Poleni sana dada kwa kutendwa vibaya mungu atakulipia kwa kupa mwanaume mwaminifu wa maisha yako.siyo kweli kuwa huwezi kupata mme wapeke yako, wanaume waaminifu wapo wengi tu ila nikumwomba mungu akupe hekima na maarifa ya kumchagua mwanaume mwenye busara na hekima ya uaminifu .
Unapo chagua mchumba wakukuoa fuata sheria zote cha kuchagua mchumba mwenye hekima na upendo wakweli wakuingia katika ndoa. kigezo cha kwanza kabisa angalia tabia yake iwenzuri yenye maadili mazuri, cha pili awenaupendo wakweli kutoka moyoni, cha tatu sehemu unayokutana kwa mara ya kwanza iwesehemu yenye madili kama kanisana au msikitini isiwe baa au club, cha nne asiwe mzinzi na mpenda ngono kupindukia , cha tano aweanamjua mungu na anahofu ya mungu, cha sita awenaheshima, cha saba aweamekoma kiakiri , cha nane awenaelimu ya kujitambua yeye ni nani na nini wajibu wake, cha tisa awenimpenda maendeleo na mchapa kazi na kumi awemwaminifu . mwanaume huyo hupo kwani hata mimi niko kwenye ndoa kwa miaka kumi na tatu , ninauwezo sana kipesa lakini ni mwaminifu kwa mke wangu sijawahi kuwa na nyumba ndogo .
usichague mme kwa kutumia vigezo vya elimu, pesa, usharobaro, umaarufu wa mme,uhansome,ubishoo, uwenzo wakufanya ngono,muonekano,cheo , gari, kabila, rangi,umasikini, pesa n.k hivi vitu havina nafasi katika mapenzi ya kweli lakini kwa bahati mbaya wanawake wengi siku hizi wanachagua mwanaume kwa kutumia vigezo hivi ndiyo maana hawapati wanaume waliotulia na waminifu katika ndoa. unaweza ukamlea lakini bado akawa siyo mwaminifu kwani wanaume wanaolelewa maranyingi huwa malaya sana kwa wanawake wengine, wewe ukimpa pesa yeye anaenda kuhonga . fuata sheria za kupata mchumba bora na mwaminifu utampata wa kwako pekee yako.