Asante sana kwa huu ufafanuzi mzuri japo hayo yote nimekwisha yaelezea vizuri acha nirudie tena kwa kuheshimu jitihada zako na kwa faida ya wengine.
1. Natambua kua mke hupelekwa kwao kwa huduma baada ya kujifungua, lkn kwao walikataa kwa hoja ya mila zao haziruhusu.
2. Hakupaswa kufanya shughuli yoyote ambayo mjamzito hapaswi kufanya au hata kama hajisikii, nilimuongezea muhudumu mwingine wa kumsaidia mbali na mama
3. Mpaka leo wazazi wangu hawajasema kama anatabia mbaya ila nimejionea mwenyewe hata kabla ya ujauzito na wakati wa ujauzito, maana nilikuwepo wiki 1 kabla hajajifungua na kuendelea kuwepo kwa wiki nyingine 2 baada ya kujifungua
4. Nimekua nikimuelekeza na kumuongoza juu ya hiyo tabia yake mbaya kwa muda mrefu bila mafanikio, tukio hili la sasa ni kama climax ya mfululizo wa uozo mwingi alioanza kuufanya muda mrefu.