Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Banjuka

JF-Expert Member
May 7, 2021
1,007
1,891
Habari za wakati huu wanajamii.

Moja kwa moja kwenye swali langu la msingi.

Nahitaji kujiunga na Updare wa Kanisa Katoliki, ila kuna baadhi ya maswali sijaweza kupata ufafanuzi wake.

1. Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?

2. Je, ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?

3. Je, kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?

Nakuombeni ufafanuzi wa kina wandugu.
 
Huo ni utume, watumwa wa utume huo wanao wito... Swali la kwanza je, wewe una wito huo au unataka?

Wito huu unahakikiwa kuanzia seminary ndogo mpaka juu huko, sio rahisi kuchukua "hoehae/mangumbalu" toka mtaani.. Je, wewe umewahi kupita kwenye malezi ya kitume?

Unataka (kadiri ya maandishi yako) kujiunga upadre, je washirika/jimbo?

Haloo, sikukatishi tamaa, lakini una asilimia 0.98% za kuupata.

Mimi sijui lolote, nimelopoka tu.
 
Kama unataka upadre wa jamii forum basi subiri majibu ya wadau ila kama una nia ya kweli ni vyema ukaenda kanisani na kukutania na padre wa miito ambaye atakujibu maswali yako yote bila wasiwasi.
Upadre naoutaka ni wa Kanisa Katoliki Mkuu.

Haya maswali nimeyaleta hapa ili kupata mwanga mahali pa kuanzia.
 
Ukifika darasa la Saba unafanya mitihani ya seminari ili kukuandaa kuingia kidato cha kwanza ,ukifaulu kwa alama wanazotaka basi unapewa fomu ya kujaza, unalipa ada zao na ndipo tunaanza kidato cha kwanza ,suala la umri ukiingia kidato cha kwanza unasoma pre_form one mwaka mmoja, mpaka unamaliza sekondari unakuwa umetumikia miaka mitano lakini pia kuna mitihani ambayo unafanya hiyo mitihani ukipata chini ya alama 50 unarudishwa nyumbani kwa maana umeshindwa kuendelea na shule hivyo kama ulianza na miaka 14 utamaliza na miaka 19.

Mwaka wa mwisho wa masomo unachagua masomo yako matatu pamoja na Bible knowledge huku ukichagua shule za kidato cha tano ambazo zinahusika na seminari za kikristo pia unatakiwa ufaulu kwa kiwango cha division one au two zile za mwanzo hivyo ukifaulu unakwenda kusoma kwa miaka miwili yaani five na six ,jumlisha miaka 19 na hii miwili inakuwa miaka 21 baada ya hapo ukifaulu unakwenda chuo kwa miaka kama 6 hivyo mpaka unamaliza unakuwa na miaka 27,28,30 na ndani ya hiyo miaka 6 ndipo unaambiwa hakuna kuona wewe utahudumia jamii tu
 
Upadre naoutaka ni wa Kanisa Katoliki Mkuu.
Haya maswali nimeyaleta hapa ili kupata mwanga mahali pa kuanzia.
Oky basi kuna mapadre wa majimbo na mapadre wa mashirika.

Je ww unapenda kuwa padre wa jimbo au shirika?

Kama unataka upadre kupitia jimbo basi naenda kanisani utaonana na mkurugenzi wa miito.

Ila kama unataka upadre wa shirika basi chagua shirika unalolitaka wasiliana nao,watakupa vigezo vyao ni rahisi tu.
 
Oky basi kuna mapadre wa majimbo na mapadre wa mashirika.

Je ww unapenda kuwa padre wa jimbo au shirika?

Kama unataka upadre kupitia jimbo basi naenda kanisani utaonana na mkurugenzi wa miito.

Ila kama unataka upadre wa shirika basi chagua shirika unalolitaka wasiliana nao,watakupa vigezo vyao ni rahisi tu.
Acha kupoteza muda.

Wa jimbo HAPATI, washirika HAFAI.

Mimi sijui lolote NIMELOPOKA TU
 
1.Ni umri gani unakuwa mwisho wa kujiunga na upadre?
Hakuna umri maalum mkuu, hata uwe na miaka 80.

2.Je ni elimu kiwango gani kinakubalika ili kuendelea na masomo ya Upadre?
Kidato cha sita kwa ufaulu wa daraja la kwanza na la pili au walau stashada (Diploma) kwa ufaulu wa walau upper second na kuendelea.

3.Je kama nilikuwa na mahausiano ambayo sikufunga Ndoa Kanisani, baadae mahusiano yakafa na tumeshapata Mtoto inakuaje?
Kama hamkufunga ndoa ya Kikatoliki unaruhusiwa lakini ulihakikishie Kanisa una utaratibu maalum utakaohakikisha mtoto anapata malezi yote (Kiuchumi) nje Kanisa.

Kila la heri mkuu.
 
Process ya vetting huwa ndefu hasa si chini ya miaka kadhaa
Siyo lazima, vetting inafanyika kipindi cha malezi ambacho ni miezi mitatu hadi mwaka kutegemeana na Jimbo au Shirika husika.

Ndiposa unaenda kusoma Philosophy, Theology unafanya Uchungaji, unakuwa Shemasi then miezi sita baaadaye unakuwa padri.

Jumla ni kati ya miaka 9 hadi 14.

Unless upate changamoto hapo katikati.
 
Back
Top Bottom