Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Kabla ya kumuoa mwanamke hakikisha moyo wako umeridhia, ndo maana dini zote ukiwa unafungishwa ndoa unaulizwa mara 3 kama umeridhia kumuoa ile siyo bahati mbaya ina maana kubwa, kama huna hisia nae achana nae.

Wanawake wanatakiwa wabadilike waache kujirahisisha unatumika miaka mi 5 mwisho unaachwa kama hivi.
 
Hua
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano. Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja. Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.

Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha. Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana. Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.

Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae. Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.

Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana JF?
Huna hisia nae kivipi
 
Uliwezaje kukaa Nae miaka mitano kwenye mahusiano kama huna his nae
 
Mkuu kuishi na mtu ambaye huna hisia nae ni mtihani sana. Bora umueleze mapema aelewe na muachane kabla hamjafika mbali..ila je tangu huko awali ulikua huna hisia nae? Au kuna mambo yamevuruga hisia zako?
yeyote yule mkianza mapenzi yanakua yamoto lakini baada ya miaka mi4, 5 au 6 ya kuishi pamoja hisia na mapenzi hupungua. kwa hiyo hata atafute mwengine baada ya miaka mitano ataleta uzi hapa tena kuwa hana hisia naye.
 
Muache tu mtoto wa watu a
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano. Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja. Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.

Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha. Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana. Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.

Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae. Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.

Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana JF?
Muache tu mtoto wa watu akutane Na mwanaume anaempenda wewe sio MTU sahihi Kwake hata ukimuoa utamtesa let her go please atakutana Na anaempenda kuliko wewe MTU mzima kileja
 
Siyo kumuonea huruma waka kumfanyia hisani.Anapaswa abebe jukumu la kuwa mwenza kwa akili nyingi.Kama wote tukiamua tu kusema hisia kwa wenza wetu zimeisha,kuna ndoa au mahusiano yatabaki salama?Mapenzi,ndoa au mahusiano ni hesabu,mipango,uchaguzi bora,uvumilivu,unyenyekevu,utu,dhamira njema,nia thabiti vinavyoongozwa na upendo maridhawa.Mapenzi siyo sukari tupu kwamba utailamba kwa furaha kila siku.Atulie na kutafakari.
Exactly,hisia ni suala la upside and down.hazipo consistent
 
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano. Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja. Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.

Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha. Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana. Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.

Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae. Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.

Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana JF?
Makubaliano ya mwanzo kabisa ya mwanamme na mwanamke kuishi pamoja kama mme na mke yana msingi sana, yakivunjwa na mmojawapo kwa hira tegemea laana na karma

Inaonyesha una vigezo vyako kwa mwanamke anayekufaa na hapo umeona huyo hajakidhi. Wengi wanaweka vipaumbele vya umbile na sura kama vigezo mahususi ( something which is partly right).

Yafaa nini mwanamke anayekutikisia maakalio makubwa, sura nzuri ila hana msaada kwa kwako? Ana kufastrate kila leo, hakuheshimu, anatoka nje ya ndoa, mvivu, roho mbaya nk

Je, huyo dada hakufai kwa lipi? Well, mwanamke usie na hisia nae means humpendi. Amekukosea nini? Mwenye shida ni wewe, so ukimwacha karma ni kitu dhahiri, utamkumbuka huyo mwanamke.

So nadhan umri wako una imply hili uliloleta hapa. That is nosense my dear
 
Kinachoniuma umemkula mdada wa watu weeeew.
Miaka mitano.
Sasa unataka kumuacha.

Bora sisi tunaeopiga one time halafu tunaacha, wanaliaga ila hatuwachakazi.
 
Kuna kitu cha muhimu sana hujakisema:

Huyu binti hujamaliza hisia kwake from nowhere. Umekaa naye miaka mitano ukimlala na bila shaka umeshuhudia mabadiliko yake ya kimaumbile. Bila shaka baada ya huo ujauzito wake mwili wake umebadilika. Pengine matiti yake yamelala yoo. Kakitambi ka kishikaji kameanza kuchomoza; na ile figure matata namba 8 iliyokuwa inakupagawisha imeanza kupotea na ukimwangalia miaka mitano huko mbele unaona kabisa kuwa atakuwa ameshachakaa wakati wewe kwanza ndiyo utakuwa kwenye peak (33!). Na hili linakuogofya sana!

Na kama hili halitoshi, naamini una kimchepuko chako kinachokupagawisha huko nje. Kibinti kibichi moto kilimbwende! Kifuani bado saa sita. Ngozi nyororo usoni na macho ya kuita. Ikulu kumenona bado kubichi kunanata hatari futa kama lote. Na huyu rafiki yako wa miaka mitano unamuona si kitu tena! What a mirage!

Na kwa vile hisia huwa hazilazimishwi, hata ukijilazimisha kubaki na huyu binti mwema mliyevumiliana naye kwa miaka mitano haitasaidia kitu maana ni mzigo mzito sana kuishi na mtu ambaye huna hisia naye hasa ukizingatia kwamba hamna hata watoto wa angalau kuwaunga pamoja kihisia na kidamu!

Ushauri wangu kwa sasa ni huu: Usifanye papara. Kaa utulie. Fanya tathmini ya mambo yote na utakakokuwa baada ya miaka mitano mingine ijayo. Je, utakuwa na furaha bila ya huyu rafiki yako ambaye kwa miaka hii mitano mmepambana pamoja? Ni nini hasa unachokitaka kwa mwanamke/mke/mama watoto wako? Ni uzuri wa umbo na sura au ni mwanamke mwema mpambanaji ambaye atakuwa mke mwema kwako na kuwa mama bora kwa malaika ambao Mungu Atawapa? Huyu binti uliyenaye anaangukia wapi katika mzani wako wa waifu matirio?

Na kama wewe siyo mbinafsi jaribu pia kumfikiria huyu binti wa watu. Miaka mitano mizima. Unaishi naye kinyumba. Amejitolea kwako kimwili, kisaikolojia na hata kiroho. Na leo unataka kumtupa tu kama ganda la muwa lilomaliza utamu. Unafikiri atakuwa na ujasiri wa kwenda kuikabili dunia peke yake, akasimama wima na kuanza safari yake ya kutafuta mwenza wa maisha na familia upya? Ungekuwa wewe ndiye yeye ungeweza? Angekuwa ni binti au dada yako ungependa apitie huku unakotaka kumpitisha?

Ukishatulia sasa na kufanya tathmini hii basi amua mwenyewe. Kama kweli hisia zitakuwa ni butu basi mwambie tu ukweli kuwa huwezi kuendelea naye lakini utaendelea kumsaidia mpaka atakaposimama tena. Ataumia sana lakini pengine hii ndiyo njia bora kuliko zingine zote.

Na unajua nini? Kama huyu binti hajakukosea kitu. Kwamba yuko loyal kwako na amewekeza kwako kabisa kabisa kwa miaka hii yote mitano. Utakuja kumkumbuka sana na kujuta mno. Na wakati huo naamini tayari atakuwa keshatwaliwa na mwanaume wa kweli atakayempenda na kumpa furaha.

Naamini kila mtu atapata anachokitafuta maana dunia ni hii hii na maisha ni haya haya.

Mungu na Akusaidie bwana mdogo maana, talking from experience, fanya makosa yooooote lakini usije ukafanya kosa la kuchagua mwenza wa hovyo. Utaangamia wewe pamoja na kizazi chako chote!
 
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano. Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja. Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.

Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha. Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana. Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.

Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae. Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.

Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana JF?
Acha ujinga.

Mwanamke ndiye huwa anatumia hisia kwenye mahusiano na hisia kwake ni kila kitu.

Ila sisi wanaume tunaishi na mwanamke aliyetiyari kusubmit, kuzaa, na kulea watoto wetu.
 
Hiyo hali huwa inatokea wala sikushangai kuna wakati unajihisi huna hisia na mtu uliyenaye lakini ni kipindi tu cha muda ukiendelea kuwa mvumilivu.
Hiyo hali baadaye inakuja inapotea na utarudi kawaida. Ndio wakati mgumu sana kwa mwanaume kufanya maamuzi ya kuwa na mwenza. Kuna wakati mimi nilifikiria hata kwenda upadre wakati huo nipo safarini kutoka kutoa barua ya posa. Pia unaweza ukaliweka suala lako katika Imani ili nguvu nyingine itumike katika kufanya maamuzi chanya/mazuri.
 
Back
Top Bottom