Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Sielewi nini kimenikuta natamani hata aniroge nianze kumpenda upya.
Hiyo inatokana na huna bond naye ya maana,huyo mtoto marehemu angekuwa hai leo usingekuwa na mawazo haya coz mkishakuwa wazazi kama zile tabia za kishenzi shenzi mwanamke hana maisha yanakuwa very simple ndani ya nyumba.

Cha kufanya inabidi wewe kama mwanaume uangalie angle ya mazuri yake,kama ana tabia tulivu siyo mapepe kaeni mkubaliane mzae mtoto nyumba itatulia.mwanaume hana sifa ya kupenda ana sifa ya kujali kutokana na anayotendewa na mkewe so kama anaenda kama unavyotaka huyo ndiyo mkeo ishi nae.
 
Kuna ndoa moja bora wameachana na talaka isha toka. Tusilazimishe ndoa jamani.

Parties yaan mlalamikaji alikuwa akimlalamikia mme hivi
1. Wanashiriki tendo la ndoa siku za kupata mimba tu, mimba iliingia watakutana tena mtoto anaefafa.

2. Wakiwa wanashiriki tendo hakuna cha kuandaana, mwanaume akimaliza anamsukukuma kuwa asimsumbue.

3.mwanamke akienda chooni, mwanaume analalamika kuwa anamaliza muda mwingi anaflashi maji mengi bili inakuja kubwa, yaaani hapa nilicheka mpaka mpavu zikauma.🤣🤣🤣

4.wameishi miaka 25 wana watoto wanne ndani ya mika 25 mwanamke anasema kama walishiriki tendo haizidi mara 10, mwanaume anakuja siku za hatari tu. Ahaaaa.
5. Siku moja nikaongea na mwanaume nimsikilize ahaaa akaniambia hakuwahi kuvutiwa nae ana mdomo, hamuheshimu, anashukuru mwanamke kaomba talaka sasa napumua.🤭😅😅😅
 
Acha upuuzi, kwanini umpotezee muda na uchezee hisia zake na mwili wake kwa muda wote huo kias cha kumtia mimba nk...

Ebu kua na adabu K zipo tu za kila rangi hata ukimwacha huyo uliemchakaza na kumchoka utatafuta zingine utazichoka pia.

Kijana mchezeaji mbinafs sana wewe, ebu jifunze kua na Utu "Karma is Real."
 
Ikiwa AKILI yako na HISIA hazipo kwake unaweza kumwambia tu kuwa haupo tayari kuoa kutokana na mambo yanayoendelea ktk MAISHA yako.

usiogope wala usiangalia muda ambao umekuwa naye pamoja.

Ikiwa she is a decent woman I hope she will get a right one

As well if you a good man you will get a Right one.

Don't live with regret.

Hakikisha maamuzi yako yoyote unayofanya hayamuumizi MTU yawe katika both side winning.
 
Sampuli za vijana wa hivi wakiambiwa wanachoweza ni kufungua lisani za kaptula na kukojoa hulalamika wametukanwa.Wanakubali kuendeshwa kwa macho na hisia mfu bila kushughulisha mbongo zao na kuitazama kesho kupitia sasa/leo.
• Ukiwaza kwa harakaharaka hapo, wameishi wote kwa miaka mitano, Mimba mwanamke imeharibika, ( kisa hana mvuto tena 🤔!!!

• Hapo atakuwa amekiona kidada kinajibinua binua hapo mtaani ndo kinamchanganya kila dakika.

• Kama angekua dada yangu ndo amemufanyia hivyo, huyo dogo ajiandae kutetwa na watu wasiojulikana ☹️☹️.
 
.........kuna kitu watu wanasahau au hawajui mara nyingi hata ndugu wnapendana sana wakiishi mbalimbali, ila siku wakiamua kuishi pamoja ndo changamoto zinaanza kuibuka, hii ni kwa sababu madhaifu na mapungufu ya mwenzio unayaexperience daily, so uvumilivu unaanza kupungua.......
........Sasa katika mahusiano unakuta mtu anasema amekaa na mwanamke miaka mitano baada ya hapo anaona hana hisia nae, no sio kwamba hana hisia nae bali ameanza kuface mapungufu ya mwenzake, ameanza kumzoea(kumuona wa kawaida) na taratibu anaanza kumchoka........
........ili kuepuka kuwachezea na kuharibu maisha ya hawa wanawake ni Bora mwanaume unapoamua kuoa au kuzaa na mwanamke basi utambue kuwa hayo hapo juu yatatokea coz mtakuwa pamoja na uwe tayari, ukiona mtu anamuacha mwanamke ambaye anadai hana shida yoyote basi yafuatayo yanahusika:
1. mwanaume ana changamoto ya afya ya
akili(mental retardation i.e zezeta)
2.maamuzi ya kuoa au kumpa mimba
mwanamke yalifanywa na kichwa cha
chini
3.presha ya kuoa ilitoka nje na sio from
within
4.licha ya kuoa, kichwa cha juu bado kinaendeleaa kufanyia assessment matako na mahipsi ya wanawake wengine, ndo mana utasikia maneno kama vile sina hisia nae, nikiwa nae kitandani navuta hisia kwingine ie kwa wenye matako.......
.......neno: tuoe tukiwa tayari na mental maturity ya kutambua ndoa sio ngono ni mahusiano yanayobeba nyanja nyingi, tunaharibu maisha ya hawa wanawake, kila familia nowadays haina baba, sio wamekufa hapana bali wameamua tu kuwaacha wanawake hao kwa kuwachokana kutokuwa na hisia nao za ngono sababu ambazo ni za kishirikina kama sio za kipumbavu, samahani kwa watakaokwazika kidogo, Asante.....
 
Jamaa umekuanae miaka 5 ukiwa na hisianae na sasahivi unaona huna hisia nae kwa akili ya kawaida hii inamaanisha hata ukimpata mwengine ukawa na hisianae ndani ya miaka kadhaa hisia zitaisha kwamaana hio utamuacha tena au.

Hisia hua zinaisha kulingana na muda unaokaa na mtu, ukioa Leo ndani ya miaka kdhaa hisia huoungua kabisa kinachobaki ni upendo na huruma, kusaidiana kulea familia hiki kitu mbona rahisi mtu mzima kuelewa wewe una umri gani.
 
Ok, achana na hao wanaokuona hauna akili sijui umemchezea bintu sijui kitu gani! Achana nao.

Hauhitaji sababu wala ruhusa kuachana na mtu.

Wala hauhitaji kutoa maelezo kwa mtu yeyote isipokuwa kwa huyo tu unaemuacha.

Usijilazimishe kuishi na mtu ambaye humtaki kwa kuhofia watu watakuonaje au kuogopa kumuumiza hisia.

Ukijilazimisha utaishi kwa majuto na pia huyo binti hatofurahia maisha na ataishi kwa mateso, maana hatopata anachotakiwa apate.

Kumsaidia mtu usiempenda ni kuachana nae, ili akapate watakaompenda.

Ninachokushauri jipe muda walau wa miezi kadhaa ukitafakari.

Ukiona bado 'humuelewi' achana nae mara moja, namna ya kuachana nae unaweza kuzingatia ushauri wa DR HAYA LAND ameeleza vizuri.

Kila la kheri na weekend njema.
 
Back
Top Bottom