Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano. Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja. Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.

Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha. Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana. Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.

Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae. Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.

Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana JF?
Siku hizi kuna mashetani yenye miili ya kibinadamu.
 
Ayo ni madhara ya zinaa Mkuu

Wanaume kama nyie ndio mnafanya wanaume wengine wenye nia nzuri kuonekana mashetani.

Yani msichana wa watu umekaa nae kipindi chote hicho na kaamua kujitoa kwako.... bahati mbaya kabeba mimba na haijawa rizki... leo unasema huna hisia nae unataka uanze upya mwenyewe. Loh!

Nikuambie tu usije ukategemea kama utafanya kitu kikasonga maana atakavyokua ananung'unika hutokaa salama wewe na hata uyo binti mpya utakae mpata utamtesa tu na izo laana zako.Alafu utaanza kusema "nimelogwa" Utajiloga mwenyewe Niseme tu... Mkataa pema pabaya panamuita.
 
Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.
Huu ndiyo uwoga wa kijinga unafanya tuishi maisha ya dhiki.... Piga chini usonge mbele na maisha , mwanamke unaishi naye wewe na siyo watu wanaowafahamu.
 
Huna michepuko mkuu, mbona hii hesabu ni rahisi sana.

Tafuta lishangazi limoja uwe na hisia nalo, unatupiamo moja mbili. Ukirudi geto lazima umuone mkeo mzuri.

Katika ushauri wote naondoka na huu mkuu [emoji1666]
 
Makubaliano ya mwanzo kabisa ya mwanamme na mwanamke kuishi pamoja kama mme na mke yana msingi sana, yakivunjwa na mmojawapo kwa hira tegemea laana na karma

Inaonyesha una vigezo vyako kwa mwanamke anayekufaa na hapo umeona huyo hajakidhi. Wengi wanaweka vipaumbele vya umbile na sura kama vigezo mahususi ( something which is partly right).

Yafaa nini mwanamke anayekutikisia maakalio makubwa, sura nzuri ila hana msaada kwa kwako? Ana kufastrate kila leo, hakuheshimu, anatoka nje ya ndoa, mvivu, roho mbaya nk

Je, huyo dada hakufai kwa lipi? Well, mwanamke usie na hisia nae means humpendi. Amekukosea nini? Mwenye shida ni wewe, so ukimwacha karma ni kitu dhahiri, utamkumbuka huyo mwanamke.

So nadhan umri wako una imply hili uliloleta hapa. That is nosense my dear

Nashukuru mkuu..naufanyia kazi ushauri wako
 
Aliwezaje kuishi na mtu miezi 60 asiye na hisia nae. Tukisema kamtumia, kamchosha na kamuondolea mvuto binti wa watu anataka kumkimbia tunakosea. Katika hili lazima gharama ihusike. Gharama ya kupoteza muda kutoka kwa Mungu au Binti.

Mazingira yetu ya kukutana yalipelekea hii khali nadhani
 
Watu humu ndani mnamlaumu jamaa kwa maamuzi hayo! Ingekua mwanamke ndie hana hisia na jamaa angelaumiwa the same??
Mimi naona jamaa asiulazimishe moyo, kwa kipindi chote cha mahusiano wote walipitia mazuri na mabaya kwa pamoja, inapotokea! Mshkaji anasema anataka kumuacha, isionekane amemuharibia dada future yake.
Mleta maada wewe anza na maisha yako mapya kuliko kuja kujilaumu when its too late. Atampata wa kwake ambae kapangiwa na Mungu
 
Uja uzito ndio ulikuwa shinikizo? Kabla ya Mimba nini kilikushinikiza kumtomb* mpaka ukampa mimba?

Vijana wa siku hizi mmekuwa wa hovyo sana.

Vingi tu ikiwemo uzuri wake upole na mengineyo.
 
Watu waliposema mkaishi kwenye shida na raha ndiyo hali unayopitia.
Mahusiano ya sasa yamevurugika sana, dunia ya sasa tunayoishi utakuja kugundua kutokuwa na hisia naye ni tatizo dogo sana.

Na tumepitia shida na raha nyingi mkuu
 
Huyu dogo inawezekana kabisa alikuwa hata matunzo hampi.

Kwanza ameanza eti anamlete geto ili watafute maisha pamoja.

Lini Mwanaume akasaidiwa maisha na Mke wake?

Huna hata mtoto ubataka pango/ kodi ya geto usaidiwe na demu?

Sijasema nasaidiwa mkuu hajanielewa labda
 
Back
Top Bottom