Kaka Nawapasulia mimi nakushauri ondoka tu huko usijari utapokelewa maana wanajua nyote ninyi mlihama kwa "hasira". Ila nikukumbushe tu ondoka bila kupindisha ukweli huko utokapoa, Marando sio aliyevuruga NCCR kama umeshau pandikizi la chama kule alikuwa ni A.L Mrema na alifanya kazi yake vizuri tu, ndio maana safari hii amepelekwa Vunjo akajaribu tena! Unasema unaondoka kwa Sababu Slaa anaishi na Josephine na wewe unaita huo kuwa ni udhalilishaji, aaa basi nikuambie tu kama huo we unaona ni udhalilishaji basi huujui udhalilishaji, na kwa kuwa umeonesha nia ya kuondoka huko basi karibu CCM huku tutakuonesha nini hasa maana ya udhalilishaji, labda nikupe kipande tu! Huku kwetu katibu mkuu alibaka mwanafunzi wakati akiwa mwalimu lakini sisi hatujali, mweyekiti wetu anahonga ajira za BOT na ukuu wa wilaya kwa vimada wake sisi kwetu ni poa tu, mjumbe wetu wa kamati ya maadili (wenyewe mnamuita mzee wa vijisenti) anakula shemeji yake lakini kwetu huu sio udhalilishaji! halafu we unasema Slaa kuishi na mwanamke aliyeachika kwa mumewe ni udhalilishaji! si unamjua yule mwenyekiti wa jumuiya ya wabeijing wa chama chetu, si unakumbuka alizaa na mume wa mtu, yule mzee KK
Umesema eti jamaa wakishinda unahofu ya ukabila, usogope hilo mbona ni dogo na haliwezekani, ila njoo huku kwetu CCM maana tumekwisha amua kuwa tukishinda tu Ikulu ni mali ya familia ya mwenyekiti wetu, maana hadi sasa tumekwisha kabidhi chama kwa familia yake bado serikali tu!
Njoo haraka na wala usiwaombe hao ushauri, si unajua wengi wengine walikuwa huko na waliwahi kusema kuwa wakirudi huku labda walale na mama zao!lakini leo tunao na waliondoka bila kuomba ushauri, maana wangekumbushwa kulala na mama zao, hivyo nakushauri rudi tu usiombe ushauri. Namaliza kwa kukukaribisha, KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!