukimuacha sitashangaa kwa kuwa yapo mengi ambayo umesema mkeo ameyafanya lakini hujayaweka wazi hiyo ni kutokana na sababu unazozijua mwenyewe. Lakini katika kufanya maamuzi hayo pia uwe makini ukizingatia vigezo vyote vilivyopo na vile vile hakikisha umejua sheria inasemaje.

Ushauri wangu kwa wanawake: tubadilike zamani wanaume ndio walikuwa wana kila sifa mbaya unazozijua lakini sasa hivi ni wanawake. Wanawake tumekuwa tunajiamini sana hasa tunapokuwa tayari tumeingia katika ndoa ndio mtu anafyatua kucha alizokuwa amezificha.

Na wachangiaji mada hebu someni mada kwa ufasaha kabla hujachangia uelewe kwanza. Sio watu wanaropoka tu.

Nathamini sana muda wako ulioutumia kuandika post hii ndefu na iliyo pangika vizuri, nashukuru pia kwa umakini wako katika kutambua nn kinahitajika lakini pia kunisaidia kutoa darasa kwa wengine, hapa kuna kitu cha kujifunza ingawaje wengi mnaniona -----
 
For real?!!! Unataka kumuacha mkeo kwa ajili ya niniiii? Hebu kwanza nenda soma wamama wajawazito wanapitia vitu gani wakiwa kwenye hiyo hali, no wonder mama yako hakusema kitu sababu naye aliishapitia wakati kakubeba wewe. Acha ujinga, unless una yako mengine unamtafutia sababu. Duhhh, hii ya leo kali.
 
Tukikuelekeza namna ya kumuacha huyo wa kwanza ndiyo itakuwa muendelezo kwa watakaofuata,hutooa tena au
nawe utajirudisha kwa wazazi wako mkuu?
 
Una lako jambo. Inaonekana wewe ndio mwenye domo chafu, inawezekana hata ulikua humjali huyo mzazi mwenzako...mfewwww.

Nashukuru kwakua enapata majibu mwenyewe kadri unavyo zidi kusoma hiz post. Endelea kusoma kisha karibu tena kwa post ingine
 
Back
Top Bottom